"Tujisahihishe" 2018

"Tujisahihishe" 2018

DR. MWAKABANJE

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2012
Posts
1,986
Reaction score
3,151
Kheri ya mwaka mpya!

Tukiwa na muda mchache tangu tuuanze mwaka ni vyema tukajikumbusha maneno ya baba wa taifa hili Mwl. Nyerere ili tuweze kuanza mwaka na tafakuri nzito juu ya makosa yetu kama taifa na kuyasahihisha makosa hayo, ujumbe huu alipata kuutoa May 1962 lakini ni Ujumbe mzito uliobeba maono ya taifa letu pengine kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Nitanukuu hotuba hiyo lakini pia nitaweka hotuba yote kwa PDF ni fupi sana ni vyema tukaisoma kwa kujikumbusha tu.


"TUJISAHIHISHE"


Umoja wa kundi lolote ni sawa sawa na umoja wa viungo mbalimbali vya mwili au mtambo. Viungo vya mwili havina budi vitii kanuni zinazoviwezesha kufanya kazi yake sawa sawa. Lakini haviwezi kutiii kanuni hizo kama haviko katika Kali ya afya njema. Mara kiungo kimoja kinapokuwa hakina afya safi, huanza kuvunja kanuni za kazi na mwili mzima hupata taabu.
Umoja wa Binadamu ni kadhalika. Hauwezi kutimiza madhumuni yake bila viungo vyake vyote kutiii kanuni zinazouwezesha umoja wa binadamu kufanya kazi zake sawa sawa. Nataka kutaja makosa machache ambayo mara nyingi huzuia Umoja wo wote kuwa imara hata ushindwe kutimiza madhumuni yake.

Ukiondoa matatizo wayapatayo binadamu kwa sababu ya mambo kama mafuriko, nzige, kiangazi, n.k., matatizo yao mengi hutokana na unafsi. Unafsi ni wa aina nyingi. Swali ambalo twalisikia mara kwa mara, "Hali yetu ya baadaye itakuwaje?", ni swali amblao sina shaka kuna watu wanaouliza kwa nia safi kabisa. Lakini mara nyingi linalotokana na unafsi. Mtu anayeu-
liza anafikiri kuwa T.A.N.U. iliundwa kwa faida yake yeye binafsi. Ni kama kwamba T.A.N.U. ilipoundwa ilimwahidi kwamba ikiwa atakubali kuwa mwanachama, au kiongozi, basi T.A.N.U. itamfanyia yeye jambo Fulani kama tunzo! Anasahau kabisa kuwa T.A.N.U. inajishughulisha na haja za Jumuiya kwa ujumla. Lakini kwa mtu wa aina hiyo, hata kama T.A.N.U. inatimiza madhumuni yake ya Jumuhiya, ataona kuwa ni umoja ambao hauna maana kwa sababu haum-
timizii haja zote za nafsi yake! Huu ni unafsi. Kama wanachama wa T.A.N.U., na hasa viongozi, hawatakihukumu chama chetu kwa mahitaji ya Jumuiya, bali watakihukumu kwa mahitaji ya nafsi za wenyewe, chama hakitadumu. Wanach-
ama wa aina hiyo ni ugonjwa katika chama.

Dalili nyingine ya unafsi, na ambayo ni ugonjwa mbaya sana, ni fitina. Kanuni moja ya T.A.N.U. inasema hivi: "Nitasema kweli daima. Fitina kwangu ni mwiko." Lakini bado tunao wanachama ambao niwafitini wakubwabila kujitambua. Ni wa aina mbalimbali.

