Tujihadhari na virusi vya computer haswa ukiwa upo kwenye email unatumia internet online

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,331
33,141
Computer-virus.jpg


Virus kwa ufupi

Ni program kama program nyingine za komputa. Tunaposema program ya komputa

inamaanisha kwamba mtaalamu wa kuandika program ametumia ujuzi wake kuandika program

inayoweza kutumika kwenye komputa kama vile Microsoft Word n.k. Hata hivyo hii si program

ya kawaida. Nia na madhumuni yake huwa si mazuri na madhara yake yanaweza kuwa

makubwa. Kwa mfano komputa yangu ilipoingiliwa na virusi wakati nafanya project ya mwisho

ya degree, nilipoteza kazi yangu siku mbili kabla ya kukabidhi baada ya virus kuingilia

komputa yangu. Kwa bahati nilikuwa nimeweka back up kwenye flash memory. Hata hivyo back

up haikuwa up-to-date hivyo ilinichukua masaa zaidi ya ishirini na tano kuongeza yale

niliyopoteza. Masaa haya yangeweza kutumika kwenye kuiboresha project sio kufanya upya vitu ambavyo nilishavifanya.

Kwa kifupi virus ni kipande kidogo cha software program kinachojishikilia kwa siri kwenye

program za kweli tunazotumia kila siku. Kwa mfano kama unatumia Microsoft Excel (Spreadsheet) hako kamdudu kanaweza kuwa kamejibanza kwenye hii program. Kila unapoifungua Spreadsheet unajikuta umefungua hicho kiprogram bila kujua.

Virusi vya komputa vinafanya kazi vipi?




Email Viruses- Watu wengi hivi karibuni wamekuwa wakipata virusi vya kwenye email (e-mail viruses). Email virus anajificha kwenye email na kusafiri nayo kama attachment kwenye message. Virus huyu ana uwezo wa kujiongeza

(raplicates itself) hivyo anaweza kujituma mwenyewe kwa kutumia email yako kwenda kwa watu wote walio kwenye

contact zako. Hata hivyo virus huyu hawezi kufanya kazi mpaka ufungue attachment au link iliyoificha. Hivyo kama

umepokea email yenye virus, bado hawezi kufanya chochote mpaka utakapofungua attachment au link iliyomficha.

Kwa sababu hiyo kuanzia leo USIFUNGUE email attachment au links kama huna uhakika. Mtumie email rafiki

aliyekutumia uhakikishe kama ni yeye aliyetuma.


Email+Virus.jpg



Trojan Horses– Hawa ni pia ni komputa program. Program inajifanya kuwa program ya kawaida ila unapoifungua tu inaingia na kujificha kwenye hard disk ya komputa yako. Ana tabia ya kufuta kila kitu kilichopo kwenye hard disk na hata kuharibu operating system hivyo kuiua komputa yako kabisa. Tofauti nyingine kati ya email virus na huyu Trojan ni kwamba Trojan hawezi kujiongeza (can not replicate itself).

horse+trojan+virus+REMOVED.jpeg

Worms– Hawa wana tabia ya kutumia komputa network kujiongeza na kutafuta komputa ya mtu siyo na vikingaji (antvirus program) ili waingie.
computer-virus-rmoval.png


Kwa nini watu wanateneza virus?

Unaweza kujiuliza ni kwa nini watu wanatengeneza virus! Ukweli ni kwamba kuna sababu kama mbili:


  • Uharibifu - Kuna watu wanpenda kuharibu na kuona wengine wanahangaika kutafuta solution kwa kitu ambacho amekifanya yeye
  • Sifa ya kuvumbua - Kila mtu anapenda kuwa kama Isaac Newton. Kuacha historia kwamba waliweza kuitingisha dunia na kufanya kitu ambacho weni hawajakifanya.

Jinsi ya kujikinga na virus

Kuna njia kadhaa:
1. Kama una hofu kubwa sana ya virus basi tumia operating system yenye kinga zaidi kama UNIX. Ni vigumu sana kusikia virus wameingilia operating system ya UNIX kwa sababu ya kinga mbali mbali zilizotengenezewa ndani.

2. Kama unatumia operating system nyingine yeyote basi hakikisha unaweka vikinga (ant-virus - virus protection software). Unaweza kupata kopi yabure hapa.

3. Usiamini program nyingi unazozipata kwenye internet, nyingi zina virus isipokuwa program unazopata kutoka kwa watengenezaji wenyewe wanofahamika. Wakati mwingine nunua program iliyo kwenye CD kuliko kuchukua (download) moja kwa moja.

4. Usifungue email attachment bila kuwa na uhakika.

5. Hakikisha umeruhusu (enable) Macro Virus Protection(angalia maelezo hapo chini) kwa wanaotumia Microsoft applications. Pia usiruhusu macros unapofungua document. Macro hazihitajiki kwenye document hivyo ukipokea document yenye macro jiulize ni kwa nini kabla hujaruhusu.

Jinsi ya kujikinga na Macros unapotumia Microsoft Word (maelezo haya ni kwa version mpya za Microsoft Office)
i. Go to ‘File'








ii. Click Options







iii. Click Trust Center


iv. Click Trust Center settings








v. Click Macros

vi. Set the settings as shown



 
Thanks mzizimkavu kwa maelezo haya mazuri. Tunashukuru pia kwa hii antivirus (avast) japo kwa virus vya bongo, kuwa na avast ni sawa na kutokuwa na antivirus.
 
Thanks mzizimkavu kwa maelezo haya mazuri. Tunashukuru pia kwa hii antivirus (avast) japo kwa virus vya bongo, kuwa na avast ni sawa na kutokuwa na antivirus.

kwa kwel mkuu unaposema "avast n sawa na kutokua na Antivirus," unakosea maana avast wanajtahid sana ktk ku protect pc
tena ukiwa na avast Internet securit 8.
Saf sana hyo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom