Tujifunze: Nilivyoibiwa na fundi sitaki mwingine aibiwe

Mangi flani hivi

JF-Expert Member
Jan 2, 2016
2,026
3,107
Salam,

Juzi nilipata tatizo kwenye kibebi woka changu. Power window zilikuwa kama zimechanganyikiwa, ukishusha vioo vya gari nzima kwa kutumia batons za mlango wa dereva, vioo vinagoma. Ikabidi niende kwa fundi, fundi akaniambia nirudi jioni na gharama nzima ni elfu 55.

Kumbe lile sio tatizo ni kitu cha dk5 tu na kinasababishwa na kutoa betri kwenye gari na hivyo ukirudisha betri ni kama unatakiwa ufanye setting ndogo tu ya power window na saa kwenye gari, ambavyo vinakuwa kama vimevurugwa kwa zoezi la utoaji na uwekaji wa betri.

Cha Kufanya:
Una shush kioo kimoja kimoja kwa baton ya mlango wake, kisha unapandisha lakini ukipandisha unashikilia baton bila kuachia kwa at least 30sec. Hivyo tu na system nzima inarudi vizuri.

Nimelijua leo na hapa najiandaa niende kupachimba gereji.

Usiibiwe na wewe.
 
Kama huna ujuzi kuhusu tatizo linalokukabili, kuibiwa na fundi ni given. Lakini pia nimejifunza kuwa kumwamini sana fundi, haijalishi umefanya naye kazi kwa muda mrefu kiasi gani, nako ni chanzo kingine cha kuibiwa kwetu kirahisi. Mimi nilimwamini sana fundi akaishia kuniliza sh. 250,000 kijinga tu. Ilikuwa hivi:

Nilikuwa katika hatua za kupaua kibanda changu, nikawa nahitaji kununua mbao za kenchi. Fundi akanambia ana jamaa yake anauza mbao na tunaweza kuchukua kwake kwa bei nzuri. Siku tuliyopanga tukanunue mbao akanipigia simu akisema tayari ameshafika dukani na anaomba nimruhusu aanze kuchagua mbao ili kuokoa muda. Sababu ya kumwamini nikampa ''go ahead''.

Nimekuja kufika dukani nikaoneshwa muuzaji ili niongee naye kuhusu bei. Niliambiwa sh.5,500 kila ubao kwa mbao 250. Nimelialia kupunguziwa bei nikaambiwa mwisho kabisa nitoe sh. 5,000 kwa kila ubao, maana yake nilipe sh. 1,250,000 kwa mzigo mzima. Fundi akiwa anatusikiliza, naye aka-comment kuwa hiyo ni bei ya kawaida. Nikalipa tukachukua mzigo.

Mbao zilipopelea, akataka aende mwenyewe kule kule kuongeza mbao nyingine. Nikamkatalia na nikaamua kwenda mwenyewe sokoni. Nilikwenda duka jingine, nikafanikiwa kupata mbao aina na size ile ile kwa sh. 4,000 kila ubao. Maana yake kule pa mwanzo nilipigwa sh. 1,000 kwa kila ubao kwa jumla ya mbao 250 = 250,000.

NIMEJIFUNZA KUTOMWAMINI FUNDI YEYOTE HATA KAMA NI JAMAA YANGU KIVIPI!
 
Mkuu njoo nikuazime kijiko ukachimbe vizuri.. Hahahaaaaa
 
Mkuu, hata Kinyozi humuamini?
 
Back
Top Bottom