Tujikumbushe Kauli za CHADEMA Kwa Lowassa

Tujikumbushe Kauli za CHADEMA Kwa Lowassa

View attachment 1039966

Lowassa akiwa CCM Kabla ya Kuhamia CHADEMA

1.Nashangaa wanachoma moto vibaka wanamuacha Lowassa anatanua Mitaani-Freeman Mbowe
2.Nina Ushahidi wa kutosha kuhusiana na wizi na ufisadi wa Lowassa na Rostam-John Mnyika
3.Ni heshima kwa Mungu kumzomea na kumtukana mtu fisadi kama Lowassa-Godbless Lema
4.Anayemuunga mkono Lowassa akapimwe akili haraka sana-Peter Msigwa
5.CCM wamempatia fisadi Lowassa fomu ya kugombea Urais, ni hatari sana-Tundu Lissu


LOWASSSA akiwa CHADEMA
1.Mimi ninayejua kiu ya Watanzania nitakuwa mwendawazimu kama eti tutaacha kumpokea Edward Lowassa , Kiongozi mwenye nafasi kubwa katika Taifa hili, Kiongozi ambaye ana wafuasi wengi katika nchi hii,-Freeman Mbowe


2. Wakati tunakwenda kwenye uchaguzi Mkuu Mwaka 2015 tulikuwa tumejipanga kwelikweli, tulitafuta Wataalam watwambie tunashindaje Uchaguzi, wakatwambia , katika 'Political Personalities' zote za Tanzania Lowassa peke yake anatembea na wapiga kura 18%-Tundu Lissu

3.Tusifike mahali Lowassa akaonekana ndiye mzaaaaaambi kuliko watu wote hapa Tanzania, hiyo hatumtendei haki-Peter Msigwa

Baada ya Lowassa Kurudi CCM

1.Tulimkaribisha na kumpatia majukumu ya kutuongoza kenye mapambano ya Mwaka 2015 na alitekeleza majukumu hayo vizuri kwa kadiri alivyoweza-Tundu Lissu

2.Kama kuna kazi ya maana Lowassa amefanyia CHADEMA ni kuhamia CCM-Peter Msigwa
3. Kuondoka kwa Lowassa kunatupa nafasi CHADEMA kutafakari uamuzi wa kuwapokea wanasiasa kutoka vyama vingine wakati wa uchaguzi-Freeman Mbowe


Tafakuri: Hapana shaka kwamba Lowassa amewafanya CHADEMA wasijiamini na kubaki kutapatapa. Siyo mara ya kwanza CHADEMA kusema hawatapokea wanaohama CCM, Kabla Lowassa hajahamia CHADEMA, Mbowe alisema na nanukuu: "Hatupokei tena Makapi kutoka CCM" leo anasema kuondoka kwa Lowassa kunawapa nafasi ya kujitafakari, huko ni kutapata kwa kiwango cha juu kabisa. Hapana ubishi kwamba CHADEMA bado walikuwa wanamhitaji Lowassa kuliko Lowassa alivyokuwa anawahitaji.

Kwa upande mwingine ujio wa Lowassa CCM hauna faida au hasara yoyote kwa CCM zaidi ya kutunza heshima yake kwa jamii. Kifupi Lowassa anaihitaji sana CCM kuliko CCM wanavyomhitaji,


Tuletee na zile kauli za upande mwingine baada ya ENL kuhamia chadema.
 
Siasa ni ujanja , Lowassa kawamaliza CHADEMA kirahisi sana

Siku nyingine tumia akili japo kwa uchache, nani kakuambia chadema wamemalizika? ameachwa ameenda kwa heshima, hakuna aliyemtukana kama ambavyo walimtukana wao alivyowaacha, na hiyo ni busara katika chadema, hakuna vijana wakosa adabu kutukana wazee wetu........ nakukumbusha tu kuwa alikuwa mgombea na kura zilionekana, bila shaka angekuwa kiongozi wa nchi kama haki ingetendeka, sasa jiulize alienda kwa lengo la kuwamaliza chadema au alitaka uongozi wa nchi kupitia chadema?
 
[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122] CCM na CDM ni kama mke na mme ndani wakigombana we kalale tu ugonvi huishia kitandani tuuu, ukitetea mmoja kesho asubui utaonekana kama vile kituko


shabikia timu ila sio mchezaji, akihamia timu pinzani sajiri mwingine mkali
 
Baadhi ya Watanzania wanafanywa shamba la bibi hata na wanasiasa uchwara.
Ni aibu watu wazima kuruhusu wanasiasa kuchezea akili zao namna hii.
 
Back
Top Bottom