Wengine humwona mwenzao anafaya kosa. Badala ya kumwambia pale pale kijamaa kwamba atendalo ni kosa, watanyamaza kimya Lakini hawanyamazi kabisa! Watakwenda kumteta katika vikundi vya sin sifi. Mateto haya si ya kumsaidia mwenzao, ni ya kumdhuru. Hii ni aina moja ya fitina. Wengine hugawa watu katika mafungu. "Fulani" japo akifanya kosakubwa sana hasemwi. Lakini "Fulani" wa pili akifanya kosa japo dogo, kosa lile hukuzwa likawa kama mlima Kilimanjaro. Hawa hutafuta sababu za kumtetea "Fulani" wa kwanza, au za kumlaumu "Fulani" wa pili, ambazo hazifanani kabisa na ukweli. Kwa watu wa aina hii, ukweli ni jambo ambalo hutegemea mtu-si kitu kinachojitegemea chenyewe bila kujali mtu. "Fulani" wa kwanza akisema katika majadiliano kuwa mbili na mbili ni tano, wao watakubali. Lakini "Fulani" wa pili akisema sivyo, mbili na mbili nne, watamwona ni mtu mbaya kabisa ambayo hastahili hata kusikilizwa. Hawa hawajali ukweli, hujali nafsi tu. Kwao, ukweli ni maoni yao na matakwa yao. Hatuna budi, hasa katika majadiliano na mazungumzo yanayohusu Jumuiya, tujifunze kusikiliza hoja zenyewe zinazotolewa na wenzetu, na kuzijibu zile hoja kwa kuzikubali au kuzikataa, bila kujali kama aliyezitoa ni rafiki au si rafiki. Pia wanaopingwa hawana budi wakubali kuwa kinachopingwa ni zile hoja zao, siyo wao wenyewe. Bila mazoea haya, mazungumzo hayana maana ; yanakuwa ni kupoteza wakati, maana huwa tumekwisha kuzihukumu hoja za mtu hata kabla hajazitamka! Kadhalika, hoja zetu zikijibiwa kwa kupingwa halafu tukawakasirikia waliozipinga tunafanya mazungumzo yasiwe na maana, kwa sababu tunapenda hoja zetu zikubaliwe tu hata kama si hoja safi.
Ukweli una tabia moja nzuri sana. Haujali mkubwa wala mdogo; haujali adui wala rafiki. Kwake watu wote ni sawa. Pia ukweli unayo tabia ya kujilipiza kisasi kama ukipuuzwa. Ukiniona nataka kulipiga teke jiwe kwa kuwa nafikiri kuwa ni dongo au mpira, natumaini utanionya. Lakini nikilipuuza onyo lako kwa sababu eti wewe ni mdogo au kwa sababu sikupendi, nikalipiga teke, basi litanivunja dole japo ningekuwa nani. Ukweli haupendi kupuuzwapuuzwa!

Wakati mwingine, mtu tunayempinga huwa ana makosa kweli, lakini hoja tunazozitoa ni za kinafsi na hazihusiani kabisa na hoja zake. Nikisema mbili na tatu ni sita, nakosa. Lakini ni bora kunionyesha kwamba pengine nafikiri tunazidisha kumbe tunajumlisha. Ni kweli mbili mara tatu ni sita; lakini mbili na tatu ni tano, siyo sita. Lakini ukijaribu kuwashawishi wenzetu wakatae mawa-
zo yangu na kukubali yako kwa kusema kuwa meno yangu ni machafu, au natoa kamasi daima, utakuwa unatumia hoja ambazo hazina maana. Huu ni mfano wa upuuzi ; lakini mara nyingi hoja tunazotumia kuwashawishi watu wakatae mawazo ya wale tusiowapenda, au kukubali mawazo yetu, huwa hazihusiani kabisa na mambo tunayoyajadili.

