Tujuzane namna ya kuishi na msichana wa kazi vizuri.

shonkoso

JF-Expert Member
Mar 13, 2015
687
1,455
Darasa ni popote jamani kuna watu wanaishi na hawa Dada wa kazi kama ndugu zao au Mara nyingine kwa haraka haraka waweza dhania ni mtoto wa hapo hapo,wengine wanakaa na hawa watu mpaka wanaolewa,sisi wengine week moja tu Vingi kashaanza kuulizia kama anaweza kwenda kusalimia kwao,wenye uzoefu wenu karibuni
 
Mara nyingi wadada wa kazi ndio tatizo...!
Huwa wakipendwa wanasahau kilichowapeleka...!

Wengine huwa wanakuja na lengo tofauti, kufanya kazi za ndani huwa ni Gia tu ya kutimiza malengo yao.

All in all, wadada ndio wanatakiwa wawajibike zaidi. Maana ile ni ajira kama ajira nyingine.. Changamoto atakazo kumbana nazo kazini, ana wajibu wa kukabiliana nazo kama sehemu ya kazi yake.
Hapo ataishi vizuri tu.
 
Kuna wakati atataka kutoka kutembea ili akutane na wanaume wamtongoze, acha aende maana ukimzuia atalala na watoto wako wa kiume au mmeo ama ndugu yeyote wa kiume, acha kuletea watoto wako tu zawadi bila yeye kumpa hata kidogo, acha kumsema wakati wa kula msosi hatakama amekuudhi namna gani, usimwache nyumbani unapoenda kwa ibada, mtie moyo muonyeshe kuwa anaweza ikiwezekana mpeleke kozi fupi ya jioni/weekend kuhusu fani yoyote, msaidiane kazi inapowezekana, mshauri kuhusu mabadiliko ya mwili wakati anapokaribia kupevuka pia kuwa karibu naye katika mambo yote.
 
Usimfanyishe kazi mfululizo.
Usimkaripie.
Piga nae story Cheka nae mtanie kidogo.
Sometimes Fanya kama unampenda sana kupita wote hapo nyumbani.
Vihela vidogo vidogo uwe unampa.
Uwe unampa na vizawadi eg body spray, nguo, biscuits etc
 
Wakina dada-na mama zetu huwa ndio changamoto kubwa ya kuishi na hawa wafanyakazi wa ndani,
Huwa wanawanyanyasa sana sjajua huwa ni Elimu ndogo au roho mbaya,utakuta mfanyakazi anapigwa au kurushiwa matusi makubwa kwa makosa madogo-madogo ambayo angeelekezwa kwa u taratibu tu.

Jambo la msingi ili kuishi nao vyema waelekezwe kwa utaratibu kama wamefanya makosa pasipo lugha za kejeri na dharau naamini utaishi nao vyema!!!!

Nb: Tuwe na upendo wa dhati kwa kila binadamu bila kujali hali yake ya Maisha.
 
From experience, hamna hard and fast rule kuhusu kuishi nao eti ukijua watakaa sana kwako.

Zingatia tu ubinadamu na mahitaji yao yote namaanisha basic needs wapate. Usimtenge mfano kwenye masuala ya msosi, hakikisha analala pazuri na anaweza kufanya ibada.

Epuka kutumia matusi kejeli ama dharau. As long as umemchukua chini ya paa lako ishi nae kama unavyoishi wa wengine chini ya hilo hilo paa. Apate mda wa kupumzika na muache huru akishaelewa formula ya home ajipangie kazi zake.

Toka nae kwenye family outings. Nina kawaida ya kumwambia ajipikoe chakula cha kwao anachotamani na kama ni halal tunakula wote.

Utafikiri ninae ambae amedumu hata mwaka. Lol.
 
