aka2030
JF-Expert Member
- Jan 5, 2013
- 2,650
- 3,662
Hili ni moja ya kundi la muziki ambalo halipewi heshima inayostahili. Kundi hili lililoanza katikati ya miaka ya tisini likiundwa na wasanii 3 drezzy chief, computer na clonic fingure.
Hawa,jamaa walikuwa na uwezo wa kurap kuimba rnb pamoja na dancehall. Ni kundi la kwanza kabisa kumiliki mtandao uliojulikana kama bdpkamili.8m.com pamoja na mavazi yao ya bdp gear ambapo hapo gangwe mob wakadesa
Hawa jamaa walifanikiwa kutoa album 2. Album ya kwanza iliitwa "wosia" Ikiwa na hit song rudi mpenzi na zingne kama kitambo kidogo, unakosea, bahati yamwenzio, manjumati, wosia, huku nyimbo zote ukiwa ni mkono wa mika mwamba.
Jamaa, walifanikiwa kutoa album ya pili mwaka 2005 ilioitwa "BDP KAMILI" ikiwa na nyimbo kama majobless, kumwimbia, kichwa cha chief, maimuna, zote mpishi akiwa enrico wa soundcrafter
Baada ya hapo jamaa kimya mpaka leo ladha yao hakika tunaimiss kwenye game