Tujiulize maswali : Uchaguzi mdogo ( Kinondoni )

Tujiulize maswali : Uchaguzi mdogo ( Kinondoni )

Wakuu ,

Napenda kudeclare interest kwenye ishu inayoendelea mitandaoni na hata katika jamii ya Tanzania kwa ujumla.Sina uanachama wa chama chochote,sishabikii uhalifu,sishabikii uminywaji wa haki za kibinadamu na za kikatiba,sishabikii uvunjifu wa sheria na katiba ya JMT.Mimi ni mtanzania,raia safi na mtii wa sheria bila shurti.

Naungana na watanzania wenzangu kuomboleza kifo cha binti aliyefikwa na mauti pamoja na wengineo katika harakati za uchaguzi katika jimbo la kinondoni.Mungu azipumzishe roho zao pema peponi !

Uchunguzi unaendelea na siyo vizuri kuingilia uchunguzi wa kipolisi kwa kuwa jambo lipo kwenye mikono ya dola tayari.Lakini umma wa watanzania umejawa na maswali mengi.Wadadisi wanasema ili kupata jibu sahihi ni lazima kuuliza swali sahihi.

Naomba tuandike maswali ambayo pengine yakipatiwa majibu yatasaidia kuelezea mnyororo wa matukio yaliyotokea :

1.Ni kwanini mkurugenzi kwa kujua na kutambua umuhimu na unyeti wa zoezi la uchaguzi,acheleweshe barua za mawakala?

2.Je,ni kwanini kama vyama vya siasa(husika) vilikuwa na shida,Mkurugenzi asitoe muongozo mapema kabla ya uchaguzi kusudi watu wapige kura kwa amani na kumchagua kiongozi wao?

Endelea ;
Kulikuwa na uhuni na kukosa uwajibikaji upande wa Tume ya Uchaguzi, msimamizi wa Uchaguzi (Kagurumujuli ) na pia upande wa polisi.

Vv
 
Je , kama silaha zilikuwa zinamilikiwa na waandamanaji/ wafuasi wa vyama (husika) ..ni ushahidi gani umepatikana mpaka sasa ??? (Makasha ya risasi,bunduki )
 
Nitajieni sehemu moja ambako ccm inatakiwa na watz.....ni polisi na tume ya uchaguzi tu ndo wanafanya ccm iendelee kukaa madarakani......
Mwisho wao ukaribu sn sn
Teh teh ee.. mkuu dodoma wanaihitaji sana, kwa kuwa mji wao unafanywa makao makuu!
 
Swali langu ile risasi ilikuwa inamlenga nani?, Nakama ilikuwa imedhamiria kuilenga Costa je waandamanaji walitumia Costa kuandamana?
 
Back
Top Bottom