Raphael Mtui
Senior Member
- Nov 26, 2024
- 134
- 293
Fikiri mfano huu: umeshika simu yako, ghafla tu unasikia imeita, kabla hata hujapokea inakatwa. Unaachana nayo. Hujabonyeza chochote.
Lakini!!
Simu yako ndio imeshadukuliwa hivyo!! Meseji zako zote za kawaida na za whatsapp, zinasomwa. E-mails zako zote zinasomwa! Simu zako zote zinasikilizwa! Kamera yako inapiga picha maeneo uliyopo na zinatumwa mahali. Maiki ya simu yako inarekodi sauti zote mahali ulipo na kutuma mahali. Taarifa za mahali halisi ulipo na unapoenda zinatumwa!
Kumbuka, hukubonyeza chochote. Huhitaji kutegeshewa link yenye maneno ya mvuto ili ubonyeze. Ile kupigiwa tu, tayari programu ya Pegasus iliingia na kujificha kwenye simu yako na hutaiona.
Hiyo ni hatari kubwa sana!
Pegasus si programu ya kawaida ya udukuzi; ni mfumo wa kijasusi wa kiwango cha kijeshi (military-grade spyware) ulioundwa ili kupenya simu janja (Android na iPhone) kwa siri na kugeuza kifaa hicho kuwa chombo cha ufuatiliaji wa saa 24.
Kampuni ya NSO Group ambayo ndiyo inamiliki programu hii, ilianzishwa mnamo mwaka 2010 huko Herzliya, Israel. Jina "NSO" ni kifupisho cha majina ya waasisi wake watatu.
Niv Karmi: Ofisa wa zamani wa kijasusi wa jeshi na shirika la Mossad (alijiondoa mapema baada ya kampuni kuanza).
Shalev Hulio: Mjasiriamali na meja mstaafu katika kitengo cha uokoaji cha jeshi la Israel.
Omri Lavie: Mjasiriamali na rafiki wa tangu utotoni wa Shalev.
Ingawa waasisi wake hawakutoka moja kwa moja Unit 8200 kama inavyodhaniwa mara nyingi, lakini kampuni hiyo imejaa mamia ya wahitimu wa Unit 8200, ambao wameajiriwa na wamekuwa injini kuu ya utafiti na uundaji wa programu hizi tata.
Tofauti na programu nyingine za udukuzi zinazohitaji mlengwa abonyeze kiungo (link) au apakue faili, Pegasus imepata umaarufu kwa teknolojia ya Zero-Click. Hapo ni hatari kabisa!
Fikiri, programu hii inaweza kuingia kwenye simu kupitia mwanya wa kiusalama (vulnerability) katika programu kama WhatsApp au iMessage. Mlengwa anaweza kupigiwa simu ya WhatsApp na asipokee, lakini simu hiyo tayari inatosha kupandikiza programu hiyo.
Mara ikiingia, Pegasus ina uwezo wa kusoma barua pepe, SMS, na jumbe zilizosimbwa (kama Signal au WhatsApp).
Pia, inaweza kufungua kamera na maikrofoni kwa siri ili kurekodi mazingira.
Kadhalika, Pegasus inaweza kufuatilia mahali mlengwa alipo (GPS) kwa wakati halisi.
Bila kusahau, programu hii inaweza kuchukua picha na nakala za mawasiliano yote.
Ingawa NSO Group ni kampuni ya watu binafsi, lakini inafanya kazi chini ya uangalizi mkali wa Wizara ya Ulinzi ya Israel.
Kila mauzo ya Pegasus kwa serikali ya kigeni lazima yapate leseni ya usafirishaji wa bidhaa za kijeshi kutoka serikalini.
Inakadiriwa kuwa katika miaka ya hivi karibuni (kama 2020), NSO Group imekuwa ikipata mapato ya takribani dola milioni 240 hadi milioni 250 kwa mwaka. (Milioni mia sita za Kitanzania).
Thamani ya Soko: Mnamo mwaka 2019, kampuni hiyo ilikadiriwa kuwa na thamani ya karibu dola bilioni 1.
Licha ya mafanikio yake, Pegasus imekuwa kitovu cha kashfa za kimataifa baada ya uchunguzi wa "Pegasus Project" (2021) kufichua kuwa serikali kadhaa zilitumia programu hiyo kufuatilia wanahabari, wanaharakati wa haki za binadamu, na viongozi wa nchi.
Hii ilisababisha Marekani kuiweka NSO Group kwenye "orodha nyeusi" (blacklist) mnamo Novemba 2021, hali iliyozitikisa fedha za kampuni hiyo na kupelekea kujiuzulu kwa baadhi ya viongozi wake.
