Tulia ametenda uovu

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
DK. Tulia Akson, naibu spika wa Bunge, amefanikiwa kuvuna aibu. Ni kule kukubali kwake kusimamia uamuzi wa kufukuza wabunge saba wa upinzani katika Bunge la Jamhuri, anaandika Saed Kubenea.

Miongoni mwa waliofukuzwa, ni Tundu Lissu, mbunge wa Singida Mashariki na mnadhimu wa kambi ya upinzani bungeni; Zitto Kabwe, mbunge wa Kigoma Mjini, na Godbless Lema, mbunge wa Arusha Mjini.

Wengine ni Esther Bulaya, mbunge wa Bunda Mjini; Pauline Gekul, mbunge wa Babati Mjini, na John Heche, mbunge wa Tarime Vijijini.

Baadhi yao walishitakiwa mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge. Wengine wamesomewa mashitaka na kuhukumiwa bila hata kusikilizwa.

Wengine walishitakiwa na wakaweza kujitetea, lakini wakiwa wamezuiwa kuwakilishwa na mawakili, kama ambavyo kanuni za Bunge zinaelekeza.

Mwenyekiti wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, ni George Mkuchika, kada mashuhuri wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Tayari uamuzi huu uliosimamiwa na Dk. Tulia umeanza kupingwa ndani na nje ya Bunge.

Hata hivyo, naibu spika hakutoa nafasi ya kusikiliza hoja tofauti. Miongoni mwa hoja hizo ni zifuatazo:

Kwanza, kazi ya kamati ya haki, kinga na madaraka ya Bunge, ni kuchunguza na kutoa mapendekezo kuhusu masuala yote ya haki, kinga na madaraka ya Bunge.

Kazi hizi zimetajwa kwenye kanuni ya 4(1) (a) na (b) ya nyongeza ya nane ya kanuni za kudumu za Bunge, toleo la Januari 2016.

Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, katika suala hili, haikutimiza majukumu yake kama ilivyoelekezwa na Bunge.

Imetenda kazi zake kwa njia ya kibaguzi. Haikufungulia mashitaka wabunge wa CCM wanaotuhumiwa kufanya vurugu bungeni siku hiyo.

Kwa mujibu wa kumbukumbu rasmi za bunge, kwa kutumia picha za video zilizowasilishwa mbele ya kamati, baadhi ya wabunge wa CCM, wanaonekana wakifanya vurugu, ikiwamo kuongea bila utaratibu na bila ruhusa ya kiti cha spika.

Wengine wametumia lugha isiyoruhusiwa ndani ya Bunge.

Vile vile, baadhi ya wajumbe walipohoji sababu za watuhumiwa kutofikishwa mbele ya kamati, mwenyekiti hakutaka kusikiliza.

Hata ripoti iliyosomwa bungeni haikueleza hoja za wajumbe wengine wa kamati kushinikiza wabunge wote wanaoonekana kwenye kumbukumbu hizo wafikishwe mbele ya kamati ya Bunge.

Hivyo, kamati ilipokea maelekezo ya spika ya kuchunguza mwenendo wa wabunge, kinyume cha Katiba, kanuni za Bunge na sheria za nchi.

Pili, wajumbe walio wachache walipinga pendekezo la kamati la kutoa onyo la jumla kwa wabunge wote wa upinzani; kwamba ikitokea mbunge yeyote wa upinzani ametenda kosa jingine, atachukuliwa hilo ni kosa lake la pili.

Huku ni kukiuka haki na utoaji wa haki. Yawezakane adhabu kugusa wabunge wote wa upinzani, wakati wengine hawakushitakiwa, hawakutuhumiwa na wala hawakupata fusra ya kujitetea?

Kamati inawezaje kutumia maneno, “baadhi ya wabunge,” lakini papo hapo ikahukumu wabunge wote wa upinzani?

Wala spika hakuelekeze uchunguzi wa ziada dhidi ya wabunge wengine walioonekana kwenye video iliyowasilishwa mbele ya kamati. Ameishia kung’ang’ana na wabunge wa upande mmoja tu – upinzani.

Tatu, wabunge saba wa upinzani wamehukumiwa kinyume cha kanuni ya 74(3)(a) za kanuni za Bunge.

Sehemu ya sita kwenye ukurasa wa 53 kanuni ya 74 inaeleza aina ya kosa. Ikiwa mbunge aliyeshitakiwa ametenda kosa la kwanza, mbunge huyo atazuiwa kuhudhuria vikao vya Bunge visivyozidi 10.

Aidha, kanuni inasema, “ikiwa hilo ni kosa lake la pili au zaidi, mbunge huyo atazuiwa kuhudhuria vikao visivyozidi 20.”

Baadhi ya wabunge wamehukumiwa kutohudhuria mikutano miwili ya Bunge – mkutano wa Bunge la bajeti unaondelea sasa na mkutano ujao wa Bunge.

Wala ndani ya kanuni, hakuna utaratibu wa kutuhumu makosa ya jumla. Kuna utaratibu wa kuwapo maelezo ya kina kwa kila kosa na kwa kila anayetuhumiwa na wakati kosa limetendeka. Kamati ilituhumu kwa jumla na bila kuzingatia matakwa ya kanuni.

Nne, naibu spika hakuzingatia mapendekezo ya wajumbe wachache walioshauri kuwa kabla ya uamuzi kufikiwa na Bunge, ni muhimu watuhumiwa wakapewa fursa ya kujitetea mbele ya wabunge wenzao.

Ni kama ilivyofanyika kwenye Bunge la Tisa, ambapo Zitto alipewa fursa ya kujitetea mbele ya Bunge zima kabla ya azimio juu ya adhabu yake kufikiwa.

Ni wakati wa sakata la mkataba wa Buzwagwi, ambako Zitto alituhumiwa kusema uongo bungeni. Baadaye ikafahamika kuwa kilichoitwa “uongo” na watawala, kilikuwa kweli tupu.

Naibu spika hakusikiza hoja zote hizo. Hakusikiliza, si kwa sababu alikuwa na hoja. Hapana. Ni hulka yale ile ile ya ubabe na kutaka kufurahisha waliompa cheo. Basi!

Kwa mfano, kanuni ya 5 (1) ya kanuni za kudumu za Bunge inaelekeza spika, katika kutekeleza majukumu yake, kuzingatia uamuzi wa maspika waliotangulia.

Katika Bunge la Tisa, aliyekuwa spika wake, Samwel Sitta, aliruhusu wajumbe wawili wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Christopher Ole Sendeka na Anne Kilango Malecela, kuwasilisha maoni yao mbadala bungeni.

Ni pale kamati ilipokuwa ikijadili shauri lililofunguliwa na Dk. Reginald Mengi dhidi ya aliyekuwa mbunge wa Mkuranga, Adam Malima.

Kilango na Sendeka waliruhusiwa kusoma maoni yao mbele ya Bunge zima.

Naye Sitta baada ya kusoma maoni ya Kilango na Sendeka alifikia hitimisho, kwa kukubaliana na maoni ya wajumbe wawili dhidi ya kundi la wajumbe waliowengi.

Sitta alifikia uamuzi huo kutokana na mazingira ambayo yalitawala kuanzia usikilizaji wa kesi, utoaji ushahidi hadi uandishi wa hukumu.

Mengi alilalamika kuwa Kamati iliyokuwa chini ya Juma Nhunga na makamu wake, Willison Masilingi, isingemtendea haki.

Alisema kwamba kulikuwa na mazingira ya mhimili wa utawala (executive) kuingilia mhimili wa Bunge (legislature), jambo ambalo ni kinyume cha utawala bora na mgawanyo wa madaraka.

Alidai kuwa aliyekuwa waziri mkuu wakati huo, Edward Lowassa, alimshauri ajitoe katika kesi hiyo, kwa kuwa wabunge wamehongwa na mmoja wa wafanyabiashara wakubwa nchini.

Philimon Ndesamburo, aliyekuwa mmoja wa wajumbe wa kamati, alijiuzulu katikati ya shauri kwa kile alichoita, “kamati kuhongwa.”

Ili kuondoa utata, Sitta alimwandikia barua Ndesamburo ili kufafanua tuhuma alizoporomoshea wabunge na Bunge.

