Tujikumbushe Kuvunjika kwa Mchakato wa Katiba Mpya

Umkonto

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
2,102
3,614
Hii ni kwa wale vijana waliokuwa wadogo, nao ni vyema wangepata ABC za kuvunjika kwa mchakato wa katiba mpya mwaka 2014.

Ieleweke pia, mswaada wa katiba mpya uliishandikwa na wajumbe wakiongozwa na Mh Chenge (Huyu ndiye alikuwa mwenyekiti wa uandishi wa mswaada katiba) baada ya kufanya mabadiliko kutoka mapendekezo ya tume ya katiba. Hii inaonesha kuwa, hata wana CCM walikuwa tayari kupata katiba mpya.

Angalizo: Kama nitakuwa nimekosea historia vizuri, mtanisahihisha kwa sababu, kipindi hicho nilikuwa mwanafunzi ila nilikuwa nafuatilia mambo kupitia vyombo vya habari.

Mambo yalivyokuwa;

Mambo yalienda vizuri sana katika tume ya katiba iliyoongozwa na jaji Warioba, ambapo tume ilikusanya maoni nchi nzima.

Baadae, mapendekezo ya tume taliwasilishwa katika bunge la katiba, ambalo nakumbuka ilitangazwa kuwa lilikuwa na wajumbe kama 600 kutoka makundi mbalimbali, wakiwemo wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Speaker wa Bunge alikuwa ni Pandu Ameir Kificho kutoka Zanzibar.

Wajumbe, walianza kujadili vipengele katika mapendekezo ya tume, kimoja baada ya kingine na kufanya marekebisho kama ilionekana inafaa.

Nakumbuka, miongoni vya vipengele ambavyo vilisababisha ubishi ni MUUNDO WA SERIKALI na TUNU ZA TAIFA, ila hasa muundo wa serikali.

Mapendekezo ya tume yalikuwa ni uwepo wa SERIKALI TATU (Serikali ya Muungano, Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Tanganyika).

Wajumbe kutoka vyama vya upinzani (Ambao waliunda umoja wao "UKAWA) waliunga mkono hoja ya kuwa na serikali tatu, wakati wajumbe wengine wakiongozwa na CCM walitaka kuwa na SERIKALI MBILI.

Maamuzi ya kupitisha vifungu baada ya majadiliano yalikuwa ni kwa njia ya kura. Baada ya UKAWA (CHADEMA, CUF, NCCR MAGEUZI, NLD) kuona kwamba, wajumbe wengi ni CCM basi UKAWA wakaamua kususia bunge la katiba kwa sababu wangeshindwa kwa kura za wazi.

Wajumbe waliobaki waliendelea na majadiliano. Mwisho, Mh Chenge ndiye alikuwa mwenyekiti wa uandishi wa katiba, ambapo mswaada wa katiba uliandikwa usiku na mchana, na kusubiri hatua zingine.

Kwa hiyo ieleweke, mswaada wa katiba mpya upo unasubiri hatua zingine. Mswaada huo uliandikwa na wajumbe waliobaki ndani ya bunge, UKAWA walitoka nje.

Kwa hiyo, hata leo tukisema tuanze mchakato wa katiba mpya, basi ni kazi rahisi sana kwa sababu tunapo pa kuanzia. Yaani ni marekebisho machache sana yatafanyika katika mapendekezo ya tume ya jaji Warioba, hivyo haitakuwa kazi ngumu sana kama ambavyo watu wanafikiri. Kwa mfano, tukaacha serikali mbili halafu tukayabeba mengine ya tume, kwani kuna ubaya gani?
 
mimi nasubiri wajumbe watakoelezea kwa ufasaha tukio la paul makonda(sikumbuki wakati huo alikuwa na cheo gani) kumvamia mzee warioba pale ukumbini ubungo plaza siku ya mdahalo wa kujadili katiba mpya.

nilishuhudia hili tukio kupitia television. nataka nifahamu, alitumwa na nani?, alifanya kwa utashi wake?,ili kumfurahisha nani?, lengo lilikuwa nini?.
 
Back
Top Bottom