Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,709
- 9,030
Novemba 7, 2015 ikiwa ni siku mbili baada ya kuapishwa, aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli alipiga marufuku safari zote za nje ya nchi na kuelekeza zifanywe na mabalozi, baadae zikatengenezewa utaratibu wa kibali. Magufuli akajiweka mfano kwa kuamua kutulizana ndani, mara chache akitembelea nchi za majirani. Sambamba na kupiga marufuku safari za nje likatoka tangazo la elimu bure.
Soma=> Magufuli apiga STOP Safari za nje ya Nchi; Elimu Bure kuanza Januari 2016
Wananchi tukaanza kulalamika, Rais gani tunabanana nae nchini bila kwenda kupata exposure huko nje, tukamsema kuhusu betri na uhusiano wa ndege pamoja na kujitetea kwake kwamba Ulaya ameshaishi. Hapo tumeshasahau kisanga cha Rais aliyepita na safari za nje.
=> Safari za Rais Jakaya Kikwete tangu aingie madarakani 2005
Pia wanasiasa hawakuwa nyuma => Joseph Mbilinyi (Sugu) amtaka Rais Magufuli asafiri Nje ya Nchi ajifunze kwa wenzake
Imekuja awamu ambayo haiwazi kuhusu matumizi yake, upungufu wa madarasa tu ukaleta tozo ambayo hatujawahi kuiona, ukakopewa trilioni zaidi ya moja. Vyanzo viwili vya mapato kwenye kazi moja ambayo zamani ilitumia mapato ya kawaida ya Serikali.
Tupo tunakamuliwa kuhudumia msafara mkubwa zaidi wa Serikali unaokaa siku nyingi zaidi nje ya nchi, umebeba mawaziri, maafisa wa Serikali, waandishi na wengineo na kila siku wakipokea, hela zinazotobolewa kwenye mifuko yetu kwa namna yoyote ili ziwahudumie.
Tuliwataka wanaosafiri, wamepatikana na wanatengeneza makazi madogo nje nchi. Covid inaishia hii, tutawaelewa zaidi siku zijazo.
Pichani, Rais Magufuli akiongoza kikao kilichopiga marufuku safari za nje ya nchi mwaka 2015