Tujitafakari

Vivac

JF-Expert Member
Apr 12, 2015
475
479
Wasalaam,

Hope ninyi wazima na kama kuna mgonjwa bas Bwana ampe afya njema.

Kilichonifanya niandke hii thread ni kwa kusudi jema tu la kutaka tukumbushane mambo kadha wa kadha hususani katika matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii.

Inasikitisha sana mtu mzima aliyepewa akili ya kutafakari mema na mabaya, anakaa chini na kuandika mambo ambayo kimsingi hayaleti mantiki yoyote.

Mfano, posts za kufanya mapenzi na mke/mume wa mtu, kufanya ngono na wanawake/wanaume wengi kuliko mwingine na kujitapa kwa kuwa hodari wa ngono, yaani kila wakati ni ngono tu.. Nk.

Hivi jamani ni kweli hii forum n kwa mambo hayo? Badala yake, nilidhani huu ungekua uwanja wa kushauriana mambo mema sisi kama vijana lakini sivyo nilivyotegemea kwa niloyakuta humu.

Nadhani tubadilike sasa, vijana ni nguvu kazi ya taifa, Fanya kazi kwa ajili ya kujijenga mwenyewe, familia yako na taifa kwa ujumla.

NB: Kwa wenye upeo wa kutafakari mambo kwa upana wake, watanielewa. Ila kwa wale ambao kwa bahati nzuri Mungu amewapa akili lakini kwa makusudi wanazitumia vibaya, watatukana.

Tafakari, chukua hatua.
 
Ulivyo wewe ama unachofikiria/kuwaza sio lazima tufanane.

Alafu wote tungekuwa na mawazo sawa ingeboa.

Afu kama hujui JF Kuna majukwaa mengi sana, hapa ni mahusiano, mapenzi na urafiki (MMU) yaliyomo yanaendana na Jukwaa husika.
 
Wasalaam,

Badala yake, nilidhani huu ungekua uwanja wa kushauriana mambo mema sisi kama vijana lakini sivyo nilivyotegemea kwa niloyakuta humu.
Teh! Watu wanaharibu kinomanoma.
 
Kwenye mitandao si kwamba kuna watu tofauti sna na hao wanaotuzunguka kwenye jamii ndiyo sisi tulioko huko kwenye jamii na tabia tofauti tofauti sana ndiyo sisi tupo huku kwenye mitandao...Kuna watu wanaopenda utani, kuna wakorofi, kuna wenye wivu kuna much know, kuna wambea, kuna wazinifu, kuna wacha Mungu nk...Na hakuna interview ya kukufanya uwe member huku ni taratibu unafuata tu na unajoin...
 
Humu kuna hadi jukwaa la kombolela/mchezo wa baba na mama linaitwa chit chat so usighadhabike humu kuna wenye ubongo ulio kamili na nusu kasoro robo
 
  • Thanks
Reactions: Dyf
Wasalaam,

Hope ninyi wazima na kama kuna mgonjwa bas Bwana ampe afya njema.

Kilichonifanya niandke hii thread ni kwa kusudi jema tu la kutaka tukumbushane mambo kadha wa kadha hususani katika matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii.

Inasikitisha sana mtu mzima aliyepewa akili ya kutafakari mema na mabaya, anakaa chini na kuandika mambo ambayo kimsingi hayaleti mantiki yoyote.

Mfano, posts za kufanya mapenzi na mke/mume wa mtu, kufanya ngono na wanawake/wanaume wengi kuliko mwingine na kujitapa kwa kuwa hodari wa ngono, yaani kila wakati ni ngono tu.. Nk.

Hivi jamani ni kweli hii forum n kwa mambo hayo? Badala yake, nilidhani huu ungekua uwanja wa kushauriana mambo mema sisi kama vijana lakini sivyo nilivyotegemea kwa niloyakuta humu.

Nadhani tubadilike sasa, vijana ni nguvu kazi ya taifa, Fanya kazi kwa ajili ya kujijenga mwenyewe, familia yako na taifa kwa ujumla.

NB: Kwa wenye upeo wa kutafakari mambo kwa upana wake, watanielewa. Ila kwa wale ambao kwa bahati nzuri Mungu amewapa akili lakini kwa makusudi wanazitumia vibaya, watatukana.

Tafakari, chukua hatua.
una fikra nzuri ambayo wengi hawajaipenda
 
Nadhani bado hujaitambua jf vizuri, bila shaka nadhani umgeni katika hili jf ni uwanja mpana wenye watu wenye mawazo na mitizamo tofauti. pia jf ni sehemu husika katika ushauri hasa unapohitaji ushauri. Hakuna thread ya mtu aliyejisifu bila kuhitajiu ushauri either wa kujenga ama kubomoa hasa kwa jinsi lisemavyo andishi husika.

Ukitaka ushauri wa maana unaweza kwenda jukwaa la dini lakini hapani sehemu husika kwa kile ulichokisemea na mengineyo.

kuhusu kujisifia ngono nadhani inawezekana hata wewe ushawahi kudate na watu tofauti...so ushauri wako ni mzuri lakini jukwaa hili na mengine yanaruhusu.

USIOGOPE KUONGEA KINACHOKUUMIZA.

Karibu
makapuku
inc
for
life
 
Ushauri mzuri. Hapo kwenye "sisi kama vijana" umeteleza kidogo. Humu kuna wazee 50+ wana nondo balaa. Kuna watoto pia -25
 
Kwakweli binafsi nafurahiya vituko humu jamvin ila pia kuna wakati mwingine watu wako serious kulinga na post itakavyohitaji.

Mambo mengine usichukulie serious sn humu utaumia moyo bure.
 
mimi naona lisibadilike sana aiseee, maana hii JF hasa hapa MMU pamenitolea stress nyingi sana siku hizi ukikutana na mimi ni full furaha. cha kufany hapa ni kuchukua vile vinavyokupendeza na vile vibaya unaviacha.

Kuwa huru Mkuu na usipende mtu aibe furaha yako kamwe.
 
wazo lako zuri na una nia njema sana.....MMU inahusu kila mtu.... ....chukulia lilivyo tuu...
 
Back
Top Bottom