Tuliofurahia dhulma dhidi ya simba jana, ndio tunaotaka haki itendeke leo!

Baba Kiki

JF-Expert Member
May 31, 2012
1,544
940
Mimi ni shabiki kwelikweli wa soka. Natamani timu yangu ishinde kila mechi na kila kombe. Lakini pia mimi ni muumini wa haki. Napenda sheria, kanuni na taratibu zifuatwe. Napenda nidhamu ya mchezo idumishwe. Kama timu yangu ikishinda, nafurahi ikishinda kwa haki.

Lakini mashabiki wengi duniani, na hasa hapa Tanzania, wanatamani pia timu zao zishinde na ikiwezekana hata sheria zisipofuatwa kwao ni poa tu. Kama sheria zinawanyima ushindi wako tayari kujitoa fahamu na kuizika sheria, lakini fahamu zinapowarudia, wanataka tena sheria zifuatwe. FIFA ilijua shida hii ndio maana wakaja na kampeni ya fair game.

Mwaka jana wakati vita ya kugombania ubingwa wa VPL imepamba moto, Simba walifungwa kihalali uwanjani na Kagera Sugar 2-1. Wapinzani wao Yanga walifurahi mno. Meno yote 32 na Simba wakinyong'onyea wakakubali matokeo. Lakini ghalfa bin vuu, ikagundulika Kagera Sugar walimchezesha mchezaji Mohamed Fakhi akiwa na kadi 3 za njano kinyume cha kanuni. Simba walikata rufaa, na ushahidi ukawekwa hadharani, wakapewa pointi 3 na magoli 3 ya halali kabisa kutokana na kanuni. Hadi leo kila mtu anajua Fakhi alikuwa na kadi 3 za njano
Iliuma kwa Kagera Sugar, ambao walikuwa wametoa jasho, machozi na damu uwanjani kuvuna pointi 3 lakini kanuni ikawakatili.

Hivyo ndivyo ilivyo dunia nzima, usipofuata kanuni, kazi yako inakuwa bure. Azam iliwahi kunyang'anywa pointi 3, Simba waliwahi kunyang'ang'aywa pointi 3 tena dhidi ya Kagera Sugar, hata Yanga ilishawahi kunyang'anywa pointi 3 dhidi ya Coastal Union. Hakuna aliyepiga keleke kabla.

Lakini kipindi hiki cha mwaka jana wakati Malinzi ameshika hatamu, tuliona Yanga wakitumia ubabe na ushawishi wao kupitia TFF kutengua maamuzi mchana kweupe bila hata soni. Wakatumia mbinu ya kupiga kura kwa wajumbe kama Simba apewe pointi 3 au la, kura zikapungua upande wa Simba, wakanyang'anywa tena zile pointi. Ikawa furaha na nderemo upande wa Yanga na Kagera Sugar na kilio kikubwa kwa Simba hadi kutishia kwenda FIFA. Simba wakapewa jina Mezani FC. Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku zikayoyoma.

Wenye akili tukasikitika sana, tukaonya na kusihi sheria zifuatwe maana ndio msingi wa kuheshimiana dunia nzima. Sheria ni tamu na chungu wakati wote kutegemeana na uko upande gani. Watu waliweka pamba masikioni, kebehi zikawa nyingi, wakasisitiza matokeo ya uwanjani yaheshimiwe!!! Leo walewale waliokebehi ufuatwaji wa sheria, ndio wanataka ushindi wa mezani dhidi ya Mbeay City. What a joke! Yaani miezi 10 tu iliyopita ni kweli watu wamesahau kuwa waliongoza kampeni ya kuvunja kanuni na ilipovunjwa wakashangilia? Leo wanapata wapi moral authority ya kudai pointi 3 nje ya uwanja?

Hata hivyo kwa kumalizia, mimi nitaendelea kusimamia kanuni. Kama kweli kuna wachezaji wa Mbeya City walizidi uwanjani, sheria na kanuni zifuate mkondo wake, na Yanga wapewe nafuu inayowastahili kwa mujibu wa sheria. Lakini pia kuna wachezaji walipiga wenzao viwiko vya makusudi, mashabiki walirusha mawe, n.k, hatua stahili zichukuliwe. Na iwe funzo kuwa hatuwezi kuendesha mchezo wa mpira wa miguu kwa hisia pekee. Logic, reasoning na common sense lazima itumike.

Haki Itendeke na Ionekane kuwa Inatendeka.
 
Yanga
IMG-20180423-WA0012.jpg
 
Hakuna la maana uliloandika. Hayo matukio uliyolinganisha hayafanani kimazingira wala kikanuni. Rudi ukajipange tena Ili uje na thread yenye mashiko.
 
Hakuna la maana uliloandika. Hayo matukio uliyolinganisha hayafanani kimazingira wala kikanuni. Rudi ukajipange tena Ili uje na thread yenye mashiko.

Hayafanani kivipi? Issue ni kutaka pointi za mezani. Usijifunge kwenye kufananisha hadi mtu awe na kadi 3 za njano. Mnapiga kelele kutaka pointi nje ya uwanja baada ya kushindwa kuzipata uwanjani. Hii ni haki yenu, ila mnachosahau mlikataa pointi zisipatikane nje ya uwanja.
 
wewe sio haji manara kweli! Mbona unaandika vitu havina sense
 
Yanga buana..wameshasahau walivoita wenzao mezani fc..sasa hivi mimacho imewatokaaa wanataka wapewe point za mezani!!! Kweli usimcheke mkunga....
 
Hayafanani kivipi? Issue ni kutaka pointi za mezani. Usijifunge kwenye kufananisha hadi mtu awe na kadi 3 za njano. Mnapiga kelele kutaka pointi nje ya uwanja baada ya kushindwa kuzipata uwanjani. Hii ni haki yenu, ila mnachosahau mlikataa pointi zisipatikane nje ya uwanja.
kwenye mambo ya sheria kuna kitu kinaitwa physical evidence... Fakhi mechi ambayo Simba walilalamika kuwa alipewa yellow card Azam TV hawakuonyesha mubashara tofauti na hii ya Yanga Eliud Ambokile jezi namba 10 hakutoka ....Timu inayofanya cheating inanyang'anywa points ni sawa na kuchezesha mchezaji sio wenu..full stop
 
Mkuu ni electronic evidence na sio physical evidence
 
Simba hawakuonewa walitaka tu kudhulumu, acheni kushikilia mambo ya kuzushwa. Yale ya Mbeya city yana ushahidi wa wazi.
 
Back
Top Bottom