Tukubali tukatae % kubwa ya ajari chanzo ni barabara

Aaron

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
3,019
4,693
Wana jukwaa
Juhudi zinazofanywa na jeshi la police pamoja na sumatra kudhibiti ajari za barabarani hazitoweza kufanikiwa kama miundo mbinu ya barabara haitarekebishwa.
Ukiangalia barabara kuu mfano dar mwanza na mikoa mikoa mingine barabara ni finyu saana...yaani gari moja likikwepa hata shimo kidogo tayari imeingia upande wa gari linalokuja mbele yake... hii ni hatari sana..haijalishi dreva amekunywa viroba au amevuta bangi...
Mfano kwa barabara za dar pamoja na magari kuwa mengi lakini ni mara chache kusikia magari yamegongana hii ni kwa sababu barabara zake zimetengwa yaani kila njia iko mbali na njia nyingine hivyo ni vigumu magari kugongana uso kwa uso hapa ata aende 180km/hr ni vigumu kusababisha ajari labda agonge lililoko mbele yake..ambayo nayo ni ngumu sana...
Kwa ongezeko la magari na uchumi kukua kama hizi barabara hazitapanuliwa basi kukoma kwa ajali ni vigumu... barabara hizi zinabeba magari makubwa ya mizigo na likiiangia barabarani linachukua eneo zima la upande mmoja... hivyo ili gari jingine likitaka ku overtake lazima kwanza litoke kwenye saiti yake na kuingia saiti nyingine ila kuangalia kama mbele kuna gari...ndipo li over take... sasa asume liingie laini nyingine na wakati huo huo kuna gari lina kuja karibu itakuwaje...??
Hii ni hatari sana!!!
 
unachozungumza kina ukweli ndani yake lakini asilimia 80 ni uzembe wa madereva na hakuna haja ya kuwatetea hata kidogo labda nitoe tu ivi vichache
1. Idadi ya watu imeongezeka hivyo matumizi ya vyombo vya moto yameongezeka mara 1000 times wakati miundo mbinu yake imebaki palepale
kwa mfano songea dar sio chini ya busi 8 zinatoka Arusha-dar idadi haijulikani, bado magari ya mizigo,mifugo njiani watembea kwa miguu,magar ya watu binafsi sasa so barabar inakuwa ipo bize kwa nini tusibutuane
2. miundombinu i mibovu,siyo za kimataifa
Miaka hii ufanisi wa magari ni mukubwa sana gari lina speed/km 180 au na zaidi kwa mabasi, sasa unategmea nini
Miaka ya zamani gari zilikuwa hazina speed songea dar mnalala njiani leo ni massa tu
ana
3.Madereva
Hawa ndio wajinga mara 1000 mfano ajali ya bus la Luwenzo na lile lilo tumbukia pale ruaha ni uzembe wa madereva,ndugu mleta mada usiwatetee hata kidogo ni wajinga sana na ndio wanao tuua kila siku nakubali barabara ni za zamani sasa kwa nini wasiendeshe vile barabara inavyotaka
asilimia ndogo sana ajali inasababishwa na hitilafu ya gari na barabara nyingi ni hawa wapuuzi
4.Ulevi na uchovu
bangi, viloba na mirungi na ulevi hawa jamaa mara nyingi wanatumia sana hivyo vitu wanasema starter tena barabara ya arusha-dar
5.Ushirikina
nguvu ya mungu ifanyike mara kwa mara ipo sana iringa na mbeya
6.Abiria hawatoi ushirikiano wakati dereva anapo over speed sana
Nina experience ya hii tabia na sio mara moja watu wanakuambia sisi tunaenda bukoba tutafika leo
7.Rushwa kwa trafiki
Hapa napo ni jibu barabara zote tanzania
8.Sheria za barabarani ziwe reviewed adhabu ni ndogo sana
hujawahi kusikia madereva wanasema bora kuua kuliko kumpa mtu majeruhi
 
Sawa barabara ni sababu lakini cha kwanza kabisa na kikubwa kuliko vyote ni uzembe wa madereva
 
hapana tatizo ni barabara na ukitaka kujua hilo angalia kwa makini barabara ya morogoro road anzia stop over mpaka chalinze jinsi ilivyo
 
Back
Top Bottom