Tukio la Khashoggi lingefanywa na Iran,Dunia nzima ingemuwekea vikwazo Iran.

mcomunisti halisi

Senior Member
Jan 17, 2017
103
325
Tumeshuhudia mara Kadhaa nchi za Saudi Arabia na Israel wakifanya uvunjifu lakini wamekuwa wakitetewa na kukingiwa kifua na USA.

Kuna matukio mengi lakini ningependa leo kuelezea matukio ya kihalifu yaliyofanywa na ufalme dhalimu wa Saudi Arabia.Miaka ya nyuma Saudia Arabia ilituhumiwa kufadhili wale hijackers walioangusha na kuharibu majengo pacha september 11 2001 lakini serikali ya US imekuwa ikiwatetea na kuogopa kuigusa serikali ya Saudi Arabia licha ya Congress kutaka serikali ya Saudi ichukuliwe hatua.

Juzi tumeona tukio la kinyama aliyofanyiwa Jamal Khashoggi na nyaraka za siri na uthibitisho umetolewa na dunia inajua ufalme wa Saudi Arabia ndio ulifanya unyama ule lakini US anamkingia kifua Saudi Arabia tunaona tena serikali ya Trump ikisema wazi wao na saudi ni marafiki na washirika na wanasaidiana kichumi na tutegemee kama miaka yote nothing will happen.

Lakini turudi nyuma US na UN wamekuwa wakiishambulia Iran sana na mengine ni ya kipropaganda sana mfano tumeona Iran waliingia Syria na kuwaondosha ISIS lakini propaganda zinatengenezwa kuwa Iran ana fadhili ugaidi wakati wao ndio walio wipe out isis syria.

Je hili Tukio la Khashoggi lingekuwa limefanywa na Iran unahisi kipi kingetokea kwanza US ingeshindikiza kila taifa lilaani tukio hili pia wangezidisha vikwazo na kutoa amri kwa mataifa mengine yaweke vikwazo kwa Iran na hata baraza la usalama la umoja wa taifa ungeitwa kwa dharura kuzungumzia ishu hio.

Tuache double standards
Tuache imperialism
 
Ndo ujue sasa kua democratic/developed countries ni wanafiki tu wanaoangalia masilahi yao
Well said walahi
HEKIMA MPE MWENYE HEKIMA WALAHI
Maana bado kuna milaaniwa ina fikiria wadhungu ndio kila kitu, mijitu mizima ovyo kabisa walahi
 
Well said walahi
HEKIMA MPE MWENYE HEKIMA WALAHI
Maana bado kuna milaaniwa ina fikiria wadhungu ndio kila kitu, mijitu mizima ovyo kabisa walahi
kwa avatar yako hio,....... kama zipo basi za kushikiwa
 
Watu wa Marekani hawana shida yeyote na watu wa Iran. Lakini kwa sababu Israel iko na shida na Iran, Marekani lazima itii Israel na waseme Iran ni adui.
Kwa sababu Saudi na Israel ni marafiki(chini ya maji), Marekani haiwezi kata uhusiano wake na Saudi, hata kama waliua Khashoggi.
Lakini kama ingekuwa Iran ambayo imetenda hilo tendo, wangepata 'extra sanctions'.
 
Wanafiki wakubwa na majizi ya kutisha
Saudia analindwa kwa mikataba ya miaka 500 na ufalme unalindwa kwa hali na mali na in return wananyonya petrol na kuwauzia silaha ambazo zinaangamiza ndugu zao wa Yemen
 
Back
Top Bottom