Tukosoe Serikali ya Magufuli kwa hoja si vijembe

MWATANI

Member
Feb 14, 2014
44
125
Serikali ya awamu ya tano imekuwa ikisiginwa na kukosolewa na makundi tofauti tofauti ambayo yamekuwa hayafuraishwi na kile kinachoonekana kama mabadiliko na misimamo hasi yenye sura ya kimapinduzi kutoka kwenye mifumo ya mazoea, utovu wa nidhamu, ufisadi, rushwa, na upigaji dili kuelekea kwenye mifumo ya kiuchumi na viwanda yenye fursa sawa kwa wote, na mifumo inayolenga kumpa unafuu wa maisha mwananchi wa kawaida, wachambuzi wa siasa wanaamini haya ni mabadiliko mutambuka kuelekea kwenye taifa la uchumi wa kati.

Pengine ni kweli hoja za wadau kuikosoa serikali ya Dkt. John Pombe Magufuli kamwe hazipaswi kubezwa na bila shaka zina mantiki ndani yake lakini ukweli ni kwamba kinachoendelea kwa sasa katika hatua hizi za awali za awamu ya tano ni kuinyoosha nchi na kuirudisha mahali pake kama ilivyokuwa enzi za awamu ya kwanza, pili na tatu, serikali yoyote duniani inapofanya mabadiliko ya kupambana na mizizi ya mafisadi waliozoea kutumia mali za umma kwa maslahi yao na kuondoa kila aina ya uharifu na uozo ni lazima mwananchi wa kawaida apate misukosuko ya kiuchumi na ndicho kinachoendelea hivi sasa.

Wapo wanaoamini taifa liligeuzwa mali ya watu binafsi waliotumia mifumo ya kiutawala kuendesha mambo yao kwa maslahi ya vizazi vyao, Matabaka yaliibuka kati ya walipa kodi na wasio lipa kodi ushawishi wa wafanyabiashara wakubwa kuindesha serikali uliongezeka huku taasisi nyeti kama takukuru na mifumo ya kimahakama zikikosa meno ya utendaji, wakati fulani taifa lilifika pahala likawa na watu ambao wanakula kilafi kisha kutapikia viatu vya wafadhili “eating like gluttons before vomiting on the shoes of donors” Hii ni kauli aliyowahi kuitoa balozi wa zamani wa Uingereza nchini Kenya, Edward Clay.

Bila shaka hakuna Mtanzania mzalendo ambaye atambui kuwa taifa hili changa kiuchumi lilikuwa limefikia hatua mbaya yakuwa kama kichaka cha wezi, mafisadi, rushwa, utovu wa nidhamu kwa watumishi wa umma, mikataba mibovu, ulanguzi na kila kadhia ya taabu na karaha ziliandama taifa hili, uwepo wa matukio haya ulionekana kama kikwazo kwa maendeleo ya mtanzania wa kawaida ambaye anaishi maisha ya hoehae ya kula mlo mmoja kama mnyama kwenye taifa lenye maliasili za kila aina.

Licha ya watawala kujinasibu kuwa Tanzania ni taifa tajiri sana lenye madini, misitu, milima na mabonde yenye kuvutia watalii kauli hizi kwa miongo mingi sasa zimebaki kuwa ni porojo za kisiasa zisizokuwa na tija kwa mtanzania wa kawaida, Mtanzania wa leo anahitaji majigambo ya kusifia maliasili za taifa lake yatakayoendana na kipato cha maisha yake ya kila siku na si ngonjera zenye vimelea vya uhuni wa kisiasa ndani yake.

