third eye chakra
JF-Expert Member
- Dec 27, 2023
- 919
- 2,155
DEATH OF MIND (KUPOTEZA KUMBUKUMBU)
Unaweza kuita 'detachment'!
Yaani ni ile hali ya Roho yako (consciousness) kutengana na akili zako (intelligence) pale UNAPOKUFA na kuelekea kwenye ulimwengu wa roho, ili aidha uweze kusonga mbele kuelekea kwenye highest dimensions (unyakuo/ ascension) au urudishwe duniani tena (reincarnation) humalizie kibarua chako!
NB: Kila roho imetumwa duniani, kukamilisha kusudi fulani ikiwa kwenye mwili.
Kwenye sehemu ya 3 ya somo hili (SPIRIT REALM) nilisema kuwa "Unapokufa au unapovua mwili huu wa damu na nyama, chap chap unaingia kwenye ulimwengu wa roho ambako huko unakutana na viumbe wa kila aina wa kiroho"
Kutokea hapo ndipo inapojulikana kuwa UNAPANDA JUU ZAIDI (ascension) au utalazimika kushuka/ kurudi tena duniani!
Wale waliokufa wakiwa wameifikia enlightenment level, hawahitaji tena kurudi duniani, badala yake wanapanda level ya juu zaidi ili kwenda kuwa sawa na Chanzo (The Source) cha vyote, SUPER COSMIC ENERGY ambayo wengine huita Mungu!
Maana sharti kila kitu kiirudie Asili yake, kilipotoka!
Nishati Kuu ambayo tunaita Mungu ni very pure na ikiingia kwenye miili ya viumbe (uumbaji) purity yake inapungua kutokana na hali (state) ya mwili ilipojiingiza, kwa hiyo inapotaka kutoka ili irudi kama mwanzo ulazimika kupitia mchakato tunaouita enlightenment kwa ajili ya purification in the process of turning back to the Source!
Ndio maana kila Nafsi inapewa awamu 108 ili ku-reincarnate, kwa kusudi la kutakasika (purification) kabla haijarudia Asili yake ya Uungu!
Kumbuka kila kitu KIMETOKANA na SUPER COSMIC ENERGY ambayo tulikubaliana katika masomo haya tuiite MUNGU MKUU (MWENYEZI MUNGU) na lazima kwake kila kitu kirejee!
So, kinarejea vipi?
Kikiwa na 'makorokoro' yake kiliyokuwa nayo wakati kimevaa mwili?
Hapana!
Lazima kwanza kiyaachilie (detachment) ili kibaki pure spirit ndipo kwake kirejee, kirudi ndani yake na kuwa kama Yeye!
Ndio maana katika masomo ya huko nyuma nilikwambia kuna kingdoms NNE za viumbe wa kimwili na viumbe vyote hivyo vina consciousness (roho/ uhai) na vinapokufa roho zake (Consciousnesses) huenda kwenye ulimwengu wa roho ambako kuna matabaka kwa kila roho (pitia masomo yangu ya nyuma)
Huko kwenye ulimwengu wa roho, kuna struggles za kila roho kupandishwa ngazi.
Roho za viumbe ambao sio binadamu hupambana ili zirejeshwe upya duniani, lakini mara hii kama binadamu, si kama wadudu, ndege, wanyama au mimea.
Roho zilizokuwa kwenye maumbo ya binadamu hu- struggle ili zipandishwe levels za pure spirits (malaika, miungu nk) au zirudi tena duniani zizaliwe upya kama watu.
Ni scrambling na struggling kila roho kwa namna yake. Kila roho inatafuta kufuzu badala ya kubakia level ile ile.
Roho zote zinazobaki kwenye ulimwengu wa 4D (zilipofikia) kwa muda mrefu zinakuwa wondering spirits na hivyo kutumiwa na wanadamu kufanya shughuli zao hapa hapa duniani!
Ngoja niendelee mbele tena kidogo . . .
✍🏻Kabla hujarudishwa tena duniani (hujazaliwa upya au kuzaliwa mara ya pili), unatakiwa kwanza kupoteza kumbukumbu zote za maisha ya dunia, maana unapokufa, kumbukumbu zote unaondoka nazo, isipokuwa wale waliofikia enlightenment, hao ndio wakiondoka kila kitu wanaachana nacho hapa hapa duniani!
Kwa wale waliokufa bila kufikia enlightenment ya juu kabisa, ndio hao hutakiwa ku-reincarnate.
Inakuchukua miaka kuanzia 4 hadi 600, Waalimu wengine husema ni kuanzia siku 1 hadi miaka 600, ili kupoteza kabisa kumbukumbu zote za maisha ya hapa duniani ndipo unaporuhusiwa ku- reincarnate.
Huwezi ku- incarnate ukiwa na kumbukumbu zote za maisha yako ya avatar!
Lazima kwanza hupoteze kumbukumbu zote za maisha uliyokuwa nayo ulipokuwa duniani, ingawa wakati mwingine kuna watu wanazaliwa na 'kiasi fulani' cha kumbukumbu za kuwahi kuishi, ila ni wachache sana na huwa hawakumbuki kila kitu!
Unakuta mtu anaenda mahali, lakini roho yake inamwambia "niliwahi kuishi hapa" au unaona kitu kwa mara ya kwanza, lakini roho yako inasema ndani yako "lakini hiki kitu nakifahamu" na ikitokea watu wa aina hiyo wakakutana, hujikuta wanaanza kuulizana "hivi tumewahi kuonana wapi, mbona kama sura yako sio ngeni" wakati hawajawahi kabisa kukutana na si kwamba wanakuwa wanafananishana, la hasha, roho kwa roho zinakuwa na some 'intelligences' (yaani waliwahi hata kuishi pamoja au mmoja aliwahi kuwa bibi au baba au mama au baba wa mwingine, ila kumbukumbu haziwezi kukaa sawa for 100%, wanaishia kwenye guessing ili maisha yaendelee)
Unakuta walikuwa ndugu miaka 700 au 800 iliyopita!
Lakini, kwa kawaida, the Universe haikurudishi duniani ukiwa na kumbukumbu zako (avatar mind), ni mpaka zi- dissolve kwanza na lazima miaka isiyopungua 600 ipite.
Ndio maana Eliya alipoondoka, ilibidi arudi kama Yohana Mbatizaji (roho ya Eliya) miaka karibu 700 tangu aondoke.
Kwa hiyo incarnation ya roho ya Eliya (Yohana Mbatizaji) ilitakiwa ikae foleni kwa miaka 700 ili mind iwe dissolved. Ndicho kitu tunaita the death of mind, kabla ya reincarnation!
Mtu mmoja aliniuliza "we unajuaje kwamba lazima wakae hiyo miaka?"
Jibu langu: Wataalam husema hivyo!
Kumbuka hakuna kitu cha kimwili au cha kiroho kisichokuwa na wataalam.
Utaalam wa kitu ni ujuzi wa kitu unaotokana na uzoefu. Ndio maana tuna wataalam wa Sayansi, wataalam wa Afya, Wataalam wa mambo ya jadi, Wataalam wa Ecology, Philosophy, Archaeology, Theology nk.
Hawa wataalam wa mambo ya roho zinazoondoka kwenye mwili huitwa Mediums, yaani wana uwezo wa kuongea na kila roho na kudodosa taarifa za mambo wanayoyataka!
Hujawahi kusikia mtu anasema "Roho Mtakatifu akaniambia?" au "malaika akaniambia" au "jini, mzimu wa babu ukaniambia" nakadhalika?
Hiyo ndiyo elimu ya kuwasiliana na roho (medium-ship)!
Wanaotaka kukutawala hawataki ujue hizi siri na unufaike nazo kama walivyokuzuia kwenye elimu ya meditation, nyota nk, kwa madai ya ni 'haramu' wakati wao kwao ni halali!
Elimu zinazoweza kubadilisha maisha wanazitaka wao tu na kwa wengine wanaziita "forbidden knowledge" au "dark knowledge" ili mradi usizijue ukanufaika kama wao!
Aidha, kuna elimu tunaita 'Hypnosis' ambayo hutumika kujua the past life!
Wajuzi wa elimu hii wanaweza kujua kama waliwahi kuishi duniani na hivyo wame-reincarnate au ndio mara yao ya kwanza!
HUKO MBELENI SANA KWENYE SHULE YA ESP (EXTRA SENSORY PERCEPTIONS) TUTAJIFUNZA KWA KIREFU KUHUSU HYPNOSIS!
Mtu anapokufa, yaani anapovua mwili wake, roho yake huwa haiondoki muda huo huo, yaani papo kwa papo, isipokuwa wale waliofikia level ya juu ya enlightenment.
Hawa wengine roho zao zinakaa-kaa kwenye mazingira yao zikiangalia miili waliyotoka kwa dakika kadhaa, kisha kumbukumbu zao huanza kuwaambia 'umekufa' (maana wanakuwa bado wako kwenye atachment, yaani roho na Nafsi zinakuwa bado zimeshikamana)
Detachment huchukua muda mrefu wa hiyo miaka 4 - 600 kama nilivyokwisha eleza huko mwanzo.
Kwenye kipindi cha kama dakika moja hivi, mtu aliyekufa (akiwa nje ya mwili wake) anaangalia mwili wake, waombolezaji na matukio yanayokuwa yakiendelea akiwa kama katoka usingizini...
Baada ya huo muda ndio anatambua "kumbe nimekufa na hawa ni wazazi wangu yule ni mke au mume wangu, wale ni wanangu, yule ni mshkaji wangu nk."
Anang'amua "tayari nimeshauacha mwili wangu"😢
Wale waliofikia high level of enlightenment/ spirituality hawanaga hizo habari, wanakuwa detached na mambo yote ya dunia. Wanaosikitika na kuhuzunika (kulia na kusaga meno😅) ni wale ambao hawakuwa enlightened, ambao kwao maisha ya duniani yalikuwa na maana sana!
Ndio hao hukomaa na ndugu, jamaa, marafiki na watu wao wa karibu. Kila mara wanajitokeza, lakini mara nyingi kwenye njozi au ndoto au hata kwenye maono wakiwa na jumbe nyingi za kiroho!
ASILI NI MAFUMBO
MDHARAU ASILI HUFA KIKATILI.