Makosa yetu mengine hutokana na woga ; woga unaotuzuia kumlaumu mkubwa japo tunajua kuwa kakosa, au kumtetea mdogo anayelaumiwa na wakubwa japo tunajua kuwa hana makosa. Na msingi wa woga pia ni unafsi. Pengine huwa tunaogopa sisi wenyewe kulaumiwa au kupata hasara fulani.
Pengine twaweza kuwa hatuna cheo cho chote abacho tunaogopa kupoteza; pengine huwa hatuna wala tamaa yo yote ya kupata cheo fulani. Lakini woga unaweza kutokana na tamaa ya kila binadamu kupendwa na binadamu wenzake. Sisi wote tunayo tamaa hii, au sivyo tusingekuwa binadamu. Woga huu huweza ukamfanya mtu kuvumilia maovu, hasa kama maovu yale yanatendwa na walio wengi kwa walio wachache, au yanatendwa na wakubwa kwa wadogo. Kwa kuogopa kuwaudhi wengi tunawaacha watende makosa bila kuwasahihisha, wasije wakatuchukia. Huu ni unafsi mbaya sana. Ni kweli kwamba democrasia haiwezi kudumu ikiwa wachache hawatakubali matakwa ya wengi. Lakini matakwa ya wengi hujulikana katika majadiliano au mazungumzo ya wazi wazi.

Kadhalika, matakwa ya wachache hujulikana katika majadiliano na mazungumzo Bila wale wachache kusema wazi wazi matakwa yao, majadiliano hayana maana. Wakati mwingine, hata baada ya majadiliano, wachache-japo wamekubali kutii uamuzi wa wengi-wanaweza kuendelea kuamini kwamba mawazo yao ni sawa, na ya walio wengi yamepotoka. Democrasi inawapa haki, na ukweli unawapa wajibu wa kuendeleza mawazo yao mpaka wengi waone kuwa ni ya kweli. Bila hivyo maendeleo katika mawazo hayawezekani, kwani mara nyingi wazo zuri hutokanan na mtu mmoja tu. Mwanzo laweza likapingwa, pengine kwa nguvu kabisa, na walio wengi, lakini hatimaye wengi hulikubali. Huu ndio msingi wa maendeleo katika mawazo ya binadamu.
Makosa ni makosa na dhuluma ni dhuluma, japo watendao makosa hayo au dhuluma ile ni wakubwa au ni wengi. Chama kinachopenda ukweli na haki hakina budi kiwape wanachama wake uhuru na nafasi ya kusahihisha makosa na kuondoa dhuluma. Wananchama hawana budi waone kuwa ni wajibu wao kuutumia uhuru huo, na nafasi hiyo. Wanachama wasiotumia uhuru huo na nafasi hiyo, kwa sababu ya kuogopa kuchukia au kupoteza nafasi zao, wanafanya kosa kubwa la unafsi, ambalo ni adui wa haki na ukweli.

