Tukifanya haya tutafikia Tanzania ya viwanda

Pamputi

JF-Expert Member
Apr 22, 2016
984
1,000
Kila siku huwa ninapozungumzia ujenzi wa demokrasia katika nchi yetu, baadhi ya watu huwa hawanielewi ninaposema kwamba CCM imara ni lazima iambatane na upinzani makini. Na kwamba kwa mazingira yalivyo sasa pasina kuwa na upinzani makini CCM itayumba, na kuyumba huku sio lazima kuiangushe CCM leo, lakini sote tunakubali kwamba kuwa katika safari ambamo gari linayumba yumba huwa si dalili njema. Nadhani wengine wanaendelea kutonielewa, mantiki ya uwepo wa vyama vya siasa katika ulimwengu wa leo ni kuibua hoja, kujenga hoja, kuleta mawazo ya kustawisha maisha ya watu na raia wa Taifa letu.

Kama chama kimojawapo kipo madarakani na kinatekeleza mawazo yake ya kustawisha maisha ya Wananchi, kazi ya vyama ambavyo haviko madarakani ni kuibua hoja na kujenga hoja ya namna mawazo hayo ama yanafanikiwa au la na kuhakikisha chochote kinachofanyika kweli kina mguso chanya kwa Wananchi. Aidha vyama vile ambavyo havipo madarakani vina kazi kubwa pia ya ama kuboresha mawazo ya chama kilichopo madarakani au wanaweza kuja na mawazo mbadala kabisa, ilhali lengo likiendelea kuwa kustawisha maisha ya watu na raia wa Taifa letu.

Sijui niseme hivi karibuni au tangu kitambo, kumejengeka dhana mbaya kwamba mkiwa katika vyama tofauti basi ninyi ni mahasimu, ninyi ni maadui na wengine huenda mbali na kujinasib wao ni wa utawala wa nuru na wengine ni wa utawala wa giza. Mimi nakubali kabisa vyama kama Taasisi ni watu na watu hukosea na tukubaliane kwamba watu wanapokosea wanapaswa kuwajibika kwa mujibu wa taratibu tulizojiwekea, Katiba na sheria zetu ikiwa ni mojawapo. Kwahiyo watu wakikosea, wawajibishwe, hata kama watu hao wanatoka chama chako, na si ustaarabu iwapo unashabikia watu kuwajibika kutoka vyama vingine wakati katika chama chako kuna matatizo.

Unapokuwa sio msafi unapoteza mamlaka ya kimaadili “moral authority” ya kukemea wengine wasio wasafi. Hata katika vitabu vya dini imeandikwa “ufalme mmoja hauwezi kuinuka juu ya ufalme uleule bali ufalme mwingine”, tafsiri yangu ya ufalme hapa yaweza kuwa watu wasio wasafi hawawezi kamwe kuwawajibisha watu wachafu na halkadharika watu safi hawana sababu ya kuwawajibisha watu walio safi, hiyo ni asili. Tunataka watu wasafi zaidi kama mtu mmoja mmoja katika mifumo yetu na mamlaka zetu za nchi ili watu hawa wasafi sio tu waende kuhakikisha mifumo na Taasisi zetu zinafanya kazi kwa uadilifu ili kutoa haki na hukumu kwa kila anayestahili bali wakajenge pia utamaduni wa watu wasafi tu kushika mamlaka. Imeandikwa katika vitabu vya dini watu wenye haki wakishika mamlaka Wananchi hufurahi na kunufaika.
 

treborx

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
4,630
2,000
Kichwa cha habari na yaliyojadiliwa kwenye mada ni tofauti kabisa. Au ulitaka kusema tukiimarisha demokrasia Tanzania itakuwa nchi ya viwanda??
 

dr mayunga

Member
Sep 16, 2011
6
20
Watanzania asilimia kubwa tunaishi kwa unafiki. Kama wewe ni mshaur mzur unapaswa kuongea kwa uwazi. Sio unapindisha pindisha. Sijaona mapendekezo yako juu jinsi ya kufikia nchi ya viwanda...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom