Tujikumbushe historia ya kundi la THE BEATLES

Tujikumbushe historia ya kundi la THE BEATLES

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,746
Reaction score
25,672
1535201097324.jpeg
544 × 700 - rockhall.com
Hakuna kundi la muziki litakalopata jina kama lilivyokuwa The Beatles lililokuwa likiundwa na wanamuziki wanne, John Lennon, Paul McCartney, George Harrison na Ringo Starr.

Walikuwa vijana wadogo, Waingereza wanaojua kuimba kupita kawaida katika miaka ya 1960. Umri wao ulikuwa ni miaka 18 mpaka 22 lakini walikuwa balaa.

Wao ndiyo waliolipaisha sana jiji la Liverpool. Waliopendwa duniani, safari yao ya kwanza kwenda Marekani walikamatwa na bangi vyumbani, watu wakaandamana waachwe ili wapige shoo.

Walipata pesa nyingi sana katika umri mdogo, walifanya chochote walichokitaka. Katika nyimbo 100 bora katika chati ya Billboard, nyimbo tano za juu, zote zilikuwa nyimbo zao.

The Beatles walikuwa wasafi, wanajua kuvaa, ukimsikia mtu akimwambia mwenzake wewe Bitozi basi jua hilo jina lilianzia kwao kutokana na usmarti mkubwa waliokuwa nao.

Ila John Lennon alipoanza uhusiano na msichana wa Kijapan, Yoko Ono, mambo yakaharibika na baadaye kundi kufa kabisa. Mpaka sasa hivi, ni watu wawili tu ndiyo waliobaki hai ambao ni Paul McCartney na Ringo Starr. John Lennon aliuawa baada ya kusema kwamba kundi lao lilikuwa maarufu zaidi ya Yesu na George Harrison alikufa kwa ugonjwa wa kansa ya koo na mapafu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom