Tujifunze nini kupitia Dominance ya Hispania katika Soka Ulaya?

gpluse

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
636
831
Mimi ni mpenzi wa mpira wa miguu nikiungana na mamilioni ya watu wengine duniani. Mchezo huu kama mnavyojua unavutia wengi sana na kwa sasa ni industry inyoajiri na kulipa vizuri sana. Wengi sasa tungependa na tunatamani hata watoto, ndugu au hata watanzania wenzetu wapate nafasi na kunesha vipaji vyao katika vilabu vikubwa duniani. Mimi ni mpenzi sana wa mpira wa Hispania.

Nafahamu kuwa watanzania wengi hasa vijana ni wapenzi wa vilabu vikubwa vya Uingereza. Upenzi huu umetokana hasa na nchi hiyo kutangaza zaidi mpira wao. Hilo limewafanya wengi kuaminishwa kuwa mpira wa Uingereza ni bora zaidi kuliko kwingineko duniani. Kumekuwa na mijadala wakati flani kuhusu ligi ipi ni bora duniani. Wengi walioaminishwa kupitia propaganda ya vyombo vya habari vya Uingereza watakwambia ni ligi ya England ndo bora.

Naomba kidog tutizame rekodi hizi.

UEFA Champions League
2015-16 Real Madrid/Atletico Madrid Spain
2014-15 Barcelona Spain
2013-14 Real Madrid Spain
2012-13 Bayern Munich Germany
2011-12 Chelsea England
2010-11 Barcelona Spain
2009-10 Internazionale Italy
2008-09 Barcelona Spain
2007-08 Manchester United England
2006-07 Liverpool England
2005-06 Barcelona Spain

Tukumbuke pia kuwa katika kipindi cha 2005-2006 mpaka sasa, timu za Spain pekee fainali mara sita, yaani 6/11. Na tukumbuke kuwa katika kipindi hicho, timu za Spain pekee zimeingia fainali mara mbili. Hakuna nchi nyingine imefanya hivyo katika kipindi hicho. Aidha, katika kipindi hicho, Spain imeingiza timu zake zaidi ya moja kwenye nusu fainali

Europa League
2005–06
23px-Flag_of_Spain.svg.png
Spain Sevilla
2006–07
23px-Flag_of_Spain.svg.png
Spain Sevilla
2007–08
23px-Flag_of_Russia.svg.png
Russia Zenit Saint Petersburg Stadium
2008–09
23px-Flag_of_Ukraine.svg.png
Ukraine Shakhtar Donetsk
2009–10
23px-Flag_of_Spain.svg.png
Spain Atlético Madrid
2010–11
23px-Flag_of_Portugal.svg.png
Portugal Porto
2011–12
23px-Flag_of_Spain.svg.png
Spain Atlético Madrid
2012–13
23px-Flag_of_England.svg.png
England Chelsea
2013–14
23px-Flag_of_Spain.svg.png
Spain Sevilla
2014–15
23px-Flag_of_Spain.svg.png
Spain Sevilla
2015–16
23px-Flag_of_Spain.svg.png
Spain Sevilla

Hapo utaona kuwa timu za Spain zimeshinda kombe hili mara saba katika kipindi cha miaka 11. Hii haimaanishi kuwa nchi zingine ikiwemo England hazikupenda kushinda bali ni uwezo wa timu za Spain.

Ninajiuliza, hili linatufundisha nini katika mpira wetu Tanzania? Naona kuna mafundisho yafuatayo:
a) Siyo lazima mjitangaze sana ili kupata mafanikio: Ukijaribu kulinganisha na Uingereza wanaojitangaza zaidi katika vyombo vya habari, Spain inafanikiwa kuiteka Ulaya kimya kimya. Hii inamaanisha kuwa maneno matupu hayavinji mfupa
b) SpaiN ita dominate mpira wa Ulaya kwa muda mrefu: Mfumo uliopo wa kupata wachezaji Spain utaisaidia nchi hiyo kuiteka Ulaya kwa muda mrefu
c) Mpira wa Spain ni wa kuigwea kwa kuwa ni beautiful football: Tofauti na kwingineko, soka la Spain kwakwel ni zuri kuangalia na linaburudisha
d) Kuwekeza kwenye soka la watoto ni vizuri zaidi ili kujenga timu bora hapo baadaye: timu za Spain hasa Barcelona zimewekeza sana kwenye soka la watoto. Hii inawasaidia sana kuimarisha vilabu vyao na timu taifa pia

Asanteni
 
Ni sawa kabisa unavyosema kwamba Uingereza inapigia debe sana mpira wao wa kwenye Premier League, lakini La Liga ni ligi inayoongoza kwa ustadi wa wa mpira na ukuzaji vipaji vya watoto.

