Tujitafakari kama kwanini mamlaka ya Serikali yanatoka kwa wananchi

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Nilitahadharisha yatakayo tokea kwenye chaguzi zetu, nikashauri tuandike historia mpya ili kulinda amani ya nchi yetu, nikasema, vyama vitapita Tanzania itabaki lakini kilicho tokea vyama kwanza Tanzania watajua wao.

Uchaguzi umegeuzwa uwanja wa mapambano ya silaha na si hoja. Vyombo vya dola na silaha zilizo nunuliwa kwa kodi za wananchi ndizo vikwazo vya kutunza amani yetu.

#Matukio ya chaguzi mbalimbali nchini yaliyo fanyika jana yameinajisi demokrasia, yamelipaka doa la damu ya wasio na hatia taifa letu.

Haki ya watanzania wanyonge chini ya rais wao ina dhulumiwa, watanzania kwa watanzania wanahasimiana kwa mapanga na silaha mbalimbali eti kwa kuwa tu uhuru uliopatikana kwa mtutu wa bunduki hauwezi kutolewa kwa njia ya karatasi.

Swali, wanao nyimwa haki zao ni wageni au watanzania. Inakuwaje form za nakala kwa mawakala wa vyama shiriki katika uchaguzi vizuiliwe kwa mamlaka ya juu!!!?? Mamlaka hii ni ipi?

#Tuna lazimishwa utengano kwa kuunda matabaka ya wenye haki(wavunja sheria) na wasio na haki (watetezi wa utawala wa sheria). Haya yote ni kwa maslahi ya nani ikiwa wote ni watanzania.

#Tupingane bila kupigana, kwa hili linalo tokea lina haribu sura ya Tanzania kwenye sura ya dunia na kuifanya Tanzania kuwa si sehemu salama ya kuishi.

#Katibu mkuu msomi wa CCM anasema, CCM imerudi kwenye misingi ya waasisi wa taifa hili, je ni kweli waasisi hao walipuuza matakwa ya wananchi. Je ni kweli Azimio la Arusha lilisimamia misingi ya uchaguzi kwa kumwaga damu!!!

#Tanzania imepotezwa taswira yake, jeshi la Polisi limekuwa sehemu ya Tume, sehemu ya chama cha mapinduzi.

Kwa mantiki hii kuna haja gani ya kuwa na uchaguzi ikiwa matokeo ya uchaguzi yana amuliwa na mamlaka ya juu. Ikiwa uchaguzi una sababisha umwagaji damu kwa wananchi wa taifa hili!!!

#Kubwa zaidi watanzania tujitafakari kama tubastahili kufanya chaguzi zenye kupoteza rasilimali watu, muda lakini matokeo yapo chini ya mamlaka ya juu!!!

#Lingine jipya baada ya kutengeneza matabaka ya uporaji haki za uchaguzi, vinara wale, wakurugenzi wa uchaguzi waliopokea maagizo toka mamlaka ya juu wamehamishwa Leo asubuhi baada ya kazi kubwa ya kupora maamuzi sahihi ya wananchi.

Hii ina liingiza taifa kwenye mfumo mpya na utawala mpya kabisa kinyume na katiba ya Jamhuri ya Muungano, ambayo ina amini madaraka na mamlaka ya serikali yatatoka kwa wananchi na serikali msingi wake mkuu ni ustawi kwa wananchi wake.

Turudi tujitazame kama kweli tunakubali kupokea mfumo mpya usio jali ya matakwa ya wananchi.
 
Back
Top Bottom