econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 22,138
- 32,715
Juzi mzee makamba alitoa kauli yenye ukakasi ambayo ilisema "WAZURI HAWAFI" Hii kauli imeibua hoja tofauti kutoka wanachama wa CCM na wasio CCM . Ukizingatia kauli hii imetolewa na Kiongozi mkuu mstaafu wa CCM.
Mwenyekiti wa CCM Mh Samiah Suluhu Hassan, akirekebisha kauli ya mzee makamba, aliomba radhi na kuelezea kwamba kauli ya Makamba haikuwa na nia mbaya bali kurekebisha kauli ya awali aliposema "KAMA MAMA HATAFIKA 2025 MUNGU ATALETA MTU MWINGINE MZURI" .
Kulingana na Rais Samiah kauli ya Makamba ilikuwa kwaajili ya kuondoa Hali ya kwamba anamuombea mama mabaya, kwamba anaweza kufa kabla ya 2025, hivyo akajirekebisha kwa kusema "WAZURI HAWAFI". Alimaanisha mama Samiah Ni mtu mzuri hivyo hatakufa kabla ya 2025.
Ingawa Mwenyekiti wa CCM Mh Samiah ametoa ufafanuzi kuhusu kauli ya mzee Makamba, bado kuna kundi linadai kauli hiyo ilimlenga Rais amwendazake Mh John Pombe Magufuli, na kwamba ile kauli ya mzee makamba ililenga kuonesha kwamba Mh Magufuli alikuwa mtu mbaya ndio maana amefariki.
Wengi wametukana na kuonesha hasira kwa hii kauli, tena ikitolewa mbele ya mjane wa Mh Magufuli. Lakini nachotaka mimi sio kuonesha ubaya wa kauli ya mzee makamba bali kuuliza swali tumefikaje hapa? Inakuwaje Leo kifo cha Kiongozi kinakuwa mjadala hata Kama hajatajwa moja kwa moja?
Naomba tutafakari Kama watanzania inakuaje Leo Kuna chuki ya wazi Kati yetu. Huyu akifa tunashangilia na huyu akifa tunafurahia. Kwanini tumefikia hapo?. Ni muhimu kuangalia tulipo jikwaa sio kuanguka.
Kauli ya mzee makamba Ni matokeo ya kukubali siasa za chuki na kubaguana, mwishowe hakuna hata mwenye huruma hata na kifo Cha mwingine. Unapoongza watu kwa chuki na kubaguana mwisho wake ni chuki na visasi, lakini unapoongoza watu kwa upendo na amani matokeo yake ni mshikamano watu wanakuwa wamoja
Itakuwa ni unafiki kukasirikia kauli ya mzee makamba wakati Kama taifa tulichekea chuki za wazi tukidhani ni fahari, Leo matokeo yake ndio hayo.
Kuna mambo Kama taifa tuliyachekea ndio yamezaa kauli Kama za makamba.
1. Kwanza, Kuna watanzania wawili mpaka leo miili yao ilipo ni Siri kubwa. Ben Saanane na Azory Gwanda. Lakini Kama taifa tulikaa kimya na kuona ni Jambo sahihi maana walikuwa wapinzani, hasa saa nane. Sio Bunge, Mahakama, polisi au wizara ya mambo ya ndani iliyotoa tamko kuhusu hili, kisa ni wapinzani hawastahili kufanyiwa uchunguzi Wala lolote. Unadhani mke, watoto, ndugu au marafiki wa hao watanzania wawili wanjisikiaje na huko mbeleni wajukuu zao wakilipa kisasi?. ( Mnakumbuka kesi ya Rais wa kwanza zanzibar?)
Kama tuliona kupoteza roho mbili za watanzania bila sababu ya msingi ni jambo la kawaida iweje leo tuione kauli ya Makamba ni mbaya?
2. Pili, Kuna mbunge alimiminiwa risasi hadharani mchana kweupe pale dodoma kwenye makazi ya mawaziri. Kwa sababu alikuwa mpinzani serikali iliona haina haja ya kufanya upelelezi mpaka leo. Polisi wakaja na visingizio vingi ili mradi wasimfanyie upelelezi huyo mbunge Tundu Lissu.
