Adili Magayuka
Member
- Jan 14, 2015
- 5
- 2
TUJIFUNZE KUWAPENDA WENGINE
Nimeona watu wengi wakitoa matamko hasa baada ya kuumizwa au kuona wengine wakiumizwa, kua jipende mwenyewe kabla hujapenda wengine. Ni sahihi. Lakini ni lini unaanza kujipenda? Kwa muda gani kabla hujaanza kupenda wengine? Siku mbili, wiki, mwezi au miaka mingapi? Kipindi unajipenda mwenyewe utakua unawatendea vipi wengine?
Hakika kujipenda na kupenda wengine ni mapacha wasioachana. Ni vitu viwili vilivyo sambamba, hakuna kinachotangulia au kuanza. Ukidhani unaweza kujipenda mwenyewe pasipo kupenda wengine tutakuita mbinafsi. Wamefaulu sana wale wachache wanaopenda wengine (zaidi ya wanavyojipenda wenyewe, kwa mtazamo wa wengine) kwani tayari wanakua wameua ndege wawili kwa jiwe moja.
Amani kamili ya moyo hupatikana kwa kuwapenda wengine. Hapa ndipo ulipo mtihani mkubwa kwa baadhi ya watu, ni somo ambalo binadamu tunatakiwa kujifunza katika maisha yetu yote. Hujachelewa.
Kabla hatujaona ni namna gani tunaweza kujifunza kuwapenda wengine, ni vema tuone tafsiri ya kupenda (mtihani bila shaka!).
Mungu kupitia vitabu vyake vitakatifu katuagiza upendo. Lakini kwa kiasi kikubwa alituacha tutafsiri wenyewe. Na kwa kiasi kikubwa tumefanikiwa. Wapo waliotafsiri upendo kama kujali. Wengine wametafsiri kama ifuatavyo:
*kua na hisia za kimapenzi juu ya mtu fulani
*kulazimika kujali bila kuangalia maovu ya mtu (Agape love). Mungu anatupenda bila kujali dhambi zetu.
Mimi nitatafsiri upendo/mapenzi kama kumkabidhi mtu nguvu ya kuvunja moyo wako, lakini ukiamini kua hatauvunja, na kumpa nafasi nyingine pindi akiuvunja.
Unadhani haujafanikiwa kumpa mtu hizo nguvu? Kumuamini je? Basi fanya yafuatayo.
1: PANUA WIGO WA UELEWA JUU YA MAPENZI/KUPENDA
Mapenzi ni zaidi ya hisia. Ni zaidi ya mahaba. Ni zaidi ya kuhudumia familia. Kupenda kunamaanisha kujali hisia za watu wengine zaidi, sio za kwako. Ukielewa hili utafanya yale wanayotaka wao na sio unayotaka wewe katika njia sahihi.
Unampenda mama yako na ana mwaka anataka umpelekee mjukuu akamuone bila mafanikio? Unampenda mkeo ilhali anakushawishi kila siku uwahi kurudi nyumbani baada ya kutoka kazini? Jitazame upya.
2: TENGENEZA MTAZAMO CHANYA
Kuwapenda wengine ni ghali sana. Bahati mbaya sana ghali haiwezi kulipwa. Kwa hiyo usitegemee malipo (to be loved back) kwa unaowaonesha upendo. Timiza wajibu wako taratibu na baada ya muda fulani utazoea.
3: ONESHA UPENDO WAZI
Usifiche hisia zako, ingawa mwanzoni unaweza kulazimisha au kudanganya (fake). Shiriki katika vikundi vya kijamii, toa zawadi na tia moyo wale wanaohitaji. Usibague kwa imani wala kabila.
4: KUBALI CHANGAMOTO
Wapo watakaokuona kama unajipendekeza kwa watu. Hata utakaowaonesha upendo wapo miongoni mwao watakaohisi kuna kitu unategemea kutoka kwao. Usife moyo, upo ushindi mkubwa miguuni mwako.
Najua itachukua muda kuzoea, lakini kitu kikubwa na cha msingi ni kudumu katika kujaribu. 'Practice makes perfect' Ukifanikiwa katika hili utaweza kuishi bila kuvunjika moyo katika maisha (binafsi nimefanikiwa katika hili), utajiamini na kupata afya ya ubongo. Utaweza kumuelewa na kupunguza migogoro na mwenza wako, familia na jamii kwa ujumla.
Imeandikwa na:
Adili Magayuka
adilikitenga@gmail.com
Fb: adili magayuka
Instagram: @adilimagayuka
Whatsapp: +255(0)755 223 648