Binafsi, niliumia sana nilipogundua kuwa yule mkosoaji maarufu wa Saudi Arabia Jamal Kashoggi aliuawa baada ya programu hii kutumika kumfuatilia!
Haya yalikuwa 'matumizi mabaya sana' ya programu hii.
Wengi mnakumbuka tukio hili maana lilitikisa vyombo vyote vya habari duniani kote kwa miezi kadhaa tangu alipouawa kwa sababu ni tukio lililofanyika ndani ya jengo la kidiplomasia na lilihusisha mbinu za kutisha za kijasusi na kikatili.
Tujikumbushe kidogo tukio hilo:
Jamal Khashoggi alikuwa mwandishi wa habari na mkosoaji mkubwa wa serikali ya Saudi Arabia. Aliuawa tarehe Oktoba 2, 2018, ndani ya ofisi za ubalozi mdogo wa Saudi Arabia mjini Istanbul, Uturuki.
Uchunguzi wa kitalamu uliofanywa na maabara ya Citizen Lab ya Chuo Kikuu cha Toronto, pamoja na Amnesty International ulibaini yafuatayo:
Kwanza, kulikuwa na Ufuatiliaji wa Watu wa Karibu: Simu ya mke wa Khashoggi, Hanan Elatr, ilidukuliwa na Pegasus miezi kadhaa kabla ya mauaji hayo. Pia, simu ya rafiki yake wa karibu, Omar Abdulaziz, ambaye alikuwa akifanya naye kazi ya kukosoa serikali mtandaoni, ilikutwa na programu hiyo.
Pili, kupitia udukuzi huo, inasemekana wauaji waliweza kujua mipango ya Khashoggi, mawasiliano yake binafsi, na mahali alipo, jambo lililorahisisha kumvizia na kumvuta kuingia ubalozini.
Wauaji walijua muda halisi atakaofika pale ofisini kuchukua vyeti vyake vya ndoa. Kikosi cha wauaji hao wakiwa 15 kilimdhibiti, wakamwua kwa kumnyonga kwa mfuko wa plastiki, kisha mwili wake kukatwa-katwa vipande, hadi leo mabaki ya mwili huo hayajapatikana.
Kuna hoja mbili kuu kuhusu nafasi ya Israel katika suala hili:
1. Uidhinishaji wa Leseni: Kama tulivyozungumza awali, NSO Group haiwezi kuuza Pegasus kwa nchi yoyote bila kibali cha Wizara ya Ulinzi ya Israel. Serikali ya Israel ilitoa leseni kwa Saudi Arabia kutumia teknolojia hii kama sehemu ya mkakati wa kuboresha uhusiano wa kidiplomasia na nchi za Kiarabu (kama sehemu ya kile kilichokuja kuwa Abraham Accords).
2. Diplomasia ya Siri: Ripoti za magazeti kama The New York Times zinaonesha kuwa hata wakati NSO Group ilipotaka kusitisha huduma kwa Saudi Arabia kutokana na matumizi mabaya, serikali ya Israel iliingilia kati na kuhimiza huduma hiyo iendelee kwa sababu za kimkakati.
Hapa inashangaza, na inaumiza! Programu ni mali yenu, ni ninyi mliitengeneza, mmeweka sheria za kuitumia, kuna 'mteja' kaitumia vibaya kuua mtu, unataka kumsitishia huduma, serikali inakuambia 'Kaa chini tulia, huyu ni besti yangu! Mwache aendelee kuitumia.' Mnabaki hamna la kufanya, programu yenu inaendelea kutumika kuua watu wa jinsi hiyo bila nyie kupenda!
Mauaji ya Khashoggi yalileta pigo kubwa kwa sifa ya NSO Group na kuleta shinikizo kwa Israel kurekebisha sheria zake za uuzaji wa silaha za kidijitali.
Marekani, licha ya kuwa rafiki mkuu wa Israeli, alisema 'sitaki huu upumbavu' kwa kuiweka kampuni hiyo kwenye orodha ya blacklist kwa kuwa teknolojia hiyo inatumika kukandamiza haki za binadamu na demokrasia.
Kuna yule mwandishi wa Mexico ambaye anaitwa Cecilio Pineda Birto ambaye naye aliuawa baada ya serikali ya Mexico kununua programu hii na kuitumia kumfuatilia.
Cecilio alikuwa alimebobea katika kuripoti habari za uhalifu, rushwa, na ushirikiano wa siri kati ya magenge ya madawa ya kulevya na maafisa wa serikali.
