mwamba c
JF-Expert Member
- Jan 2, 2017
- 690
- 2,361
Nmepanga pango la biashara,wapangaji wenzangu ni waislam,wakristo nikiwepo mm na walokole.Ndugu wadau,
Najua humu JF tupo wengi sana tuliopanga katika hizi nyumba zilizopo Uswahilini, mtasema wenyewe kama upo Uswazi. Basi narudi madani na nitaanza ni hichi kitabia kinachonikera sana mpaka roho inapasukaga ila haifi.
Umeme katika nyumba hizi hua ni ugomvi usioisha, yaani unakuta kama kuna wapangaji zaidi ya wawili panatokea choko za watu kutaka kuhesabiana vyombo vya umeme na wanakupimia matumizi kupitia midomo ooh Mara we una Friji oooh unavaa nguo smart unatumia Pasi ooh Mara juisi kila siku sana anatumalizia umeme.
Na Mara zoote Umeme ukikatika unalaumiwa mwenye kauchumi oooh bila flani huu umeme tungemaliza mwezi.
Naamua kuishia hapa ili na waswazi wenzangu waulize, waseme vijitabia hovyo tujirekebishe au tushauriane ila kaswali; "kama unaona nina vyombo vingi vya umeme nani kakuzuia usiwe navyo wewe pia?".
Changamoto kubwa tuliyonayo ni katika ulipaji wa hela ya umeme na mlinzi,mara nyng wanaotukwamisha ni hawa walokole yaan ukiwapa taarifa kuhusu ulipaji wa umeme wanakuwa wakali vbaya na wanaingia ndani wanafunga milango wanaanza kusali na kulia.Huwa najiuliza kanisani huwa wanafundishwa nn?hawajui kumkwaza mtu ni dhambi?kwann mlinzi ahatarishe maisha yake kwa kulinda mali zako kisha usimpe pesa yake?kwann wenzako watoe pesa ya umeme ww usitoe?taabu kweli