Ikumbukwe kuwa wapo wasomi, wanazuoni na baadhi ya viongozi wa dini na makada wa chama tawala na vyama pinzani waliopaza sauti zao kupinga mifumo ya uendeshaji wa serikali hasa awamu ya nne, ambayo pengine ilionekana kutokuwa na maslahi kwa mtanzania wa kawaida mzee Butiku na jopo lake mwaka 2010, walisema rais Kikwete amefungwa minyororo na mafisadi na kupiga kelele kuwa kwa kipindi hicho awezi kufurukuta yupo kifungoni, wapo walionena na kudai serikali inaendeshwa kishikaji wapo waliosema taifa linayumba na linahitaji rais mwenye hulka za udikteta ili taifa liweze kunyooka katika muundo wa kiutawala na kiuchumi.

Dhana nyingi zilijengwa wakati huo kutokana na kile kilichoonekana kuwa kero sugu za watanzania kushindwa kutatuliwa na utawala wa wakati huo, wadau na wasomi walijenga hoja na sababu za msingi kuwa serikali imeshindwa kupambana na mifumo ya ufisadi wa mali za umma kutokana na ukimia na upole wa kiongozi wa wakati huo inawezekana dhana hii ilikuwa na mashiko ndani yake maana wapo wanafalsafa wanaoamini kiongozi mdhaifu na goigoi uzalisha tabaka na mifumo dhaifu ya kiutawala na kiongozi imara shupavu na mwenye hulka za ukali ndani yake uzalisha mifumo ya uwajibikaji na uchapakazi.

Inawezekana sasa kundi kubwa la watanzania ikiwa ni pamoja na wasomi pia wanazuoni wamepata jibu maridhawa ambalo kwa kipindi cha muda mrefu walikuwa wanadai kuwa na kiongozi mwenye hulka na haiba za kupambana na utaifa kwanza, ufisadi, umwinyi, nidhamu , uzalendo , uchumi imara na ulinzi wa maliasili za taifa letu hata hivyo uenda ikawa vigumu kwa umma wa watanzania kuelewa jitihada mbadala zinazofanywa na Dkt. Magufuli kwa sasa kutokana na mabadiliko hayo kuwa hasi katika maisha yetu ya kila siku.

Matunda ya mabadiliko ya staili hii kwa kawaida uchukua muda kumfikia mwananchi wa kawaida, kwa mantiki hiyo kwa kipindi hiki itaonekana serikali hii ipo kwa sababu ya kumyanyasa mwananchi wake kitu ambacho si kweli ila ni kutokana na mabadiliko ambayo imeamua kuyafanya lakini hali ingekuwa tofauti na maisha ya sasa kama serikali ingeamua kuendelea na mifumo ya awamu iliyopita ambayo wadau waliipigia kelele kama mifumo ya wachache kunyonya keki ya taifa.

Si kweli kwamba serikali ya awamu ya tano iko sahii kwa kila mipango na mikakati ya kisera inayofanya la hasha! Ukosea maana aiongozwi na malaika, kwa mantiki hiyo basi tunahitaji kujenga hoja na kujipambanua kuikosoa serikali ya awamu ya tano kwa kile inachokifanya kwa sasa kama ishara za maisha bora ya baadae kwa mtanzania wa kawaida.

Ni vema tukawakosoa watendaji na viongozi waliopewa dhamana kwa mantiki mbadala na si vijembe, kejeli na kebehi ili pale wanapokosea waweze kujirekebisha bila shaka na wao ni binadamu kama sisi tunaowanyoshea vidole na wala si malaika, sisi ni wamoja na nchi si mali ya mtu bali ni mali ya wazalendo wote kwahiyo ni vema kukosoa kwa kuzingatia dhana ya kuelimisha na kujenga falsafa za kulikwamua taifa letu lilipo kwa sasa badala ya kulalamika na kupiga kelele zisizo na misingi ya kuliletea taifa maendeleo yoyote, ni bora kupendekeza hoja mahsusi badala ya vioja na misemo isiyo na misingi ya kuinyanyua nchi kutoka hapa tulipo kwenda upande wa pili ulio bora zaidi kwa maisha yetu na vizazi vijavyo.
 