Mkuu ukitaka kuishi na msichana wa kazi vizuri yani mfanye sehemu ya familia yako, mpe Uhuru flani, kuna vitu huwa wanapenda kufanya kivyao kama kula chakula, mle wote sebleni , kwenye ile mitoko ya familia mchukue muwe pamoja

√√ Kuna Yale matoto yanajifanya much know kwa wasichana wa kazi kuwa mkali sana

√√ Msichana wa kazi haimaanishi kazi zote ni zake, hapana kuna sehemu lazima asaidiwe, utakuta anapewa nguo za familia nzima afue

Sent from my TECNO-Y4 using JamiiForums mobile app
 
All in all, wadada ndio wanatakiwa wawajibike zaidi. Maana ile ni ajira kama ajira nyingine.. Changamoto atakazo kumbana nazo kazini, ana wajibu wa kukabiliana nazo kama sehemu ya kazi yake.
Hapo ataishi vizuri tu.
Umeongea vizuri mkuu,ila wengi wao wanakuwa na umri mdogo,hawajajitambua,so kuweza kukabiliana na changamoto za kazi za ndani inakuwa mtihani kwao hasa wanapokutana na mabosi wakorofi.
 
Hata mabinti wa kazi za ndani hawana formula,ila pia namna utakavyoishi nao ndiko kutaamua kudumu kwake kazini.

Binafsi nimepata bahati ya kuwa na mabinti waelewa, huwa wanakaa sana,na hata wakiondoka hubaki kuwa marafiki wa familia,na mwaka jana mmoja ameolewa akiwa mikononi mwangu, mumewe ananiita mkwe..lol.

Ila pia nimeshakutana na wakorofi, mmoja alikuja akakaa wiki,akataka kurudi kwao,nikawa namuuliza pengine shida ni nini,hakusema,anadai jino linamuuma na dawa iko kwao,nikamwambia nimpeleke hsptl akakataa,basi kazi yake ikawa kushinda hapo nje na kabegi kake anataka kuondoka,jioni ikifika anaingia ndani analala kesho yake asubuhi na kabegi tena anashinda nje,nikaamua kumrudisha tu kwao.

Ukimpata aliyekomaa akili anayejua ni kwa nini yuko kazini atadumu .
 
Uwe na ubinadamu jiulize angekua mdogo wako wa tumbo moja ungemtreat vipi,
Msaidie kazi mara kwa mara,anafua we unapika, anadeki we unatenga Meza nk
Akikosa mpe live mweleweshe njia sahihi..mtreat like an equal family member ie mda wa kula kwenda church muwe wote nk
 
Ni bahati tu ukimpata mvumilivu na mwenye utu ishi nae vziuri ika usimsogeze sana karibu yako hasa eti ukinunulia nguo watoto wako nae lazima.

Wwka mipaka ya heshima tangu mwanzo,asiwe boss wa mtoto\watoto wako,unaweza kuta mtoto anamuogopa house girl kuliko wewe.

Kuna mmoja alinichekesha kufika tu kauliza kuna video.
 
Na from time to time mpe uhuru atoke depending na umri..walau akakalie mshedede,japo usimwambie wazi,waweza sema aende akanunue mahitaji binafsi kidogo, au akasalimie rafiki,ndugu etc
ukimbana sana mtashea hapo nyumbani nakwambia
 
Darasa ni popote jamani kuna watu wanaishi na hawa Dada wa kazi kama ndugu zao au Mara nyingine kwa haraka haraka waweza dhania ni mtoto wa hapo hapo,wengine wanakaa na hawa watu mpaka wanaolewa,sisi wengine week moja tu Vingi kashaanza kuulizia kama anaweza kwenda kusalimia kwao,wenye uzoefu wenu karibuni
NI RAHISI SANA,
1. hakikisha anakula chakula kwa uhuru bila woga, kama alizoea home kula sana mwache ale hadi achoke usionyeshe kumshangaa au kumzuia.

2. usija hata siku moja kumsema kwasababu ya chakula

3. mpe majukumu yake afanya, na akishafanya, mpe uhuru wa kukaa kitako kuangalia tv au chochote kinachofurahisha akili

4. usimuonyeshe kwa watu kama yeye ni housegirl, mwite dada, watoto wamwite dada na watu wajue kama ni mdogo wako au ndugu yako. treat her fairly.