Kosa jingine linalotokana na unafsi tunalifanya wakati wa kuchagua viongozi. Wakatimwingine hufanywanawanachama; wakatimwingine hufanywana viongozi wenyewe, au wale wanaotaka uongozi. Nimesema mahali pengine kwamba viongozi wetu hawana budi watokane na WATU. Viongozi wa T.A.N.U. hawana budi watokane na wanachama wa T.A.N.U. wenyewe, bila hila, vitisho, rushwa, au ujanja wa aina yoyote. Lakini mara nyingi wanachama huchagua viongozi bila kufikiri kwa makini kama viongozi hao wanaiweza, au hawaiwezi, kazi wanayochaguliwa kufanya. Wanachama wetu watafanya makosa makubwa sana ikiwa watachagua viongozi wao ovyo tu. Hii ni jambo la hatari kwa democrasi na chama chetu, na maadui wa T.A.N.U. wanaweza kusema kwamba democrasi haina maana kwa sababu haizai viongozi wanaoweza kazi zao! hii
si kweli, maana wote twajua kwamba democrasi inaweza kuchagua viongozi wazuri. Lakini ni wajibu wetu katika kuhifadhi democrasi kuona kuwa inachagua viongozi ambao wanaziweza kazi zao. Kazi ya kuchagua viongozi ni kazi ya wanachama wetu ; lakini viongozi wetu wanaweza kusaidia kwa kuelezea wanachama wetu kwamba jambo hili ni kubwa sana. Haifai kuchagua kiongozi kwa sababu ni mjomba, au binamu au ana sauti au sura nzuri. Wala haifai kuacha kumchagua mtu kuwa kiongozi kwa sababu kama hizo. Jambo kubwa ni kuchagua kiongozi mwenye tabia nzuri na anayeiweza kazi. Hatuna budi tutii kanuni hii katika kuajiri wafanya kazi katika T.A.N.U. au Serikalini. Hawa pia hawana budi wachaguliwe kwa sababu wanaiweza kazi wanayoajiriwa kufanya, na ni watu wenye tabia nzuri.
Kosa jingine ni kutojielimisha. Kanuni yetu moja inasema : "Nitajielimisha kwa kadiri ya uwezo wangu wote na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote". wengi wetu hufikiri kuwa kujielimisha ni kwenda kivukoni, au kupata nafasi kwenda kusoma katika nchi za nje. Wengine hufikiri kuwa kujielimisha ni kujua kusoma na kuandika. Hilo ni kosa, lakini si kubwa kama la pili. Wengi wetu, hasa baadhi ya viongozi, hufikiri kuwa tunajua kila kitu na hatuna haja kujifunza jambo lo lote zaidi. Mtaalamu mmoja wa zamni alisema kuwa mwanzo wa elimu ni kutambua kuwa hatujui kitu"

Nimesema kwamba wengine wetu wanafikiri kuwa kujielimisha ni kwenda Kivukoni au kupata nafasi kwenda kusoma katika nchi za nje kwa kweli moja ya taabu zetu kubwa ni kwamba watu wengi sana wangependa wapate nafasi ya kwenda kusoma katika nchi za nje, na chama kinashindwa kuwaridhisha wote, Tamaa ya kupata elimu ni tamaa nzuri sana ; ndiyo maana kupata elimu ni moja ya kanuni zetu tisa. Lakini kudai kwenda kupata elimu nje ya Tanganyika au pahali fulani, na halafu kunung'unika matakwa yetu yasiporidhishwa, ni jambo lisilokuwa na msingi. Tunajua kwamba elimu ni jambo la lazima kwa kila raia. Lakini tunajua pia kwamba kila raia hawezi kupata nafasi ya kwenda nje ya Tanganyika kupata elimu; au kuingia pahali fulani kupata elimu. Jambo la maana ni kujua ziko nafasi ngapi nje ya Tanganyika, au ndani ya Tanganyika na kama T.A.N.U. na Serikali huzijaza nafasi hizo kwa njia ya haki.
Kujielimisha siyo maana yake kwenda shuleni. Kama hivyo ingekuwa ndivyo, T.A.N.U. ingekuwa imefanya kosa kubwa sana kumtaka kila mwanachama ajitahidi kujielimisha na kutumia elimu yake kwa ajili ya wote. Kujielimisha ni kutafuta ukweli wa mambo. Kwenda shule hutusaidia. Lakini japo hatuwezi
kwenda shule twaweza kjifunza. chetu hakina maji ya kutosha. Kujieli-
misha ni kujua kwa nini chetu hakina maji ya kutosha: na baada ya kujua
sababu yeke, lazima tujielimishe zaidi kwa kutafuta njia zinazoweza kukipatia
kijiji chetu maji ya kutosha. Au kijiji chetu kina ugomvi daima. Kujielimisha ni kutafuta sababu za kweli zinazofanya chetu kiwe na ugomvi daima na baada ya hapo kutafuta njia za kuondoa ugomvi katika kuiji chetu. Elimu ya kweli ni ujuzi wa sababu za mambo mbalimbali; na kama ni mambo mabaya, ni kujua jinsi ya kuyaondoa; na kama ni mema, jinsi ya kuyadumisha. Mpumbavu ni yule anayeyapa mambo sababu zisizo za kweli na kushauri dawa isiyo ya kweli katika kutafuta sababu za matatizo, na jinsi ya kuyaondoa. Kila mmoja wetu anacho chombo cha kutumia-akili yake. Jambo la maana ni kuzipa akili uhuru kamili wa kutafuta elimu. Bila kutiwa kiinimacho na utashi wetu wa unafsi.

Watu walio hatari sana ni wale ambao wanafikiri kuwa wanajua kila kitu, wala hawana haja kujifunza zaidi. Hii ni tabia mbaya ambayo huzuia kabisa maendeleo. Sababu moja ambayo ilituzuia sisi Waafrika kuendelea ni majibu ya urahisi kwa matatizo makubwa. Shamba letu kama halikutoa mavuno ya kutosha, jibu lilikuwa wazi: au limerongwa au ni amri ya Mungu. Watoto wetu walipokuwa wagonjwa daima, jibu lilikuwa rahisi: au wamerongwa au ni amri ya Mungu. Nyumba yetu ilipopigwa radi ikaanguka, jibu lilikuwa rahisi: au ni uchawi au ni amri ya Mungu. Majibu ya namna hii huzuia binadamu kupata sababu za kweli za matatizo yao, na kwa hiyo yanazuia akili kutafuta njia za kweli za kuondoa matatizo hayo.

Siku hizi, tumeanza kutumia majibu mengine rahisi. Mambo yakienda mrama, badala ya kutumia akili zetu na kutafuta sababu za kweli, tunalaumu Wazungu, au Wahindi, au Ukoloni, au Ukoloni-mpya, au Vibaraka, n.k. Yawezekana kweli kwamba kosa ni la Wazungu, au Wahindi, au Ukoni, au Ukoloni-mpya, au Vibaraka n.k.-lakini yafaa akili ifikie jibu hilo baada ya uchunguzi wa kweli, siyo sababu ya uvivu wa kutumia akili! Uvivu wa kutumia akili unaweza kutufanya tutumie dawa kuondoa matatizo ambayo si dawa hata kidogo. Nikienda kwa mgaga anitibu maradhi yangu, namtazamia kuwa kazi yake ya kwanza ni kujua hasa, siyo kwa kubahatisha, naumwa nini; kazi yake ya pili ni kujua sababu ya ugonjwa wangu; kazi yake ya tatu ni kujua dawa ya ugonjwa wangu. Daktari asipojua ugonjwa wangu na sababu zake hawezi kujua dawa yake Akinipa dawa nikapona, atakuwa kaniponya kwa bahati tu, kwa desturi daktari wa namna hiyo hawezi kumponya mgonjwa, na ni daktari wa hatari sana.

Kadhalika, chama ambacho nia yake ni kuwa daktari wa matatizo ya Jumuiya hakina budi kiwe na tabia ya kujua matatizo yenyewe, sababu za matatizo hayo, na dawa yake. Bila kujua matatizo na sababu za matatizo hayo hakiwezezi kujua dawa yake. Daktari anayejidai kuwa anajua kila kitu, na kumbe hajui kitu, ni hatari zaidi kuliko daktari anayekiri kuwa hajui kitu. Kadhalika, kiongozi anayejidai kuwa anajua kila kitu, na Kumbe hajui, ni hatari zaidi kuliko yuleanayekiri kuwa hajui kitu na yuko tayari kujifunza. Kwa kweli huyu wa pili si hatari hata kidogo, kwa sababu kama nilivyosema mapema, ufunguo wa elimu ni kule kutambua kuwa hatujui kitu!

Kosa jingine, na hili husumbua na kubabaisha sana wenzetu, ni kuyafanya mawazo na matakwa ya nafsi zetu kuwa ni mawazo na matakwa ya raia. Nimesema mbeleni kwamba hatuna budi tuone daima kwamba mambo tunayoyazungumza yanatokana na watu, au mawazo yetu yanakubaliwa na watu. Mara nyingi jambo hili halitokei. Kuna wenzetu ambao wakileta madai ambayo wanajua kuwa yatakataliwa na wenzao kwa sababu hayana maana, basi huyahimili kwa kusema kuwa ni madai ya wananchi. Mara ngapi tumesikia viongozi fulani wakisema: "Wananchi wote wa upande ninaotoka wanataka jambo hili?" Viongozi hawa huwa mara nyingi hawakuzungumza jambo hilo na mwananchi ye yote. Lakini hawaoni haya kuja kubabaisha wenzao kwa kusema kuwa ni jambo linalotakiwa au li s ilotakiwa nawananchi wote ! Tabiahiinimbayakwa sababuinaondoa ukweli katika mazungumzo. Ni njia fupi ya kujaribu kuonyesha kwamba mtu asiyekubaliana na kiongozi huyo basi anapinga mawazo au matakwa ya wananchi wote.
Kosa jingine kubwa ni kuwagawa watu katika makundi; kundi "letu" na kundi "lao". Wakati mwingine "sisi" ni viongozi tunaochaguliwa kwa kura za wanachama. Hili ndilo kundi "letu". Viongozi wengine ni wale wanaoajiriwa. Baadhi ya viongozi wanaochaguliwa hujiona kuwa ni mabwana, na kwamba viongozi wanaoajiriwa ni watumishi to ambao hawastahili kuheshimiwa. Lakini mara nyingi viongozi wengi wanaoajiriwa huwa wanawazidi wengi wa wale wanaochaguliwa katika mambo ya elimu. Basi, wao pia huunda "ubwana" wa elimu na kupuuza viongozi waliochaguliwa. Kosa hili kwa pande zote mbili ni baya. Linagawa viongozi katika makundi, na ni wazi kwamba viongozi wakigawanyika katika makundi Chama pia huwa kimo katika hatari ya kugawanyika katika makundi na kukosa shabaha yake.