Ronal Reagan

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
4,843
2,000
Mwatani,

Hebu tueleze mnavyoonyosha hii nchi, je:-

1) Malengo yenu kisiasa, kiuchumi na kijamii ni yapi hasa?

2) Mkijipima na kujitathmini, mpaka sasa mmefikia/mmefanikiwa asilimia ngapi?

3) Mmetumia gharama kiasi gani kufikia hizo asilimia? Mtatumia shs ngapi kukamilisha zoezi lenu?

4) Iwapo itabainika kuwa mlitumia vibaya dhamana na rasimilimali mlizokabidhiwa kwenye "kunyoosha" je mtalirudishia Taifa gharama hizo?

5) Kwanini unafikiri dissaproval rate ni kubwa na kila uchao kelele zinazidi?
 
Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
35,933
2,000
Jee yeye mwenyewe anapokosolewa anajibu kwa hoja au vijembe?
Dawa ya moto sio maji ni moto tuu. Kwa hiyo kama naye huwa hoja anajibu kwa vijembe watu watampa vijembe vyake.
Lingine naona kama vile style ya matusi kama imeanza kutumika kujibu hoja sasa hiyo ni hatari kwani yataanza kutokea kama yale ya mbunge wa Kenya bure!
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Chachata

Senior Member
Apr 29, 2011
195
250
Yako mambo mazuri ya na yapo mambo mabaya mengi pia. Hayo mazuri hayazuii kukosoa hayo mabaya mengi
 
mliberali

JF-Expert Member
Jul 13, 2012
8,100
2,000
Serikali ya awamu ya tano imekuwa ikisiginwa na kukosolewa na makundi tofauti tofauti ambayo yamekuwa hayafuraishwi na kile kinachoonekana kama mabadiliko na misimamo hasi yenye sura ya kimapinduzi kutoka kwenye mifumo ya mazoea, utovu wa nidhamu, ufisadi, rushwa, na upigaji dili kuelekea kwenye mifumo ya kiuchumi na viwanda yenye fursa sawa kwa wote, na mifumo inayolenga kumpa unafuu wa maisha mwananchi wa kawaida, wachambuzi wa siasa wanaamini haya ni mabadiliko mutambuka kuelekea kwenye taifa la uchumi wa kati.

Pengine ni kweli hoja za wadau kuikosoa serikali ya Dkt. John Pombe Magufuli kamwe hazipaswi kubezwa na bila shaka zina mantiki ndani yake lakini ukweli ni kwamba kinachoendelea kwa sasa katika hatua hizi za awali za awamu ya tano ni kuinyoosha nchi na kuirudisha mahali pake kama ilivyokuwa enzi za awamu ya kwanza, pili na tatu, serikali yoyote duniani inapofanya mabadiliko ya kupambana na mizizi ya mafisadi waliozoea kutumia mali za umma kwa maslahi yao na kuondoa kila aina ya uharifu na uozo ni lazima mwananchi wa kawaida apate misukosuko ya kiuchumi na ndicho kinachoendelea hivi sasa.

Wapo wanaoamini taifa liligeuzwa mali ya watu binafsi waliotumia mifumo ya kiutawala kuendesha mambo yao kwa maslahi ya vizazi vyao, Matabaka yaliibuka kati ya walipa kodi na wasio lipa kodi ushawishi wa wafanyabiashara wakubwa kuindesha serikali uliongezeka huku taasisi nyeti kama takukuru na mifumo ya kimahakama zikikosa meno ya utendaji, wakati fulani taifa lilifika pahala likawa na watu ambao wanakula kilafi kisha kutapikia viatu vya wafadhili “eating like gluttons before vomiting on the shoes of donors” Hii ni kauli aliyowahi kuitoa balozi wa zamani wa Uingereza nchini Kenya, Edward Clay.