Kama Hilo halitoshi yule mbunge akafukuzwa ubunge wake bila kujali physical au psychological torture aliyopitia. Kama taifa tukaliona la kawaida na kukaa kimya yote yakifanyika.
Sasa Kama tuliona mtu kumiminiwa risasi ni kawaida na hastahili kufanyiwa upelelzi iweje Leo tuione kauli ya Makamba ni mbaya?
3. Tatu, uchaguzi wa 2020. Uchaguzi mkuu wa 2020 ndio ulikuwa hitimisho ya ubaya na ubaguzi wa nchi hii. Wakuu wa wailaya na wakuu wa mikoa na vyombo vya habari na Tume ya uchaguzi vyote viliungana na kuwa timu moja. Nakumbuka ilifika kipindi vyombo vya habari vikawa vinakata maneno kwenye kampeni za wapinzani hasa CHADEMA.
Kwa kifupi CHADEMA walibaki pekee yao mpaka polisi waliingia kwenye kampeni, mpaka Mkurugenzi wa taifa wa Tume ya Uchaguzi akawa na upande kwenye uhaguzi huo ambo kisheria ni makosa.
Nakumbuka RC Chalamila siku ya kupiga kura asubuhi saa moja aliwapiga mkwara wapinzani kule mbeya kwenye Azam TV, kwamba atawalipua na mabomu. Fikiria mkuu wa mkoa anaonesha upande kwenye uchaguzi Tena siku ya kupinga kura.
Kule Pemba JWTZ na Polisi waliweka kambi kule kutisha wanachi. Hata walipouawa wapinzani pamoja na mbunge wao hakuna aliyejali sio polisi, wananchi na hata mimi binafsi maana waliokufa ni wapinzani.
Kama Hilo halitoshi ili kuharibu uchaguzi kabisa mtandao wa internet ulizimwa siku ya kupiga kura. Tufahamu matokeo yanatumwa kwa njia ya mtandao, hivyo kuzimwa kwa mtandao kulirahisisha kupikwa kwa matokeo.
Kama taifa tuliona ni kawaida kwa uchaguzi kufanyika vile na hatukuona shida maana wanaofanyiwa Ni wapinzani. Sisi hayatuhusu. Kama tuliona kuzimwa mtandao wa internet ni Jambo la kawaida iweje tuwe wakali kwenye kauli ya Makamba?.
Kwa kumalizia, niseme hivi tutakuwa wanafiki Sana Kama hayo mambo matatu tuliyachekea na kuona ya kawaida hayatuhusu lakini kauli ya Mzee Makamba inatuumiza, Kama hatuoni thamani ya roho mbili za watanzania , tutakuwaje na uchungu na maiti?.
Ndugu zangu watanzania ubaguzi hauishi, utaendelea mpaka mwisho. Tutakapomaliza kuwabagua wapinzani , tutaanza kubaguana wenyewe. Ndio maana Sasa hivi zimeanza kauli za kanda ya pwani, mara kanda ya ziwa etc. Chuki huzaa visasi, na haitatusaidia.
Hivyo basi tuchague moja tuendelee na kubaguana na chuki? au tusameheane kwa yote tuanze moja Kama watanzania bila ubaguzi.Tukiendeleza chuki na ubaguzi zitakuja kauli za kutisha kuliko hiyo ya mzee makamba na visasi vya kudumu.
SULUHISHO
Kauli ya mzee makamba iwe wake up call au kichocheo Cha kuturudisha kwenye drawing board kama watanzania na tujiulize tumefikaje hapa?. Kwanini Leo hatuna utu, mtu akifa tunashangilia, au akifanyiwa ubaya mtanzania ila kwasababu sio CCM au upinzani tunafurahia?
Tukubali Kuna makosa yalifanyika walioumiza waombe radhi na walioumizwa wakubali kuombwa radhi na kusamehe. Wote Tusameheane tuanze ukurasa mpya na kusahisha makosa kwa kutumia sheria na utashi wa kisiasa.