Aliuawa akiwa 'Car Wash' akisubiri gari lake lioshwe. Alimiminiwa risasi kumi kifuani na kufariki papo hapo. Ule uchunguzi wa Pegasus Project 2021 ulibaini ukweli wa kuogofya jinsi simu yake ilivyokuwa imefuatiliwa na programu hii hatari.
Cecilio aliuawa tarehe 2 March 2017 muda mfupi baada ya kuruka 'live' Facebook akifunua maovu ya serikali yake.
HUENDA UNGETAMANI KUSIKIA WAKUU WA NCHI WALIOWAHI KUDUKULIWA NA PROGRAMU HII:
Ngoja nikueleze:
Uchunguzi wa kimataifa wa "Pegasus Project" 2021 ulifichua orodha ya namba za simu zaidi ya 50,000 ambazo zililengwa na wateja wa NSO Group!
Katika orodha hiyo, namba za simu za viongozi wa nchi, mawaziri wakuu, na wafalme zilikuwepo!
Hapa ninakupa baadhi tu ya wakuu wa nchi na viongozi mashuhuri ambao simu zao zilikuwa kwenye orodha ya walengwa wa udukuzi huo:
1. Emmanuel Macron (Rais wa Ufaransa).
Namba ya simu ya Rais Macron ilionekana kwenye orodha ya walengwa mwaka 2017. Serikali ya Morocco ndiyo ilikuwa imenunua programu hii na kuitumia kumfuatilia rais wa Ufaransa! Hali hii ilisababisha mzozo mkubwa wa kidiplomasia kati ya Ufaransa na Morocco, na Macron akalazimika kubadili simu yake na namba yake ya siri mara moja. Kumbuka, hizi nchi zilikuwa marafiki wakubwa!
2. Cyril Ramaphosa (Rais wa Afrika Kusini).
Rais Ramaphosa naye alitajwa kama mmoja wa viongozi waliolengwa. Serikali ya Rwanda ndiyo inasemwa ilinunua programu hii na kuitumia kumfuatilia Ramaphosa.
3. Barham Salih (Rais wa zamani wa Iraq).
Alikuwa mmoja wa viongozi wa kwanza wa nchi za Kiarabu kugundulika kuwa kwenye orodha ya walengwa. Hii ilionyesha jinsi Pegasus ilivyotumika katika maeneo yenye migogoro ya kisiasa Mashariki ya Kati kufuatilia mienendo ya viongozi wa juu.
4. Imran Khan (Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan).
Inasemekana serikali ya India (ambayo ni hasimu mkuu wa Pakistan) ilitumia Pegasus kujaribu kudukua simu ya Imran Khan wakati akiwa madarakani. Huu ni mfano wa jinsi teknolojia hii inavyoweza kutumika kama silaha ya ujasusi wa kimataifa (state-on-state espionage).
5. Mfalme Mohammed VI (Morocco).
Cha kustaajabisha ni kwamba, hata mfalme wa Morocco mwenyewe alionekana kwenye orodha ya namba zilizolengwa na vyombo vya usalama vya nchi yake mwenyewe. Hii inaashiria kuwa mara nyingine mifumo hii ya ujasusi hutumika kufuatilia hata watu wa ndani ya utawala ili kuhakikisha utii.
Viongozi wengine waliolengwa ni pamoja na:
Saad Eddine El Othmani: Waziri Mkuu wa zamani wa Morocco.
Mostafa Madbouly: Waziri Mkuu wa Misri.
Charles Michel: Rais wa Baraza la Ulaya (wakati huo akiwa Waziri Mkuu wa Ubelgiji).
Udukuzi wa viongozi wa nchi ni hatari kwa sababu programu hii inaweza kupata nyaraka za siri za kijeshi na mikataba ya kiuchumi.
Lakini kuna ile athari mbaya zaidi iitwayo 'Vitisho (Blackmail). Taarifa binafsi na picha zinaweza kutumika kuwashinikiza viongozi kufanya maamuzi fulani.
Mfano, rais wa nchi fulani anayefuatiliwa, akakutwa ana simu na meseji kwa mahawara wake, au picha zake za utupu zikanaswa, hivyo zikatumika kumtishia afanye maamuzi fulani ili mambo yake yasivujishwe. Kwa kuogopa kudhalilishwa pamoja na hatua kali dhidi yake, atakubali kufanya kila anachoambiwa na waliomdukua.
Lakini pia katika Diplomasia; Inaharibu uaminifu kati ya nchi marafiki (kama ilivyotokea kwa Ufaransa na Morocco).
Serikali ya Israel ilijitetea kuwa Pegasus inauzwa tu kwa ajili ya kupambana na ugaidi na uhalifu mkubwa, lakini orodha hii ya viongozi ilithibitisha kuwa mara nyingi ilitumika kwa malengo ya kisiasa.