Pure_sapiens
JF-Expert Member
- Dec 25, 2016
- 2,202
- 2,035
Habari zenu wana JF, Natumaini nyote ni wazima wa afya na walio na matatizo tuzidi kuwaombea Mungu atie nusra yake.
Nadhani wote tunafahamu kinachoendelea sasa katika nchi yetu si kingine bali ni swala la mchanga wa madini. Kuna baadhi ya watanzania wanaunga mkono kampuni ya ACACIA na wengine wanamuunga mkono Mh Rais. Kabla hatujaangalia upande gani wa kulaumiwa hebu tujaribu kusoma historia ya ukombozi wa Tanganyika.
MALENGO YA KUJA KWA WAKOLONI~
1. Kutafuta malighafi kwa ajili ya viwanda vyao huko Ulaya.
2. Kutafuta masoko ya kuuzia bidhaa zilizozalishwa na viwanda vyao huko Ulaya.
3. Ardhi yenye rutuba kwa ajili ya kilimo cha mazao ya biashara.
4. Vibarua wa gharama ndoto ili waweze kuzalisha malighafi.
Haya ni baadhi ya malengo ya kuja wakoloni katika bara la Afrika. Nchi nyingi za Afrika zimepata uhuru, je Mataifa ya Ulaya bado wana malengo haya?
MAPAMBANO DHIDI YA WAVAMIZI KUTOKA ULAYA.
Baada ya kuingia kwa wakoloni katika nchi yetu wazee wetu walipigana sana ili kuwaondoa wakoloni. Haya ni baadhi ya madhumuni ya kupinga uvamizi wa wakoloni.
1.Nia ya kuendelea kujitawala na kulinda heshima yao.
2. Kupinga Sera za kinyonyaji za wakoloni.
3. Kupinga kunyang'anywa ardhi yao.
4. Kutetea biashara zao.
5. Kunyang'anywa rasimali zao.
Babu zetu walitumia mbinu mbalimbali ili kupinga ukoloni licha ya kuwa walikuwa na silaha duni lakini walijitoa kwa moyo mmoja kuingia vitani na wakoloni. Kumbuka wakoloni kwa kipindi hiko walikuwa tayari wana silaha za kisasa kama bunduki, mizinga huku akina sisi tuna mapanga, mikuki, mishale na mawe.
HAWA NI BAADHI YA VIONGOZI WA JADI/MACHIFU WALIPIGANA VITA NA WAKOLONI~
Machifu kutoka maeneo mbalimbali waliongoza mapambano dhidi ya wakoloni kwa lengo ya kuendelea kujitawala. Licha ya kuwa na silaha duni.
(1) Maeneo ya Pwani na Bahari ya Hindi; Maeneo ya Kilwa, Bagamoyo, Dar es Salaam na Pangani wakiongozwa na Abushiri bin Salim na Bwana Heri na Hassani bin Omari Makunganya walipigana vita dhidi ya Wajerumani. Wajerumani walishinda vita hivyo na kumkamata na kumnyonga Abushiri mnamo 15/12/1889 Pangani. Hassani bin Omari Makunganya aliongoza watu wake kupigana dhidi ya Wajerumani kuanzia mwaka1894-1895. Makunganya alishindwa vita na kutoroka November 1895 baadae alikamatwa na kunyongwa huko Kilwa Kivinje mahali palipoitwa"Mwembe Kinyonga"mwaka 1896.
(2)Wahehe; Wakiongozwa na Mtwa Mkwawa walipigana dhidi ya Wajerumani kuanzia mwaka 1891-1898. Mkwawa alikuwa na jeshi imara hivyo alifanikiwa kuwashinda Wajerumani na kumuua kamanda Emil Von Zelewisky. Wajerumani walijipanga na kuanzisha tena vita hivyo Mkwawa alishindwa na mwaka 1898 alipiga risasi na kufa ili asishikwe mateka.
(3)Wanyamwezi; chini ya Mtemi Isike wa Tabora walipigana na Wajerumani kuanzia mwaka 1886-1893
(4)Wamatumbi; chini ya uongozi wa Kinjeketile Ngwale wakishirikiana na baadhi ya makabila kama Wangoni, Wasangu, Wamakonde, Wangindo, Wabena, Wapogoro na Wambungu walipigana vita dhidi ya Wajerumani kuanzia mwaka19o5-19o7 vita hivyo viliitwa vita vya majimaji. Haya ni baadhi ya Machifu na makabila waliopigana vita dhidi ya wakoloni kwa njia ya vita, baadhi ya viongozi walinyongwa kinyama na wengine walijiua ili wasikamatwe na wakoloni.
Historia hii lazima tujikumbushe ili tuweze kuwa wazalendo kwa ajili ya Nchi yetu kwa vizazi vijavyo kama walivyofanya wazee wetu. Mzungu ni mzungu tu alikuja kama mkoloni lakini Leo anakuja kama mwekezaji. Watanzania wa Leo tunaogopa kwa kuwa mh Rais kazuia makontena ya mchanga wa dhahabu, je tungekuwa enzi za harakati za ukombozi tungeweza kutoka kifua mbele na kupigana vita dhidi ya wakoloni? Mgogoro kati ya Marekani na North Korea nilitegemea ungekuwa kama mwalimu wetu mzuri, tunafahamu nk. ni nchi masikini lakini walisimamia maamuzi yao licha ya Marekani kutaka kuishambulia. Je tungekuwa sisi ndo nk. Tungeweza kusimamia maamuzi yetu? kupitia historia hii tunapata mafunzo gani.
Karibuni kwa majadiliano yenye uzalendo na tija kwa Taifa letu.