Ni jambo moja tu kubwa - mawasiliano ya meneja na wachezaji wake.

Makocha wa timu za Spain wanazungumza lugha moja na wachezaji wao na ukiondoa Diego Simeone Zinedine Zidane na Jose Mourinho ambao si wa kutoka Spain, mameneja wa timu za Spain na timu ya taifa wanazungumza vizuri na wachezaji na wanawachukuia kama watoto wao.

Hivyo watoto wakitoka kwenye Academy wanaendelezwa kwenda kwenye timu zao na wanakuwa wachezaji mahiri sana.

Fernando Tores aliwika sana Spain lakini alipohamia Engand akashindwa kule Liverpool na Chelsea lakini sasa yupo Athletico Madrid kidogo amerudia makali yake ingawa si kama mwanzo.

Uingereza mpira wao wameuweka zaidi katika biashara na mzunguko wa pesa lakini si katika kuukuza na kuutunza kupitia vijana wadogo.

Na ndio maana ligi zao ile ya PL na Championship au darajala kwanza zimejaa wachezaji wengi wageni au waingereza wenye asili ya mataifa mbalimbali.

Kwa sasa La Liga ndio ligi bora duniani na nasubiria Spain kunyakua kombe la ubingwa wa Ulaya kwa mwaka 2016.
 
Tunajivunia ligi ya uingereza labda kwa sababu ya lugha, lakini katika soka Uingereza si taifa la soka kabisa. Wanajivunia kuwekeza kwenye soka kwa wachezaji kutoka nje. Bara la Ulaya magwiji wa Soka ni Ujerumani, Italia na Spain. Mimi hupenda kuangalia La Liga (Spain) na Series A (Italy) na mara moja Bundesliga (Germany) kwa kuwa soka lao halipendezi kuangalia kwa jinsi linavyochezwa (nguvu nyingi ufundi kidogo). Ukipenda uhondo wa jinsi soka linavyochezwa kifundi, angalia s
 
Uwekezaji kwenye young talents na kua na falsafa moja ya mpira ambayo watoto wataielewa sana. Pia lazima kuwe na klabu ya taifa mfano kwa Spain Uwekezaji umechukua mda sana klabu ya Barcelona ndio chachu ya mafanikio kwa Spain. Falsafa Yao ya tiki taka imelifaidisha taifa Lao kwa ujumla. Wachezaji wengi wanaowika Spain ukifuatilia unakuta wametokea la masia. Wenzetu wajisacrifice leo hii wanakula bata tu.
 
We nawe Nina wasiwasi na hizi post yako yaonyesha hujui hata records za mabingwa 2006/2007 ac Milan ndo alikuwa bingwa liva ilichukuwa 2004/2005.
Na hizo stats ulizotoa zinaonyesha LA liga kuna timu chache bora uefa ni barca na real halafu Europa league ni sevilla tu kwa hiyo hizo zimedominate michuano yote. Mi kwa sasa sijui ipi ligi bora kwa sababu siwezi kukubaliana na kigezo cha mashindano ya uefa pekee yake Kama kigezo cha ligi bora tunapaswa tuvijumuishe na vigezo vingine vya ziada.
 
We nawe Nina wasiwasi na hizi post yako yaonyesha hujui hata records za mabingwa 2006/2007 ac Milan ndo alikuwa bingwa liva ilichukuwa 2004/2005.
Na hizo stats ulizotoa zinaonyesha LA liga kuna timu chache bora uefa ni barca na real halafu Europa league ni sevilla tu kwa hiyo hizo zimedominate michuano yote. Mi kwa sasa sijui ipi ligi bora kwa sababu siwezi kukubaliana na kigezo cha mashindano ya uefa pekee yake Kama kigezo cha ligi bora tunapaswa tuvijumuishe na vigezo vingine vya ziada.
Amechemka sana kwenye kumbukumbu.
Hata man u walichukua 2008/2009.
 
Kutawala kwa mpira wa ulaya ni mzunguko kuna zama ilikuwa Italy,ikaja England now Spain Wajerumani ndio wameweza ku-maintain kwenye era zote wao hawakupotea kabisa.Baadhi ya sababu za Spain kutawala na England kuchemsha soka la ulaya

1.Klabu za waingereza kuanza kumilikiwa na watu binafsi
Tangu huu mfumo umeanza umepunguza kabisa ushindani kwani wamiliki binafsi wao priority yao ya kwanza ni kupata faida na wadhamini mbalimbali ili wapate faida,hii imefanya klabu kutowapa makocha muda wa kutosha.Mafanikio ya uwanjani yamekuwa sio priority tena.Kuna timu zinanunua wachezaji ambao zinajua baada ya msimu mmoja au miwili watamuuza na kupata faida na kutojali mchango wa huyo mchezaji.Tumeona Liverpool,Newcastle na Manchester United wanavyopata tabu uwanjani lakini wanaingiza hela nyingi sana

2.England hakuna makocha wengi ukilinganisha na Spain/Italy/Germany
Wachezaji wengi waliocheza La Liga wengi baada ya kustaafu soka wamesomea ukocha na kuanza kufundisha kuanzia ngazi za chini na baadae wanapewa nafasi kwenye timu zao(Enrique,Simeone,Zidane, Guardiola,) na wengine kibao wanajihusisha na moja kwa moja na soka wakati England imekuwa tofauti kina Scholes,Caragher,Shearer,Lineker,McManaman,Campbell Le Tissier wameishia kuwa wachambuzi wa soka kwenye TV na wengine hawajishughulishi kabisa na soka
Kibaya zaidi wanakuja makocha wageni ambao inawachukua muda kuelewa lugha na utamaduni wa soka la England na wamiliki wa timu sio wavumilivu.Tumeona karibuni wataliano (Mancini,Ancelotti,Di Mateo,Ranieri) wamepata mafanikio wakati makocha wazawa wanaishia kuziokoa timu zishishuke daraja


4.Spain wana ma-scout wengi sana South America
Kuna connection kubwa kati ya nchi za South America na Spain na Portugal na wachezaji wengi kutoka South America (Chile,Uruguay,Brazil,Argentina,Paraguay) wanapenda zaidi kwenda Portgal/Spain sababu ya utamaduni unafanana,lugha na hali ya hewa.Messi,Aguero,Falcao,Neymar,James,Dani Alves wamepatikana kwa uraisi sana kwa sababu ya network ya ma-scout wao huko South America.Hata negotiation inakuwa rahisi kwao kupata mchezaji wa bei rahisi ukilinganisha na England ndio maana Sevilla,Valencia,Bilbao,Atletico kila msimu wanauza wachezaji then wanapata wachezaji wengine kwa bei rahisi na wanaendelea kufanya vizuri


Last point:Kuondoka kwa Sir Alex Ferguson ni big loss kwa soka la England
 
Serie A na bundasliga hamna kitu bora England. Angalia ni timu zipi Germany na Italy zimechukua UEFA CHAMPIONS zaidi ya bayern na ac millan na inter katika kipindi cha kuanzia 2005. Soka la Ulaya limepitia vipindi tofauti na kila kipindu Kuna nchi inadominate. Ni kweli kipindi hiki Spain imetawala soka la Ulaya. Kwa mtu aliyeanza kufuatilia soka miaka ya hivi karibuni atadhani Spain ipo hivi miaka yote kumbe sio.
 
Ni sawa kabisa unavyosema kwamba Uingereza inapigia debe sana mpira wao wa kwenye Premier League, lakini La Liga ni ligi inayoongoza kwa ustadi wa wa mpira na ukuzaji vipaji vya watoto.

Ni jambo moja tu kubwa - mawasiliano ya meneja na wachezaji wake.

Makocha wa timu za Spain wanazungumza lugha moja na wachezaji wao na ukiondoa Diego Simeone Zinedine Zidane na Jose Mouronho ambao si wa kutoka Spain, mameneja wa timu za Spain na timu ya taifa wanzungumza vizuri na wachezaji na wanawachukuia kama watoto wao.

Hivyo watoto wakitoka kwenye Academy wanaendelezwa kwenda kwenye timu zao na wanakuwa wachezaji mahiri sana.

Fernando Tores aliwika sana Spain lakini alipohamia Engand akashindwa kule Liverpool na Chelsea lakini sasa yupo Athletico Madrid kidogo amerudia makali yake inagwa si kama mwanzo.

Uingereza mpira wao wameuweka zaidi katika biashara na mzunguko wa pesa lakini si katika kuukuza na kuutunza kupitia vijana wadogo.

Na ndio maana ligi zao ile ya PL na Championship au darajala kwanza zimejaa wachezaji wengi wageni.

Kwa sasa La Liga ndio ligi bora duniani na nasubiria Spain kunyakua kombe la ubingwa wa Ulaya kwa mwaka 2016.
....km Tores angeshindwa Liverpool Chelsea wasingemnunua kwa lile dau!
 
Back
Top Bottom