Tukikipa chama cha upinzani dhamana ya kuongoza nchi

Tukikipa chama cha upinzani dhamana ya kuongoza nchi

Kyenju

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2012
Posts
5,337
Reaction score
2,907
Binafsi siipendi ccm kwa tabia zake kandamizi kwa wananchi na ndiyo maana watu wengi tuna shauku kubwa kuona siku moja hiki chama kilichozeeka kinang'oka madarakani.

Lakini nimekuwa najiuliza swali hili, kwakuwa watanzania tunapenda kuona mabadiriko makubwa ya maendeleo katika nchi yetu na tunaamini kuwa tukikiweka chama kingine kituongoze tutafikia malengo, je ikitokea wakafanya vibaya kuliko tulivyotarajia ua kuliko hata hawa magamba tuwape adhabu gani?
 
Mpaka muda huu maisha magumu wanvaa tai na vx uwe ccm hata kama wanafunzi wanakaa chini richmond wameiba milion 155 kwa siku zidisha na muda hamna hatua yeyote iliyochukuliwa twiga pembe za ndovu viwanda vya nyerere vimekwisha miaka 50 ccm imefanya nini nani wakutukomboa au badi ndani ya ccm nani mwaminifu tumpe nafasi ya mwisho maana ndugu wewe na mimi ndo tunaumia c hao wakubwa TAFAKARI......
 
waliopo madarakani hatuwataki wanaotaka tuwape madaraka hatuwaamini hiyo ndo siasa ya bongo.
NB:KILA MWANASIASA ANATAKA KULA KWA SABABU ANA MENO SO CHAGUA MTU AMBAE HATAKULA SANA.VIGUMU KUPATA ASIYEKULA KABISA.aliweza yesu tu kuwa mfalme wa amani tena kwa sababu alikuwa na nguvu za umungu,angekuwa ana hali ya kibinadam angetuchukulia hata mademu zetu kwa kujivunia uwezo wake wa kutenda miujiza.
 
Tujifunze toka mataifa mengine mfano Kaunda v Chiluba, KANU v NARC n.k. Mwenye macho haambiwi tazama!
 
Uoga ndio unaotumaliza watanzania!Tuangalie mifano kwa nchi zingine!sera na ilan ya chama ndiyo itakayotupa mwongozo ......Tusiogope,tuchague kilicho chema!Bila CCM Tanzania itaendelea.
 
Binafsi siipendi ccm kwa tabia zake kandamizi kwa wananchi na ndiyo maana watu wengi tuna shauku kubwa kuona siku moja hiki chama kilichozeeka kinang'oka madarakani.

Lakini nimekuwa najiuliza swali hili, kwakuwa watanzania tunapenda kuona mabadiriko makubwa ya maendeleo katika nchi yetu na tunaamini kuwa tukikiweka chama kingine kituongoze tutafikia malengo, je ikitokea wakafanya vibaya kuliko tulivyotarajia ua kuliko hata hawa magamba tuwape adhabu gani?

Tuwapige chini CCM ili nao waamini kuwa kuna kuondolewa madarakani na wananchi, na mafisadi tuwapeleke jela. Wakiingia CDM wakaharibu tunawapiga chini uchaguzi ujao, na mafisadi wao(lazima wataibuka tu) tuwapeleke jela. Baada ya hapo kila chama kitaitambua nguvu ya umma na watapunguza sana kucheza na haki ya mwananchi.

Hata binadamu wanashinda Misikitini na Makanisani kwa sababu wanajua kesho kuna adhabu, vinginevyo ingekuwa balaa.

Hawa viongozi wakiona adhabu inatolewa kwelikweli, watanyooka, vinginevyo tutakuwa tunacheza.
 
Hakuna Chama kwenye Katiba kilichopewa Hati Miliki ya kutawala nchi hii milele!
 
kwa hiyo kwa uoga wako unataka tuendelee na hao hao mpaka lini? hivi kwanza una habari kwamba serikali yako sasa hivi haina sumni, na tunadaiwa usipime! pesa yote imehamia mifukoni mwa viongozi na wajanja (wezi) wachache, yaani 2015 rais atakayeingia madarakani atakuwa na kibarua kigumu sana cha kuhakikisha anarudisha uhai wa hazina? eti tunaweza kuwapa wapinzani wakaharibu zaidi, kwa hiyo unataka tusitafute suluhisho la shida hii inayotukabili?
 
Mkuu labda hukunielewa na sikusema tusiwape wapinzani, ebu soma vizuri utanielewa usiwe na jazba ndugu yangu.

kwa hiyo kwa uoga wako unataka tuendelee na hao hao mpaka lini? hivi kwanza una habari kwamba serikali yako sasa hivi haina sumni, na tunadaiwa usipime! pesa yote imehamia mifukoni mwa viongozi na wajanja (wezi) wachache, yaani 2015 rais atakayeingia madarakani atakuwa na kibarua kigumu sana cha kuhakikisha anarudisha uhai wa hazina? eti tunaweza kuwapa wapinzani
 
Back
Top Bottom