Tukumbushane: Weekend kama hii.....

Twilumba

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
11,540
12,398
WanaJF,

Miaka ya 80-90 nilikuwa Morogoro Maarufu kama mji kasoro bahari, weekend kama hii haikuwa tabu na maisha ya mashaka kama sasa, wakati mwingine tukisia habari kuwa bwawa la kidatu limejaa sana maji hadi kuyaachia mengine yapungue ili kuzuia uharibifu unaoweza kutokea kwa sababu ya kuongezeka kwa maji hayo. Suala la Mgao sikuwahi kulisikia

Neno Mgawo halikuwa Midomoni mwetu kabisa hata kama lilikuwepo basi ni la mgawo wa Pelemende kutoka kwa mapadri na makasisi siku za Jumapili pale kanisa kuu la Mt. Patrick mjini morogoro, mgawo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu siku za Jumapili kwa watu wa Rika langu wakati ule Vijana wa rika la kati. tofauti na sasa ambapo Neno mgawo linaweza kumzimisha mtu kwani Upeo wa fikra zake hukimbilia kwenye Umeme na Maji......

Zamani jamani ilikuwa Raha hakuna Ufusadi mkubwa ambao ulitingisha Nchi kama huu wa sasa!!!

Sitaki kuwachosha kwa hadithi ndefu za kututoa machozi kwa kukumbuka uzuri wa taifa hili miaka hiyo, kimsingi nataka kukumbuka namna ambavyo pale Moro watu walikuwa wanakula maisha, Nakumbuka DJ John Mkimbizi a.k.a DJ John Dilinga, Dj Maarufu sana pale mji kasoro bahari akipiga kwanja Morogoro Hotel ukumbi maarufu wa shimoni, kana kwamba hiyo haitoshi kulikuwa na Bwalo la Umwema, Masuka Village, Rock Garden, Sapna, Shan Sinema na DDC.

Kiujumla sehemu hizo zilikuwa ni mwanana sana weekend kama hii tulikuwa ni kupanga tu wapi pa kwenda kujivinjari huku mwanaume ukiwa umepiga Shati lako la Eagle na Suruali ya Michael jackson, bila kusaha chini umepiga ndula au Lakuchumpa huku Jumamosi tukisumbiri gazeti la maarufu la Mfanyakazi!!

Kulikuwa na mango park garden hapo napo unakutana na Dj mkali aliyekuwa aikpiga miondoko ya Funk na Rhumba wakati huo ambayo kwa kina ndio ilikuwa inatamba mno eti kwa sasa wanaita Flashback.... hata hivyo still naipenda miziki hiyo.

Hii ni kwa Morogoro ambako mimi nilikuwepo, je MwanaJF tukumbushane wewe wakati huo ulikuwa wapi au unakumbuka kiwanja gani kilikuwa ndo cha kujivinjari maeneo eneo!!!


 
Pale dar kulikuwa na mbowe club, lang'ata, vijana hostel, tazara nk.
 
Back
Top Bottom