mwasita
JF-Expert Member
- Aug 5, 2016
- 371
- 376
Kuna binti nilikuwa nampenda sana mpaka naye alijua kuwa nampenda sana naona kujua kuwa nampenda sana akajawa na fikira potofu kuwa siwezi fanya uamuzi wowote juu yake hata akifanya ujinga!
Tumekuwa kwenye mahusiano kwa zaidi ya miaka mitatu.
Nilikuwa nimeshaanza kuhisi kuwa ana michepuko mingine. Basi nikafanya uchunguzi wangu nikagundua kuwa alikuwa nayo miwili.
Uchunguzi nilioufanya haukuwa hata na chembe ya shaka.
Mchepuko wake wa kwanza alikuwa ni jamaa ambaye nilikuwa nafahamiana naye nilichokifanya ni kumdadisi huyu jamaa pasipo yeye kujua nilitaka nini. Uzuri ni kwamba jamaa huyu hakujua kuwa yule binti nina mahusiano naye hivyo alifunguka kila kitu kwangu kama jamaa ninayefahamiana naye bila kujua kuwa anaongea na mtafuta taarifa!
Kwa uzuri wa binti huyu ilikuwa ni proud pia kuwa naye hivyo hata jamaa huyu kunisimulia story zote juu ya kuwa na uhusiano na binti huyu ilikuwa kama sifa kwake kujulikana anamiliki binti yule.
Kila alichonisimulia nilikuwa narekodi kama ushahidi. Ni kweli niliamini kuwa ana uhusiano naye kwani kuna matukio ambayo alikuwa ananiambia kuwa binti alishawahi kumwambia alionana na mimi maeneo fulani akanisalimia na ni kweli maeneo hayo tumeshawahi kuwepo na binti huyo.
Baada ya kukusanya taarifa hizo nikampa hongera jamaa huyu kwa kuwa na binti huyu na pia nikamwambia itapendeza zaidi kama tutakuwa tunatambulishana kwa mashemezi zetu basi akaniambia nisiwe na shaka atanitambulisha tu.
Mchepuko wa pili ni classmate wake aliyesoma naye chuo. Huyu naye kuna siku huyu binti alikuja home kwangu kama ilivyokuwa kawaida yake! Basi siku hiyo akaniomba simu yangu aangalie video basi sikuwa na neno nikampa!
Kwa sababu nilikuwa nachezea simu yangu basi nikamwambia anipe ya kwake niendelee na kile nilichokuwa nakifanya. Bila neno akanipa. Loo! Ama kweli wahenga walisema za mwizi arobaini!
Basi nikiwa naendelea na ishu zangu za game kwenye simu yake ghafla ikaingia SMS. Ubaya hizi smartphone zingine SMS ikiingia tu inajifungua yenyewe tayari kwa kusomwa. Macho hayana mpaka nikaisoma ile SMS ilikuwa ya kimapenzi.
Hata sikutaka kuwa na papara nilichokifanya nikaikariri ile namba kichwani then nikaifunga hiyo SMS nikaendelea na game langu kama vile sijaona kitu! Baada ya mda kuwa jioni akaenda zake kwake hata sikuonesha dalili zozote za kubadilika kwa sababu ya SMS hiyo kama siku zote nikamuaga akaenda zake.
Kutaka ushahidi zaidi, yule mchepuko wake wa kwanza nikamwambia anitambulishe kwa shemeji yangu japo hata kwa kuniunganisha kwenye simu yake, ya shemeji na ya kwangu ili tufahamiane na shemeji!
Jamaa akampigia shemeji (mpenzi wangu) yangu ili kumwambia anitambulishe kwake huyu binti akagoma siku hiyo. Siku nyingine tena akampigia akagoma akasema hataki kabisa kutambulishwa kwangu basi jamaa baada ya kumaliza tu kumpigia simu huyo binti, jamaa akanipigia simu akanielezea full story ambavyo mchakato umekwama!
Kutokana na kukamilika kwa ushahidi na pia kuridhika nao baada ya jamaa kumaliza kunielezea mkwamo wa kutambulishwa sikupoteza mda nikampigia simu huyu shemeji yangu ambaye ni mpenzi wangu pia. Nikamwambia kuanzia leo mimi na wewe basi endelea na huyo uliyenaye kama Mungu amekupangia kuolewa na huyo basi muoane naye!
Hata hakujibu neno lolote nikamwambia sawa na nikakata simu! Siku hiyo hakunipigia simu akakaa kimya kama alivyokuwa kimya kipindi nampa maelezo ya mwisho katika kuvunja uhusiano wetu!
Kesho yake akanipigia simu kama mara tatu hivi lakini sikupokea kwa sababu sikuwa na morali kabisa kutokana na maudhi aliyokuwa amenifanyia. Baada ya kutafakari usiku wa siku hiyo nikaona ngoja nimpigie nisikilize anasemaje. Nikampigia lakini hakupokea simu basi nikamwacha nikadhani labda atakuwa amelala!
Kesho yake asubuhi nikampigia tena. Hapa ndio nikachoka zaidi!
Yaani simu alipokea mwanaume akaniuliza wewe nani na unasemaje? Sikutaka kuwa na jazba nikamuuliza tu una uhakika simu hiyo ni yako? Akasema kama si yangu ningepokea?
Basi nikamwambia brother usidhanie ni ujanja kutumiwa na mwanamke eti ukidhania unanikomesha wala huko Mi siko kabisa na nisingependa tuingie kwenye mgogoro na wewe kwa sababu ya huyo mwanamke! Ila mwambie tu kuwa asidhanie ananikomesha Mi kiroho safi nimeshaachana naye hivyo awe na amani na wala Mi hainiumizi kwa hata anayoyafanya, Mi namtakia kila lakheri huko aendako! Basi nikakata simu! Kutokea hapo sikumtafuta na wala hakunitafuta tena!
Imepita miezi kadhaa bila mawasiliano naye tena nilikuwa nimeshamsahau kabisa kwenye memory yangu! Ghafla mwezi huu ameanza kunitext SMS kwenye whatsap yangu akijifanya kunisalimia! SMS za mwanzoni nilikuwa simjibu akaendelea kunisalimia na kunitakia best wishes! Sikutaka kumjibu ili nisimlete karibu nikaanza kumkumbuka tena!
Baada ya kutafakari nikaona si busara kuendelea kuwa na chuki kwa kitu ambacho kimeshakuwa historia na hakiwezi kubadilika. Na niliamua mwenyewe kuachana naye hivyo sitakiwi kuendeleza chuki zaidi ya kuondoa tu ule upendo wa kimapenzi niliokuwa nao kwake!
Basi nikawa namjibu text zake. Basi akaanza na kunipigia simu anajifanya kuniletea vistory yaani yuko confident kabisa kama kwamba hapakuwepo kitu hapo!
Kuna siku nilimuuliza unamfahamu fulani?(nikamtajia jina la yule mchepuko wake wa pili) Akawa anajidai hamjui nikamuuliza namba hii unaifahamu?(namba ile iliyotuma sms siku nilipokuwa na angalia simu yake) Akasema ngoja niangalie kama ipo kwenye simu yangu. Alipoangalia akasema oooh huyu mtu alikuwaga ananifuatilia blah blah nyingi! Nikamwambia sina kesi naye wala sina kesi na wewe!
Yaani aibu hana kabisa hata kuona aibu tu kwa aliyonifanyia hata lile la mwisho la kumpa mwanaume apokee simu nilipompigia!
Basi katika kuchati kila mara anadai nimekumis mara nakupenda Mi naishia kumwambia tu ahsante! Basi juzi akaniambia oooh nakupenda, nataka nikuzalie mtoto, nikamwambia roho yangu ilishatoka kabisa kwako juu ya hisia za kimapenzi na sitaki kabisa. Ibaki tu urafiki wa kawaida!
Nikamuuliza umefikiria nini na umekosa wanaume wengine? Kwa nini umenichagua mimi? Siku hiyo hakujibu akaacha na kuchati.
Jana akaamka na kuanzisha story zingine kabisa as if maswali yangu hakuyaona! Yaani neno lake nimekumis haliishi kutajwa!
Ki ukweli sina hata chembe ya upendo wa kimapenzi kwa huyu mdada wa watu kwa sasa na siku zote zijazo! Zaidi nikiamua kumfanyia uhuni kwa ujinga wake wa kutaka kurudisha mapenzi na wakati anajua kabisa alichonifanyia kuwa ni uhuni nitamuumiza bure kihisia!
Sikutaka kulipiza kisasi kabisa kwa kuamini kuwa hakuwa riziki yangu!
Mi niliona nitumie ustaarabu nijiengue niwaachie wenzangu na sikutaka kuwapa taarifa waliobaki japo nilikuwa nawajua wote. Niliona pia si busara kumharibia kwa hao aliokuwa nao!
Kwa situation hii ungekuwa wewe ungefanyaje kwa namna anavyokuja?
Unaruhusiwa kutoa ushauri maana kuna wengine wanaweza kunufaika na ushauri wako pale yatakapowapata. Wakati mwingine tunajifunza kutokana na makosa ya wenzetu.
Mi nilishakata shauri sitarudiana naye maana nitamchezea bure tu kwani sina moyo wa kusahau na kusamehe kwa mambo aliyonifanyia nikikumbuka nilivyokuwa nampenda na kumjali!
Sina mapenzi tena kwake zaidi ya kumpenda kwa sababu ni binadamu mwenzangu tu!