Tukubali kukosoana tukiwa wamoja

Tukubali kukosoana tukiwa wamoja

Lituye

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
1,864
Reaction score
5,697
Tupo katika wakati mgumu kama taifa kwa sasa hususani kuhusu uzalendo. Japo sio mwana CCM kwa sasa lakini kuna jambo la kujifunza kwa M.W.L JK. Nyerere.

Wakati Rais mstaafu wa Zambia Dr. Kaunda alipo wekwa remanded Rais mpya wa Zambia Frederick Chiluba.
Jumuhiya kimataifa zilimpa jukumu rais mstaafu wa Tanzania Mwl. NYERERE kutatua mgogoro huo.

Nyerere alienda kuonana na Rais Chiluba na kumshawishi amuachie Kaunda na kama kuna ishu basi Kaunda awekwe kizuizini nyumbani kwake atolewe gerezani juhudi zikiwa zinafanyiaka kutatua mgogoro.
Baada ya mazungumzo na Chiluba Nyerere aliomba kupelekwa gerezani kumuona Kaunda.

Alipo kutana na Kaunda waliongea mambo mengi na akamshawishi ale chakula kwa kuwa wamesha ongea na Chiluba. Kaunda akakataa kula akidai ili ale lazima aambiwe kwa nini yupo gerezani kwani anaona hana hatia.

Nyerere akamwambia kama hatakula hata yeye huwezi ondoka atamwambia nini Betty mkewe Kaunda kama litatokea jambo baya dhidi yake? Akamwambia Askari magereza wa Zambia atufute chumba kingine pale gerezani karibu na Kaunda ili naye alale hapo.

Mama Maria Nyerere naye akasema kama mumewe anala hapo gerezani basi na yeye atafutiwe upande wa gereza wanawake wanalala hawezi ondoka mumewe akilala hapo.

Taarifa hizo zilipo ifikia ikulu ya Zambia ziliistua serikali na ikakubali kutekeleza mambo yote waliyo jadiliana na Nyerere.

Ndipo Kaunda alikubali kula na Nyerere akaondoka Zambia. Haya yameandikwa ktk kitabu cha mtoto wa mwisho wa Kaunda.

Tanzanian ilikuwa ni nchi ya heshima kwa mataifa. Ilichukia udharimu kwa vitendo bila kujali mipaka ya nchi.
Sasa hivi kuna makaburu yanateka, kutesa kupoteza na kuua watu halafu yanasema eti watu wasiingilie kwa kuwa ni mambo yao ya ndani kuua wenzao bila hati.
 
Tafsiri ya uzalendo ya sasa ni kulinda majizi na taasisi za majizi ya Mali ya Umma bila aibu.

Mambo ya kuteka watu, Watanzania tulikuwa tunasikia kwenye nchi kama Zaire kipindi cha Seseseko,Uganda chini ya Amin, Zanzibar kipindi cha Mzee yule ambaye aliwahi kusema "Muungano ni kama koti nk.

Leo hii yapo kwenye madirisha na milango ya kila Mtanzania zile nyimbo za kisiwa Cha amani hazipo tena.

Daaa!!
 
Et Mchengerwa na Chalamila wanasema wapo tayari kulinda amani hata kwa kutoa uhai wao? Kuna watu wanachekesha sana. Round hii hatukubali mpaka Kila mmoja ajue maisha yetu sote Yana thamani.
 
Back
Top Bottom