Zinjathropus
Member
- Oct 14, 2018
- 13
- 2
*TUKIO LA MOROGORO LITUONGEZE JICHO LA TATU*
Kwanza kabisa nitumie wino huu kuungana na mamilioni ya waTanzania wenzangu *kutoa pole kwa wote waliopoteza wapendwa wao* katika tukio la ajali lililotokea mkoani Morogoro, na M/Mungu azirehemu roho za wapendwa wetu walipoteza maisha kwenye tukio lile.
*HOJA YANGU*
Tukio lililotokea Morogoro ni tukio kubwa la kitaifa ambalo kila mTanzania ameguswa kwa namna yake.
Binafsi nimesikia na kusoma maoni na matamko mengi Sana kutoka kwa wananchi wengi na watu wenye dhamana serikalini, maoni ambayo yanaonesha namna ambavyo kila mmoja alivyolipokea tukio lile, kwa kadri ya "ulimwengu wa fikra" wa mtu mwenyewe.
Ukifuatilia kwa umakini maoni ya "walio wengi', utagundua kuwa maoni yao kuna upande yanaelemea, upande ambao unaonesha namna "jeshi la polisi, jeshi la uokoaji" walivyowajibika kuanzia mwanzo wa tukio mpaka mwisho, wengi wakiona hakukuwa na weledi/juhudi za dhati za kuzuia madhara zaidi, kwa kuwa uwezekano wa kuzuia kilichotokea ulikuwa mkubwa zaidi ya hoja za utetezi wa kwanini lilitokea lililotokea.
Swali kubwa ambalo tunapaswa kujiuliza kama taifa, *je, wananchi, serikali na majeshi yake, kuna tunalojifunza kutokana na hili ?*
Binafsi ninaweza kuwa upande wa wale wanaofikiri kuwa lililotokea "linaweza lisiwe funzo", kwani tunaweza kuunganisha doti zinazohusiana na matukio ya namna hii ambayo yalishawahi kutokea, hili sio la Kwanza !!
Taifa linazo kumbukumbu za matukio kama haya ambayo yalishawahi kutokea kule Mbeya na kwingineko ndani/nje ya taifa letu.
Kama taifa lina kumbukumbu hizo, je tulijifunza nini ??? Hapa utagundua kuwa Kama taifa hatukuwa na rejea ya kumbukizi ya matukio yale, ndio maana hili la Morogoro limekuwa kama geni kwetu, linaonesha namna tulivyokosa pa kujishikilia, ndio maana tunaweza tusiamani sana kama hili linaweza kuwa funzo na kuliweka kwenye kumbukizi zetu kama taifa ili pengine tuweze "kuinuka hapa tulipolala"
Na Kama taifa, Kama tunataka kujifunza, hatupaswi kutizama tu "mazingira fanani na tukio la Morogoro"
Tunapaswa tuwe na *jicho la tatu* litakalotusaidia kuona na kung'amua *mazingira yakinifu* ambayo nayo yanaweza kuleta madhara ya milipuko katika taifa.
Jicho la tatu* lituwezeshe kuona kuhusu vituo vya mafuta vilivyozagaa mijini katikati ya makazi ya watu, je, sheria zetu za nchi tulizonazo, Kama zinaruhusu "uwepo wa vituo vya mafuta mijini" , je zinafaa kuendelea kutumika ? Na Kama sheria hizo haziruhusu, je tumekwama wapi kuzisimamia ?
Jicho la tatu litusaidie kuona, je sheria zetu za nchi zinaruhusu *magari ya abiria kwenda kujaza mafuta kwenye vituo vya mafuta yakiwa yameshona abiria ?* (Hili ni jambo la kawaida sana ) Kama Sheri zetu zinaruhusu magari ya abiria kwenda vituo vya mafuta yakiwa yameshona abiria, je sheria hizi bado zinafaa kuendelea kutumika ? Na Kama sheria zetu za nchi tulizonazo *haziruhusu* magari ya abiria kuingia vituo vya mafuta yakiwa na abiria, je wahusika wa usimamizi wa sheria wamekwama wapi kuzisimamia ?
Jicho la tatu* lituwezeshe kumulika "maeneo ya maegesho" ya malori yaliyo safarini (mf. Ndiuka, ifunda, mafinga n.k), maeneo haya yanatumika sana *kunyonya mafuta* (siwachongei madereva ila ndio uhalisia ), je ni tahadhari ipi imechukuliwa katika maeneo haya, hasa uwepo wa vifaa vya dharura vya kuzuia milipuko ambayo pengine inaweza kutokea kutokana na msambao wa gesi unaotokana na "nyonyanyonya" ya mafuta ? Hasa tukizingatia kuwa "maeneo haya ya maegesho ya malori" mengi yapo katikati ya makazi ya watu !!
Kutokana na "uoni wetu wa jicho la tatu", je, bado hatutapata *la kujifunza ?*
Bado hatutaona *umuhimu wa kuongeza juhudi katika kuwaelimisha wananchi* juu ya namna ya *kuchukua tahadhari* za kiusalama kwenye haya *mazingira husishi/tajwa* ili kupunguza Kama sio kuzuia kabisa uwezekano wa kutokea madhara kwa wananchi pindi yanapotokea matukio haya ??
e, bado hatutaona umuhimu wa *kuzitafakari/kusimamia* vyema utekelezaji wa *usimamizi sahihi wa sheria husika* juu ya magari ya abiria yanayoingia kwenye vituo vya mafuta yakiwa yamesheheni abiria ?
Ni kweli hatutaona haja ya kuweka *mazingira ya tahadhari* kwenye maeneo ya maegesho ya malori ikiwemo kusogeza huduma za uokoaji na kuweka vifaa vya uokoaji katika maeneo haya ya maegesho ya malori ?
Binafsi, siamini, Kama taifa, kuwa hili nalo litaendelea kutufanya tuendelee kuamini kuwa hatuna uwezo wa kuziishi kumbukizi za matukio makubwa Kama haya ambazo zinapaswa kutufanya kuwa na *Jicho la tatu* ili tuweze kujisahihisha Kama taifa kwa kutafakari upya "umuhimu wa elimu ya tahadhari" kwa jamii na kuzitafakari upya *sheria zetu na usimamizi wake*
*Tahadhari yetu na uwajibikaji wetu ndio usalama wa wananchi wetu*
*Prosper Lazaro*
*(Iringa Mjini)*
*@prosperlazaro94@gmail.com*