Katika barua yake kwa Sitta, tarehe 24 Januari 2007, Ndesamburo aliendelea kusisitiza kuwapo kwa rushwa na shinikizo kutoka kwa watawala serikalini.

Sitta alieleza katika uamuzi wake aliosoma bungeni tarehe 8 Februari 2007, kwamba amezingatia matokeo ya uchunguzi na ushauri wa kamati; ushauri wa wajumbe wawili waliotoa mawazo tofauti – Sendeka na Kilango – na uchambuzi na ufafanuzi wa kilichoelezwa na Ndesamburo.

Sitta hakutaka kukubaliana na maoni ya walio wengi. Alikataa. Aliridhika kuwa uamuzi huo ulitolewa kwa jazba na ulilenga kuwapo kwa nia mbaya.

Alisema kwamba maneno ya Malima dhidi ya Mengi bungeni yalimuathiri mfanyabiashara huyo na yalikuwa na athari kubwa ya kumgonganisha na viongozi wakuu wa nchi.

Katika saka hili la sasa, ukweli ulio dhahiri ni kwamba naibu spika aliamua kwa nia mbaya. Hakutaka kutafsiri vema kanuni za bunge.Hakutaka kuona maslahi ya wengi katika hoja za wabunge.

Naibu spika ameshindwa kuunganisha hekima na kanuni. Matokeo yake, ameibuka na uamuzi ambao badala ya kuunganisha bunge umelipasua katikati.
 
Tulia kitu ganiii
Sisi wa mbeya
Hua atu argue na wanawake aje ajalibu kugombea hata ubunge muone kama ajapigwa chin
Pili mwanamke mwenye matatizo la kike ................
.........
Nafikir mtakuwa mmenielewa huwa wana matatizo kama hayo
 
hivi kuna mtanzania mzalendo anaweza kusikiliza na kuamini anachokiandika au kukiongea huyu kubenea?? huyu si ndiye aliyeandika kuwa Lowassa hasafishi?????
 
Tulia kitu ganiii
Sisi wa mbeya
Hua atu argue na wanawake aje ajalibu kugombea hata ubunge muone kama ajapigwa chin
Pili mwanamke mwenye matatizo la kike ................
.........
Nafikir mtakuwa mmenielewa huwa wana matatizo kama hayo
Hatujakusoma mkuu
 
hivi kuna mtanzania mzalendo anaweza
kusikiliza na kuamini anachokiandika au
kukiongea huyu kubenea?? huyu si ndiye
aliyeandika kuwa Lowassa hasafishiki??
 
Haya wale wa kukariri wanaoimba kila siku kuwa naibu spika anasimamia kanuni waje watuambie hizo kanuni 'zisizowagusa' wabunge wa ccm anazosimamia!
 
hivi kuna mtanzania mzalendo anaweza
kusikiliza na kuamini anachokiandika au
kukiongea huyu kubenea?? huyu si ndiye
aliyeandika kuwa Lowassa hasafishiki??
Sasa hivi kuna wanyarwanda pia ni watanzania,
 
hivi kuna mtanzania mzalendo anaweza
kusikiliza na kuamini anachokiandika au
kukiongea huyu kubenea?? huyu si ndiye
aliyeandika kuwa Lowassa hasafishiki??
Naona wewe umekuja kusaidia kuinua uchumi kutoka rwanda
 
hivi kuna mtanzania mzalendo anaweza
kusikiliza na kuamini anachokiandika au
kukiongea huyu kubenea?? huyu si ndiye
aliyeandika kuwa Lowassa hasafishiki??

Hiyo imeshazoekeka jenga hoja mkuuu so kila cku kurudia kitu kimoja hakuna mengine ya kuandika inaonesha jins gan umeishiwa .
 
Kila kitu zam zam.....zam yake itafika
Mbowe, Lissu na mbatia wanakimbia wanaogopa hadi kivuli cha Dr Tulia

wanachukua mipasho ya mitaani wanaleta bungeni, Bungeni wanaenda waheshimiwa, lazima kuongea kiheshimiwa, wahuni wote wataisoma namba
 
Back
Top Bottom