SHERRIF ARPAIO
JF-Expert Member
- Aug 25, 2010
- 9,539
- 5,923
Kwa akili yako unaamini Marekani anatetea wanyonge?
Marekani anatetea maslahi yake kwanza , nyie atawatetea kama mrija ukikaa vizuri.
Irak,Libya na Syria unafikiri wanaouwawa ni hawa viongozi wakuu.
Marekani kama mirija yake haiguswi hata uwe mnyanyasaji kama Mseven dhidi Besigye hatakugusa.
Juzi tu hapa Kabila ameua waandamaji zaidi ya hamsini umesikia marekani akishupalia ? Hawezi sababu mirija yake huko inatiririsha bila bugudha.
Ali Bongo ameua waandamaji kadhaa lakini Marekani yupo kimya sababu ndio maslai yake yalipo......hao jamaa inahitaji Diplomasia ya hali ya juu kudili nao sio kauli kama za akina Nape.
Kama tunahitaji kugusa maslai yao inabidi twende kuwaomba kwamba jamani tulegezeeni kidogo...
Sidhani kama kuna nchi yoyote ambayo haitakuwa na interests zake akikusaidia
Sio wamarekani tu hata wachina, wajapani, wahindi etc
Usipojisimamia Na kujikwamua mwenyewe basi utabaki kuwa mtumiwaji tu