Bila shaka hakuna Mtanzania mzalendo ambaye atambui kuwa taifa hili changa kiuchumi lilikuwa limefikia hatua mbaya yakuwa kama kichaka cha wezi, mafisadi, rushwa, utovu wa nidhamu kwa watumishi wa umma, mikataba mibovu, ulanguzi na kila kadhia ya taabu na karaha ziliandama taifa hili, uwepo wa matukio haya ulionekana kama kikwazo kwa maendeleo ya mtanzania wa kawaida ambaye anaishi maisha ya hoehae ya kula mlo mmoja kama mnyama kwenye taifa lenye maliasili za kila aina.

Licha ya watawala kujinasibu kuwa Tanzania ni taifa tajiri sana lenye madini, misitu, milima na mabonde yenye kuvutia watalii kauli hizi kwa miongo mingi sasa zimebaki kuwa ni porojo za kisiasa zisizokuwa na tija kwa mtanzania wa kawaida, Mtanzania wa leo anahitaji majigambo ya kusifia maliasili za taifa lake yatakayoendana na kipato cha maisha yake ya kila siku na si ngonjera zenye vimelea vya uhuni wa kisiasa ndani yake.

Ikumbukwe kuwa wapo wasomi, wanazuoni na baadhi ya viongozi wa dini na makada wa chama tawala na vyama pinzani waliopaza sauti zao kupinga mifumo ya uendeshaji wa serikali hasa awamu ya nne, ambayo pengine ilionekana kutokuwa na maslahi kwa mtanzania wa kawaida mzee Butiku na jopo lake mwaka 2010, walisema rais Kikwete amefungwa minyororo na mafisadi na kupiga kelele kuwa kwa kipindi hicho awezi kufurukuta yupo kifungoni, wapo walionena na kudai serikali inaendeshwa kishikaji wapo waliosema taifa linayumba na linahitaji rais mwenye hulka za udikteta ili taifa liweze kunyooka katika muundo wa kiutawala na kiuchumi.

Dhana nyingi zilijengwa wakati huo kutokana na kile kilichoonekana kuwa kero sugu za watanzania kushindwa kutatuliwa na utawala wa wakati huo, wadau na wasomi walijenga hoja na sababu za msingi kuwa serikali imeshindwa kupambana na mifumo ya ufisadi wa mali za umma kutokana na ukimia na upole wa kiongozi wa wakati huo inawezekana dhana hii ilikuwa na mashiko ndani yake maana wapo wanafalsafa wanaoamini kiongozi mdhaifu na goigoi uzalisha tabaka na mifumo dhaifu ya kiutawala na kiongozi imara shupavu na mwenye hulka za ukali ndani yake uzalisha mifumo ya uwajibikaji na uchapakazi.

Inawezekana sasa kundi kubwa la watanzania ikiwa ni pamoja na wasomi pia wanazuoni wamepata jibu maridhawa ambalo kwa kipindi cha muda mrefu walikuwa wanadai kuwa na kiongozi mwenye hulka na haiba za kupambana na utaifa kwanza, ufisadi, umwinyi, nidhamu , uzalendo , uchumi imara na ulinzi wa maliasili za taifa letu hata hivyo uenda ikawa vigumu kwa umma wa watanzania kuelewa jitihada mbadala zinazofanywa na Dkt. Magufuli kwa sasa kutokana na mabadiliko hayo kuwa hasi katika maisha yetu ya kila siku.

Matunda ya mabadiliko ya staili hii kwa kawaida uchukua muda kumfikia mwananchi wa kawaida, kwa mantiki hiyo kwa kipindi hiki itaonekana serikali hii ipo kwa sababu ya kumyanyasa mwananchi wake kitu ambacho si kweli ila ni kutokana na mabadiliko ambayo imeamua kuyafanya lakini hali ingekuwa tofauti na maisha ya sasa kama serikali ingeamua kuendelea na mifumo ya awamu iliyopita ambayo wadau waliipigia kelele kama mifumo ya wachache kunyonya keki ya taifa.

Si kweli kwamba serikali ya awamu ya tano iko sahii kwa kila mipango na mikakati ya kisera inayofanya la hasha! Ukosea maana aiongozwi na malaika, kwa mantiki hiyo basi tunahitaji kujenga hoja na kujipambanua kuikosoa serikali ya awamu ya tano kwa kile inachokifanya kwa sasa kama ishara za maisha bora ya baadae kwa mtanzania wa kawaida.

Ni vema tukawakosoa watendaji na viongozi waliopewa dhamana kwa mantiki mbadala na si vijembe, kejeli na kebehi ili pale wanapokosea waweze kujirekebisha bila shaka na wao ni binadamu kama sisi tunaowanyoshea vidole na wala si malaika, sisi ni wamoja na nchi si mali ya mtu bali ni mali ya wazalendo wote kwahiyo ni vema kukosoa kwa kuzingatia dhana ya kuelimisha na kujenga falsafa za kulikwamua taifa letu lilipo kwa sasa badala ya kulalamika na kupiga kelele zisizo na misingi ya kuliletea taifa maendeleo yoyote, ni bora kupendekeza hoja mahsusi badala ya vioja na misemo isiyo na misingi ya kuinyanyua nchi kutoka hapa tulipo kwenda upande wa pili ulio bora zaidi kwa maisha yetu na vizazi vijavyo.
unajiumauma tu. ukweli ni kwamba mabadiliko hayawezi luletwa na ccm.

unaweza kuandika makala ndefu kujaza server lakini ukweli utabaki kuwa ukweli.

ushauri ili kututuoa hapa tulipo ni kuitoa ccm madarakani tu.

naona ccm mnaanza kukiri kwamba mlichemka na mnaendelea kuchemka.

mpaka kufika wakati mnatuomba ushauri jinsi ya kuendesha nchi.

kwanza mkubali kuachia madaraka ndo tutatoa ushauri kwa chama kitakachochukua.

nyie hatuwapi ushauri NGO.
 
jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
32,038
2,000
Magufuli atapimwa kwa kuifuata Ilani ya CCM tu....ndio mkataba kati ya wananchi na Rais kupitia CCM.
 
stigajemwa

JF-Expert Member
Nov 12, 2016
449
500
Tatizo la raisi yeye mwenyewe anapenda kupiga vijembe, azungumzi kama raisi wa nchi mara nyingi hupenda kuzungumza kama mwenyekiti wa chama na kama amiri jeshi mkuu, tunataka azungumze kauli zenye kutuunganisha kama taifa na zenye kutupa matumaini na si zenye kutukatisha tamaa kwani yeye ndio kama baba. Hivyo lazima tunaopenda kutafiti mambo tumkosoe vinginevyo nchi itaharibika
 
AGOLA

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
1,345
2,000
Yeye mwenyeweni mtu wa vijembe hayo maneno aliyoyaporomosha Bukoba ni vijembe au ya kiutashi?
 
Marlex Jr El

JF-Expert Member
Nov 6, 2015
1,785
2,000
"sita yafukuwa makaburi" nini maana ya kauli hii?

Ikiwa makaburi hayafukuliwi kauli na unafiki wa kunyoosha nchi unatoka wapi?

Pia tujiulize ili kupata mafanikio ktk nchi hii kuelekea uchumi wa kati ni mambo yapi ya msingi tunapaswa kufanya si kila siku matamko kama nchi ni disco vijana wanatambiana Kwa pesa zao.
 
G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
10,635
2,000
Hakuna kitu anachofanya Magufuli zaidi ya ujinga wa kisiasa. Hajawahi na hatowahi kuonyesha ufanisi wowote ule kwenye uongozi wake! Mtu huyu anaiangamiza nchi na lazima hilo kila mmoja wetu alione tena na alitazame kwa macho ya mshtuko!

Magufuli hafai kamwe kuwa rais wa nchi na amethibitisha hilo kwa matendo na maneno, anaendekeza siasa za ubaguzi mkubwa kisiasa na kamwe hatofanikiwa kwenye uongozi!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom