Ipi dot com
JF-Expert Member
- Mar 28, 2011
- 306
- 166
Hili Life ndo lakikamanda...Inaendelea....
Siku hiyo kumbe basi moja halikufanya safari kati ya mawili ambayo yalikua yanaenda lusaka mpk Harare hivyo ilibidi abiria wa
Basi nyingine tuingie kwenye basi
Moja.
Kwa kweli hali ilikuwa mbaya sana maana basi lilijaa sijawai ona maana kama unavyojua wafanya biashara wanakuwa na mizigo mingi mno ilikuwa huwezi hata kusogeza mguu ukizingatia hatukupata siti.
Tulisafiri usiku kucha tukiwa tumesimama takribani km 800 kwa kweli hali ilikuwa mbaya sana asubuhi tukafika mji wa kapili pale ndio tukapata siti zilibaki kama km 200 tufike lusaka kwa jinsi tulivyochoka ilikuwa kama km moja tu mpaka lusaka.
Tukafika asubuhi ile tukauliza wenyeji malazi ya bei rahisi tukapata pa kulala,nilipata usingizi mzito haijawai tokea.
Baada ya siku moja tukakata tiketi tayari kwa safari ya harare,kesho yake mapema tukawa ndani ya basi kuelekea zimbabwe.
Tukasafiri hadi mto zambezi ni mpakani ikabidi tuchenji kwacha kuwa zimdorar(pesa ya zimbabwe)
Kama kawaida pale boda kuna utaratibu wa kujaza fomu za uhamiaji kuna kipengere unajaza show money ndugu yangu john akaandika kiasi chote tulichokua nacho, kumbe kisheria za kwao ilikuwa kosa
Wakamwambia hebu lete hiyo hela tuone loo kumbe ilikuwa bonge la kosa alipo itoa tuu wakachuku hela zote na kuanza kutusomea sheria zao na kutuambia mnaruhusiwa kudai baada ya miezi sita.
Hapo nilihisi kuona nyota nyota maana hatubakiwa na hela yoyote kwa kweli tulichanganyiwa sana
Baada ya hapo safari iliendelea tunaenda ugenini hatuna hata senti
Itaendele...
Sent from my SM-J730G using JamiiForums mobile app
Kweli kabisaaaHili Life ndo lakikamanda...
Hapo haina kukata tamaa wala kulegeza...
Walamba midomo wa humu JF wataona kama Geni sanaa na wata skizia sanaa muendelezo.
Any way hata mimi nina langu...
Siku ntadondosha
Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Twende kazi....
Baadae sana wale viongozi wakaniita nijieleze huyo mchungaji alieko harare namfahamu kivipi,nikawaeleza kuwa ni rafiki yake babaangu japo yeye hanifahamu mpaka nikajieleze.
Kumbe kati yao mmoja wao alikuwa na safari ya kwenda harare hivyo wakaniambia hawana imani na mimi hivyo nitakaa nyuma kwenye pick up yake nikaona fresh na gari yenyewe imefunikwa kwa hiyo nikakubali,jamaa kanipeleka kwake tukala kisha safari inaanza ya km 400 na ushee.
Usiku saa mbili tunafika kwa huyo mchungaji maeneo karibu harare university,jamaa kagonga hodi mala anatoka kijana mmoja anatusalimu kisha anatukaribisha ndani.
Ndani tunamkuta mwenyeji baada ya salamu(kwa kiingereza) jamaa anamwelekeza mchungaji (hapo jamaa alikuwa na hofu kuwa huenda nikakataliwa)
Jamaa akamueleza kuwa huyu mtu kapatwa na changamoto ya viza lakini kakutaja wewe kama ndugu yako hebu msikilize,mzee kaniuliza kwa kimombo unatoka wapi?
Mimi:Tanzania
Mzee; hujambo
Mimi; sijambo shikamoo
Mzee: unatoka mkoa gani?
Mimi :mbeya
Mzee; unaitwa nani?
Mimi; lukaa (si jina halisi?
Mzee: babaako?
Nikamtaja yaani kufumba na kufumbua nilikumbatiwa na familia nzima yaani mama mtoto na baba kumbe mama alikuwa sehemu anasikia kila kitu na aliposikia jina baba alifurahi mno kwa kweli nikasahau shida zangu kwa muda.
Yule jamaa alienileta alifadhaika sana kwa jinsi nilivyopokelewa....
Sent from my SM-J730G using JamiiForums mobile app