JERUSALEMU
JF-Expert Member
- Sep 19, 2012
- 3,112
- 3,536
Amani iwe nanyi wanabodi,
Tumedanganywa tena! gesi imetoka.Kumbe kudanganyana duniani hakutakwisha.wakati wa gesi inatoka haitoki ilikuwa shughuli pevu kule Mtwara na wilaya zake.Mwanzoni serikali serikali ilielemewa ,askari walizidia nguvu na vijana wa kimakonde,wakapata imani kuwa wamedhibiti gesi haitatoka na viwanda vya kuchakata gesi lazima vitajengwa hukohuko Mtwara.umoja ukaimarishwa miongoni mwa vijana wakiongozwa na bodaboda.
Serikali haikukubali kusalim amri, wakajipanga, wakaja na mitarimbo, silaha za kila aina kukabiliana na akina uchimung'unye wala uchiteme.tukaambiwa sasa matembezi mwisho saa moja na ikifika saa mbili kila mmoja awe amelala!
Akaja bibi wa gesi, akatusadikisha kuwa gesi haiendi kokote kama wana wa Nchi ile wasipo ridhia.Na kwamba viwanda vya kuchakata gesi lazima vitajengwa Mtwara.Bibi akawanasihi vijana kuto pigana kwani kila kitu kipo sawa na ushindi upo upande wetu.Gesi haitatoka.
Yawezekana bibi alizuia maafa kwa kutumia saikolojia yake maana jamaa walijiandaa kikweli na silaha zingine zilikuwa zinaonekana kama za nuclear! zingetumika nani angesalimika!utu uzima dawa!
Htimaye gesi imesafirishwa na inatoka Kinyerezi ingwa inaonekana Bagamoyo haitafika.Dah kinjekitile na bibi wa gesi sina hamu nao, ni wajanja sana.