Tukumbushane "table manners" mbovu

Mkeo kaleta wali na nyama, mgeni analazimisha kunawa na kuomba aongezewe nyama. Mnaanza kula tu, yeye anatafuta nyama kubwa kubwa huku akiongea kwa furaha kana kwamba yuko kwake na kulalamika kuwa chakula ni kidogo hamta shiba huku akimuita mkeo. Shemeji mbona hiki chakula umepakua kidogo hivi, hakuna kilichobaki huko jikoni?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…