Tukope kwa busara!!!

HARRISON ONE

Member
Jan 8, 2014
42
30
kukopa si jambo baya sana pale ambapo mkopo husika utatumika katika kuleta suala la maendeleo kwa mtu binafsi,jamii,na hata taifa kwa ujumla,na hata nyingi ya biashara kubwa na hata makampuni makubwa ni matokeo ya kukopa fedha toka katika mabenki na kutumika kama ilivyokusudiwa.Miongoni mwa jamii ya kitanzania kuna baadhi ya watu hupenda kukopa pesa toka kwa wenzao katika mambo ambayo kwa jinsi moja au nyingine si muhimu sana na hatimaye kumwingiza mtu katika lindi la madeni,hebu wana jf tuangalie je ni busara mtu kuja kukukopa fedha
1) Akapige maji(pombe)
2) Ili amtoe mtu wake(hawara,dem,mchumba) outing kwenye hotel ya five star k
3) kama ni mwanafunzi mara baada ya kupata boom na kumpeleka mtu wake shopping,then aje akukope
4) hela ya kusukia ya hawara yake
5) kukopa hela akacheze kamari(gambing)

Wana jf tutiririke sababu nyingine ambazo tunafikiri si za lazima sana
 
Back
Top Bottom