Tujikumbushe FikraPevu ilisema kuhusu sekretarieti

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,812
1,250
Chama cha Mapinduzi (CCM) kinatarajia kufanya mabadiliko makubwa katika uongozi wake wa juu, ikiwa ni pamoja na kubadilisha baadhi ya viongozi wake wa juu ikiwamo wajumbe wa Kamati Kuu (CC) yake,*Fikra Pevu*imejulishwa.Taarifa za ndani ya CCM zinaeleza kwamba, Mwenyekiti wa CCM, Taifa Rais Jakaya Kikwete, anatarajiwa kuwasilisha mapendekezo yake katika kikao cha Kamati Kuu ambacho kimeanza mchana huu mjini Dodoma.“Mwenyekiti atatoa taarifa kwa wajumbe wa CC mchana huu, kabla ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kitakachoanza Jumatatu. Tutarajie mabadiliko makubwa ndani ya CCM maana ameona akichelewa madhara yatakuwa makubwa zaidi,” anasema kiongozi wa CCM aliyeko Dodoma.Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya M. KikweteMiongoni mwa nafasi ambazo zinatarajiwa kufanyiwa mabadiliko ni nafasi ya January Makamba, ambaye ni Katibu wa NEC Siasa na Mambo ya Nje, ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.Katika mabadiliko ya hivi karibuni, viongozi wa serikali hawapaswi kuwa viongozi wa Kamati Kuu, jambo ambalo liliwagharimu aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, George Mkuchika na aliyekuwa Katibu wa NEC Siasa na Mambo ya Nje, Bernard Membe.Nafasi nyingine inayotarajiwa kubadilishwa ni ile ya Itikadi na Uenezi inayoongozwa na Nape Nnauye, ambaye anatajwa kukabidhiwa madaraka makubwa zaidi na anatajwa mmoja wa viongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) kuchukua nafasi yake.Katika mabadiliko hayo, inaelezwa kwamba kuna maandalizi ya kumrudisha katika siasa aliyekua Katibu Mkuu wa CCM, Philip Mangula, ambaye anatarajiwa kurudi katika nafasi nyingine badala ya ile ya Katibu Mkuu.Imeelezwa kwamba, Kikwete anatarajiwa kuweka msimamo kuhusiana na hali ya kisiasa inayoendelea sasa ambako tayari Erward Lowassa, mtu aliyejigamba kuwa swahiba wake ambaye “hawakukutana barabarani” amejitokeza hadharani kukishambulia chama chake, huku akitajwa kuwa nyuma ya hujuma kubwa dhidi ya CCM.Lowassa ambaye alitajwa kuwa mmoja wa watu wanaotakiwa kujivua gamba, amekua akipambana kujinasua na hivi karibuni watu kadhaa walio karibu naye, wamejiondoa CCM na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).Pamoja na mabadiliko na mambo kadhaa kutajwa kujadiliwa Dodoma, Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM, Nape Nnauye, alisema kupitia blogu ya CCM kwamba chama hicho kinatarajia kujadili matatizo yanayowagusa wananchi na kuyatolea misimamo na ushauri wa hatua za kuchukua kuyatatua na kuyakabili.Katika taarifa hiyo Nape amesema* CCM itajadili mambo mbalimbali ikiwemo ughali wa bei za vyakula na kero mbalimbali zinazogusa wananchi.“Kwa muda mrefu wananchi wamekuwa wakilalamika hali ngumu ya maisha na kupanda kwa bei ya vyakula, hivyo NEC itapata taarifa ya serikali kuona hali ikoje na kuangalia nini kifanyike kupunguza au kuondokana kabisa na hali hiyo”, alisema Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi.Nape alisema ajenda nyingine katika kikao cha NEC ni mchakato wa katiba mpya akisema ni lazima chama nacho kijadili ili kuona mapendekezo na mawazo ya Chama kuhusu mchakato huo.Alisema pia CCM inatarajia kujaza nafasi zilizo wazi za makatibu wa mikoa na wilaya kwa kuwa kuna maeneo yamebaki wazi kutokana na watendaji wake kuteuliwa kuwa wakuu wa wilaya katika uteuzi uliofanywa hivi majuzi na Rais Kikwete.Categories:*Featured,*Siasahttp://www.fikrapevu.com/habari/mabadiliko-makubwa-yaja-ccm-january-kupata-mrithi
 
Top Bottom