Balantanda
JF-Expert Member
- Jul 13, 2008
- 12,484
- 4,821
Nimefurahi kuiona thread ya wadau wa Ilboru napenda na siye wa Umbwe tujikumbushe japo kidogo baadhi ya misamiati tuliyokuwa twaitumia pale 'Mti safi'..Baadhi ya misamiati ni kama: Fongo (Uji),, Katizi (Maandazi ya ubapa marefu hivi),, Maini (Maharage),,,, Fulu (Mbege)-lol nimeimiss,,, Maputo (Vyoo vya shimo kule juu dorm 8 na 9 Ukitaka kuingia wavua nguo zote ukiwa nje otherwise darasani hakutakalika). = Wadau nipeni misamiati mingine..Naikumbuka sana Umbwe a.k.a Mti safi a.k.a Umbwe Dume..Nakumbuka kipindi nasoma alikuwepo Mwalimu mmoja wa nidhamu aitwa Mallya a.k.a LOBILO alikuwa mkali huyo kama nini,ukiingia kwenye anga zake tu umeumia...Pia kuna dada mmoja aitwa Farida alikuwa anatuuzia maandazi(Katizi) sijui yuko wapi sasa hivi.................... = Nakumbuka sana Mbege ya Corner bar(ipo karibu na Mto Umbwe) kila weekend tulikuwa tukienda hapo kupata kitimoto na Mbege(lol) = Bila kuusahau ule Wimbo wetu wa shule 'Mungu baba mwenyezi bariki shule yetu.......................Umbwe ni Mti safi wa Matunda bora,yanayojenga maisha(dah)............ = Pia nakumbuka vijiji vya jirani kama KWA RAPHAEL,KOMBO,MANGO,LYAMUNGO,KIBOSHO CENTRAL,LYAMUNGO,NARUMU,UMBURI,KINDI,MANUSHI n.k Naomba kuwasilisha wadau