5. katika kila jambo unalomfanyia, step into her shoes kama ungekuwa wewe ukafanyiwa hivyo ungejisikiaje.

6. akienda kusalimia kwao, mpe zawadi za kutosha za kwake na zingine awapelekee wazazi wake.

7. weka mipaka kati yako na yeye,

8. watoto wamheshimu lakini yeye pia awaheshimu kwani ni watoto wa boss wao, asiwapige, asiwatishe na muonye asifanye vitendo vya kikatili usipokuwepo kwani ukigundua utamchukulia hatua.

9. weka mipaka na baba mwenye nyumba, wakija toka kijijini huwa wachafu na wamekonda, akikaa mwaka mmoja ananawiri na baba mwenye nyumba ni rahisi kumtamani. hivyo mipaka iwepo, na asikae karibu na baba. baba akikaa sebuleni yeye aende jikoni huko hadi aondoke. watoto wanaweza kuwa karibu na baba lakini sio housegirl, akiwa karibu kwanza hata kama baba hana wazo hilo litakuja tu.

i am talking from experience, nilipokuwa misri nimejaribiwa sana na mahousefirl wangu, nashukuru Mungu alinikomboa almanusura wavunje hata ndoa yangu kwasababu mama aliwaachia mno kunihudumia mambo mengi kwa asilimia kubwa, nikikaa sebuleni wao wanakaa pia, mwishoni uharibiru.​

mengine wataongezea wengine ila kiujumla, treat her with fairness, usimnyanyase na mfanye ajisikie yupo nyumbani wanakompenda, asiwepo utumwani. ukimzuiazuia kula wengine huwa wanaficha vyakula mkienda kulala ndio anaamka anaenda kule, au anakuwa hana uhuru.
 
Umeongea vizuri mkuu,ila wengi wao wanakuwa na umri mdogo,hawajajitambua,so kuweza kukabiliana na changamoto za kazi za ndani inakuwa mtihani kwao hasa wanapokutana na mabosi wakorofi.
Hilo ni tatizo la muajiri! Mi naona kuna vigezo maalumu mtu unatakiwa uwe navyo kabla ya kumuajiri HG. Maana wengine hata utimamu wa akili huwa hawana.

Sometimes unakuta mtu amekaa na mdada wa kazi mwaka 1 au zaidi, hapajui kwao, hajawahi kuwasiliana hata na wazazi/walezi wa HG, na zaidi hajawahi kuchunguza sababu ilimfanya aje afanye kazi za ndani.
 
Na from time to time mpe uhuru atoke depending na umri..walau akakalie mshedede,japo usimwambie wazi,waweza sema aende akanunue mahitaji binafsi kidogo, au akasalimie rafiki,ndugu etc
ukimbana sana mtashea hapo nyumbani nakwambia
Me wangu jumapili mbili kwa mwezi kutembea huko .
 
From experience, hamna hard and fast rule kuhusu kuishi nao eti ukijua watakaa sana kwako.

Zingatia tu ubinadamu na mahitaji yao yote namaanisha basic needs wapate. Usimtenge mfano kwenye masuala ya msosi, hakikisha analala pazuri na anaweza kufanya ibada.

Epuka kutumia matusi kejeli ama dharau. As long as umemchukua chini ya paa lako ishi nae kama unavyoishi wa wengine chini ya hilo hilo paa. Apate mda wa kupumzika na muache huru akishaelewa formula ya home ajipangie kazi zake.

Toka nae kwenye family outings. Nina kawaida ya kumwambia ajipikoe chakula cha kwao anachotamani na kama ni halal tunakula wote.

Utafikiri ninae ambae amedumu hata mwaka. Lol.
Ha haa wanaishia kukaa mda gani?
 
Na from time to time mpe uhuru atoke depending na umri..walau akakalie mshedede,japo usimwambie wazi,waweza sema aende akanunue mahitaji binafsi kidogo, au akasalimie rafiki,ndugu etc
ukimbana sana mtashea hapo nyumbani nakwambia

Acha uoga ww....
 
Back
Top Bottom