Tukiolewa mifumo yetu ya mwili haibadiliki jamani...

miss chagga

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
57,899
2,000
Habari za asubuhi wapendwa wangu ..
Nimeona wanaume wanalalamika ooh mke wa mtu , mke wa mtu then what?

Sasa wanaume niwaweke sawa TU kuwa mke wa mtu haina maana mimi kihisia, kimatamanio, kusikia njaa, kusikia hamu, kumtamani mwanaume, kutamani mambo mazuri, kupenda bata ndiyo once naolewa eti ndiyo mwili wangu unajifunga kama computer imebonyeza kitufe cha shut down ,,,... mnakosea sana wanaume

Mke wa mtu pamoja na kuwa mke wa mtu bado kihisia yupo active labda afikishe miaka ile ya monopose na majukumu kumbana sana ya watoto hayo mambo anaweza asiwaze..(nimesema hili naona mnaweweseka sana hapa)
ILA TU MUNGU AMETUPA UWEZO WA KUTUMIA AKILI ZETU KWA NGUVU NA KUSHINDA HAYO NA KUKAA KWA UTULIVU NA WAUME ZETU, JAMBO AMBALO WANAUME KWENYE UPANDE WA NGONO MMESHINDWA,....

Kwa hiyo kumtongoza mke wa mtu akakubali wewe uliyemtongoza ukijua ni mke wa mtu basi wewe ndiye uliyemkosea mwanaume mwenzio ....

Waume: Wewe usipotimiza majukumu yako ndani vyema kwa kigezo nimezaa sijui , oooh kwa sababu umenivisha mapete yako kidoleni ndiyo usinipe hela, usinisex vizuri, usiwe na maneno ya mahaba kwangu, haloo haloo kama upo hivyo akikutana na anaye cover hilo gape ataliwa tu atakuwa rahisi tu hakuna namna...

Mwanaume ukiingia ndani unanguruma tu kama lisimba linanjaa haupo soft , kufoka foka kama umepaliwa na mfupa wa samaki, bahili, maneno yako magumu kama ule ukuta wa kwenye tangazo la nyati cement ,.. aisee jiandae

ONYO:USIMJARIBU MKE WA MTU,
  • USIMLUBUNI MKE WA MTU KWA VIPESA VYAKO (hapa hata mi naweza kamatika)
  • USITUMIE UDHAIFU WA MWANAUME MWENZIO KULALA NA MKE WAKE.
  • ANAPOKUELEZA MATATIZO YA MUMEWE USITUMIE UO UPENYO KUMLA(wengi hapa wanaume hufanya makosa)
NB:MUME HAKIKISHA UNATIMIZA MAJUKUMU YAKO VYEMA NYUMBANI,,

asanteni; na pia sitetei uzinzi
 

NAKWEDE

JF-Expert Member
Aug 1, 2007
28,019
2,000
Tatizo wanaume waliowengi akishamuweka ndani mwanamke anapunguza baadhi ya manjonjo, mfano kama kipindi wana "shake well before use" alikuwa anaenda Uvinza, akishamuweka ndani haendi tena! Mahaba yanashuka pasipokuwa na sababu za muhimu. Wanaume badilikeni hata sie tunapenda kupendwa na kupewa "vitamu"
 

miss chagga

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
57,899
2,000
Tatizo wanaume waliowengi akishamuweka ndani mwanamke anapunguza baadhi ya manjonjo, mfano kama kipindi wana "shake well before use" alikuwa anaenda Uvinza, akishamuweka ndani haendi tena! Mahaba yanashuka pasipokuwa na sababu za muhimu. Wanaume badilikeni hata sie tunapenda kupendwa na kupewa "vitamu"
na yale maneno laini hawasemi tena , tena ukishapata mtoto utasikia mama fulani kwa lisauti la ajabu ambalo angelitumia mwanzo usingemkubali
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom