John Achila Mukumwa
Senior Member
- Jan 4, 2024
- 111
- 214
Tukatae Tabia ya Naamani
Naamani ni Nani
Katika kitabu cha 2Wafalme 5, tunasoma uponyaji wa mtu mmoja aliyeitwa Naamani, aliyekuwa Jemedari wa jeshi la Mfalme wa Shamu. Huyu Naamani alikuwa ni mtu mwenye ukoma ingawa alikuwa shujaa wa vita.
Siku moja alienda kutafuta uponyaji kutoka kwa Mungu wa Israeli, kupitia taarifa alizozipata kutoka kwa kijakazi wake aliyekuwa Muisraeli kwa asili. Alipokutana na Nabii Elisha, kwa uongozi wa Roho wa Mungu, aliagizwa akajichovye katika mto Yordani mara saba na ugonjwa wake wa ukoma utaondoka.
Mwanzo alikataa, lakini baadaye alikubali na Bwana Mungu akamponya ule ukoma, na ngozi yake ikarudi kama ya mtoto mchanga.
2Wafalme 5:14 “Ndipo akashuka, akajichovya mara saba katika Yordani, sawasawa na neno lake yule mtu wa Mungu; nayo nyama ya mwili wake ikarudi ikawa kama nyama ya mwili wa mtoto mchanga, akawa safi”.
Kwa uponyaji huo alioupata aliahidi kutotoa tena sadaka kwa miungu aliyokuwa anaitumikia hapo kabla, ambayo haikumsaidia kitu. Mungu aliyekuwa anamtumikia hapo mwanzo kabla ya kuponywa na Bwana alikuwa anaitwa Rimoni.
Pamoja na ahadi hiyo, Naamani aliona tatizo moja mbele yake. Alijua atakaporudi kwa Mfalme, bado atakuwa chini ya mfalme kama jemedari wake, na mara zote alikuwa anaongozana naye kuingia katika hekalu la mungu Rimoni. Naye pia alikuwa anasujudu. Hivyo akajua atakaporudi Shamu, hiyo desturi itaendelea.
Kwa hiyo akatangulia kuomba radhi kwa Nabii Elisha, kwamba endapo jambo hilo likitokea basi Mungu amsamehe (yaani amwachilie), kwa sababu hajadhamiria kufanya hivyo isipokuwa tu ni kwa kutimiza matakwa ya Mfalme, lakini yeye ndani ya moyo wake au kwa hiari yake mwenyewe hajakusudia kumtolea mungu Rimoni sadaka wala kumsujudia.
Nabii Elisha akamruhusu aende na afanye kama anavyoona yeye mwenyewe moyoni mwake.
MAMBO YA KUJIFUNZA KUTOKANA NA JEMADARI NAAMANI
1. Ni muhimu kupokea ushauri wa mtu wa ngazi ya chini pia
Tunajifunza imani ya kupokea uponyaji baada ya kukubali mashauri, kwani kitendo cha kuamini tu taarifa kutoka kwa kijakazi, ni imani kubwa. Siyo watu wengi wanaweza kuwasikiliza na kuwaamini watu walio chini yao kiuwezo, kielimu, kiwadhifa, na hata kiufahamu. Lakini Naamani aliweza hilo. Hata sisi, ili tuvute msaada wa Mungu na muujiza wake, ni sharti tuwe watu wa imani kama Naamani.
Imani hiyo ndiyo Bwana Yesu alirejea habari ya imani yake katika kitabu cha Luka 4:27: “Tena, palikuwa na wenye ukoma wengi katika Israeli zamani za Nabii Elisha, wala hapana aliyetakaswa ila Naamani, mtu wa Shamu.”
2. Kutokukata shauri la kumfuata Yesu Kristo kwa kuhofia kupoteza maslahi
Pamoja na imani yake ya kuponywa, Naamani moyoni alimkiri Mungu wa Israel kwa muujiza aliofanyiwa, lakini kwa matendo alimtumikia Mungu Rimoni, kwa heshima ya Mfalme. Yaani, ALISHINDWA KUACHA MASLAHI YA KIDUNIA, ili amfuaye Yesu.
Kwa maneno mengine, ni kwamba Naamani, alikuwa ni vuguvugu. Moyo wake upo kwa Mungu wa Israeli, lakini viungo vyake na utumishi wake upo kwa Rimoni (mungu wa nchi yake, Shamu).
Mfumo wa nchi yake ulimbana. Kazi aliyoifanya ilimfunga. Japokuwa alikuwa anatamani kweli kutotumika katika hekalu la mungu ambaye hakumsaidia, lakini tayari alikuwa ameshafungwa Nira, na hakuwa tayari kuikata hiyo nira.
Kitabu cha 2Wakorintho 6 kinasena: 14 “Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?
15 Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? 16 Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
17 Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha”.
Kama wakristo, ni lazima tutoke katika mahekalu ya sanamu. Ni lazima tutoke katika kazi zinazotulazimu kusujudia sanamu au kumwabudu shetani. Ni lazima tuache makundi yanayoturudisha kumwabudu shetani.
Ni kweli inagharimu, lakini hiyo ndiyo maana ya “kuubeba msalaba na kujikana nafsi”. Kama kazi inakuuzisha pombe, au mwili wako, au inakuabudisha sanamu, acha kazi, ili uondokane na uvuguvugu. Hiyo ni kwa sababu Bwana Yesu alisema atawatapika wale wote walio vuguvugu. Ufunuo 3:15: “Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. 16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu”.
Mtu hawezi kuwa mrefu na mfupi, kwa wakati mmoja. Haiwezekani. Ni hivyo hivyo kwenye imani. Huwezi kuwa vuguvugu. Yesu atakutapika. Huwezi kuwa kwa Mungu na kwa shetani, kwa pamoja. Yaani, huwezi kwenda kanisani, kisha ukatoka, ukaenda kwa mganga wa kienyeji, kumsindikiza kiongozi wako wa kazi.
Ni lazima kukata shauri. Tukatae tabia ya Naamani. Ni tabia ya unduma kuwili katika imani: yaani nuru na giza, kwa pamoja.
Aidha, USIRUHUSU MASLAHI YACHUKUWE NAFASI YA MUNGU KATIKA MAISHA YAKO.