Lakini pengine huwa kundi "letu" ni kubwa zaidi. Kwa mfano, japo baadhi ya madhumuni ya Chama chetu ni kumpatia elimu kila mtu, baadhi ya wanach-
ama wetu huwa na mashaka na watu wenye elimu-siyo kwa sababu ya makosa yanayojulikana, lakini kwa sababu ya elimu. Tabia hii inaleta mazoea ya kuse-
ma na kukashifu elimu na ujuzi kama kwamba ni dhambi. Na hasa kwa sababu Wakoloni zamani walikuwa wakituambia kuwa hatuwezi hili wala hatuwezi Tile kwa sababu hatuna elimu na ujuzi wa kutosha, basi leo, kiongozi akisema kwamba kazi fulani inahitaji elimu na ujuzi wa kutosha, huonekana kuwa ana mawazo ya kikoloni! Lakini ni dhahiri kwamba chama cho chote ambacho kimetajwa "Ujinga"-yaani ukosefu wa elimu au ujuzi-kuwa ni baadhi ya maadui wake,
hakina budi kiheshimu elimu na kiitumie. Ni dhahiri kwamba yule asiyetambua ubora wa elimu na ujuzi ni mjinga ambaye chama hakina budi kimsaidie kwa kumwondolea adui huyo anayemsumbua, yaani Ujinga! Mtu ye yote akikosa na tumlaumu kwa makosa yake, lakini tusimtilie mashaka bure kwa sababu ya elimu, kwani kuwa na elimu si kosa.
Mara nyingi wenye elimu hufanya kosa hili hili la kuwatilia mashaka au kuwadharau wale wasio na elimu. Mara ngapi tumesikia watu wakikashifu halmshauri fulalani siyo kwa kosa lo lote ambalo limefanywa na halmashauri hiyo, lakini kwa sababu halmashauri yenyewe ni ya watu ambao hawana elimu? Hili ni kosa linaloudhi zaidi. Mtu ambaye kapewa nafasi ya kuweza kuona anapofanya mambo kama kipofu hukatisha tamaa zaidi kuliko kama angekuwa ni kipofu kweli.
Pengine kundi "letu" ni la Waafrika kwa jumla, na kundi "lao" ni la Wasio Waafrika kwa jumla. Hasa katika nchi kama yetu mgawanyo huu unayo hatari ya kuzuia akili ya baadhi ya ndugu zetu kufanya kazi kabisa. Kwa ndugu zetu kama hao asiye wa kundi "letu" hawezi kusema lo lote lenye maana. Lo lote atakalolisema au kutenda huwa ni baya. Baadhi yetu hata wameanza kusema kuwa sisi Waafrika ni watu bora kuliko watu wa mataifa mengine. Huu ni ugonjwa ule ule nilioutaja mapema unaomfanya mtu kuzihukumu hoja za mwenzake kuwa ni nzuri au mbaya kabla hata hajazisikia.
Pengine kundi "letu" ni sisi WanaTANU, na "lao" ni la wale wasiokuwa WanaTANU. Kwa mfano, baadhi ya WanaTANU husahau kabisa kuwa baadhi ya Watumishi wa Serikali ni wananchi safe kabisa kama sisi, na pengine kuwazidi wengine wetu. Lakini kwa sababu hawana kadi za TANU, basi hufanywa kuwa si kitu. Pengine huongezeka kosa lile lile la kuwafanya wao kuwa ni watumishi tu ambao hawastahili heshima yo yote ya utu. Pengine, kwa sababu baadhi yao wanayo elimu nzuri, huongezeka kosa lile la kuwatilia mashaka wenye elimu. Sisemi kwamba huwa hawana budi wahukumiwe kwa makosa yao ya kweli, si kwa kubwagwa tu katika kundi la walaumiwa bila makosa yao wenyewe.
Mungu ametupa akili ili tuweze kuzitumia kwa manufaa yetu na ya Jumuiya. Makosa niliyoyataja, na mengine mengi ambayo kila mtu aweza kuyafikiria mwenyewe, huzinyima akili uhuru wa kufanya kazi yake barabara. Huwa kama ni kutu inayokizuia chombo kufanya kazi yake vizuri. Ni wajibu wetu kujitahidi kadiri iwezekanavyo kuzipa akili zetu uhuru wa kufanya kazi bila kutu na uchafu wa aina nilioutaja.
Yawezekana kuwa mara nyingi makosa tunayofanya sisi hutokana na makosa ya wengine. Kumtia mashaka mtu anayekutilia mashaka ni jambo la kibinadamu.

Kumrudishia kofi mtu aliyekupiga kofi ni jambo la kibinadamu siyo kusema kuwa ni cha busara. Kipofu akinivamia na kuniumiza, nikikasirika kwa sababu ya mauamivu aliyonitia, ni jambo la kibinadamu. Lakini nikijitoboa macho ili na mimi nimvamie ni kumwumiza haitakuwa nimefanya jambo la busara.

Nimejaribu kueleza makosa machache ambayo yafaa tuyaondoe na kuyaepuka katika chama chetu. Sitaki Mtu ye yote afikiri kuwa mimi niliyeandika maneno hayo sinayo makosa hayo. Hivyo si kweli. Kosa moja kubwa sana ambalo pia linatokana na unafsi ni kutaja makosa ambayo sisi wenyewe hatunayo, na kuficha makosa ambayo sisi wenyewe tunayo. Hii ni kosa lile lile linalotufanya tulaumu tusiowapenda, na kutolaumu tunaowapenda, bila kujali ukweli. Nimetaja makosa haya iii yatusaidie, siyo katika kuwahukumu wenzetu to ambalo ni jambo rahisi, lakini katika kujihukumu sisi wenyewe, ambalo ni jambo gumu na la maana zaidi.



Mwisho

Nb. Attachment ya PDF inanigomea!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom