PreGE2025 Tujikumbushe ahadi 10 za wana CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Dr Adam Francis

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
464
Reaction score
687
Tujikumbushe kidogo ahadi 10 za wana CCM kwa chama chao. Zamani za Mwl. Nyerere kabla ya kupata kadi, wana CCM walitakiwa kuhitimu kwanza darasa la itikadi ya Ujamaa na Kujitegemea. Siku ya kukabidhiwa kadi, ilihitimishwa kwa tamko la mwanachama mpya kuunga mkono ahadi 10 za mwana CCM. Hapa chini, ndizo ahadi zenyewe.

1. Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja.

2. Nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote

3. Nitajitolea nafsi yangu kuondoa umaskini, ujinga, magonjwa na dhuluma.

4. Rushwa ni adui wa haki. Sitapokea wala kutoa rushwa.

5. Cheo ni dhamana. Sitakitumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu.

6. Nitajielimisha kwa kadiri ya uwezo wangu na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote.

7. Nitashirikiana na wenzangu wote kuijenga nchi yetu.

8. Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.

9. Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa CCM na raia mwema wa Tanzania na Afrika.

10. Nitakuwa mtiifu na mwaminifu kwa Rais wa Serikali ya Tanzania
 
Kweli hiyo ilikua zamani kabla anasa za dunia hazijatufikia, kwa sasa watu wanatumia vyeo vyao kwa manufaa binafsi.

Kwa sasa kila mtu anaejua kusoma na kuandika anataka awe mwana siasa, ikiwezekana apate na ubunge, maana bungeni ni kijiwe cha kupeana conection za kugawana mali za umma.
 
Tujikumbushe kidogo ahadi 10 za wana CCM kwa chama chao. Zamani za Mwl. Nyerere kabla ya kupata kadi, wana CCM walitakiwa kuhitimu kwanza darasa la itikadi ya Ujamaa na Kujitegemea. Siku ya kukabidhiwa kadi, ilihitimishwa kwa tamko la mwanachama mpya kuunga mkono ahadi 10 za mwana CCM. Hapa chini, ndizo ahadi zenyewe.

1. Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja.

2. Nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote

3. Nitajitolea nafsi yangu kuondoa umaskini, ujinga, magonjwa na dhuluma.

4. Rushwa ni adui wa haki. Sitapokea wala kutoa rushwa.

5. Cheo ni dhamana. Sitakitumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu.

6. Nitajielimisha kwa kadiri ya uwezo wangu na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote.

7. Nitashirikiana na wenzangu wote kuijenga nchi yetu.

8. Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.

9. Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa CCM na raia mwema wa Tanzania na Afrika.

10. Nitakuwa mtiifu na mwaminifu kwa Rais wa Serikali ya Tanzania
Dogo hizi zilikuwa ahadi za Mwana TANU. Kipindi hicho tukiimba,
"Ndugu sikilizeni, ahadi kumi za Mwana TANU,
Ahadi ya kwanza....................,
Ahadi ya pili................................,
Ahadi ya tatu.............................,
Ahadi ya nne...............................,
Ahadi ya tano.............................,
Ahadi ya sita..................................,
Ahadi ya saba...............................,
Ahadi ya nane...............................,
Ahadi ya tisa...................................,
Ahadi ya kumi...............................,

Ilikiuwa raha sana!
 
Back
Top Bottom