Kwa kiasi kikubwa tumekengeuka kimtazamo na kutekwa na masham-sham ya kampeni. Tunatumia msuli mwingi kujadili vitu na watu badala ya masuala (issues). Sehemu kubwa ya mijadala yetu ya leo ni ile ya msimu itakayokoma 31 Oktoba. Tunasahau kuwa Tanzania itaendelea, uchaguzi utapita.
Siasa na maamuzi ya kisiasa kutegemea kwa kiasi kikubwa hisia na matakwa ya watu (preferences), au tabaka fulani katika jamii. Hadi sasa, mwenendo wa uchaguzi unaonyesha dhahiri kuwa hisia za watu zimewathibitisha Mhe. Kikwete na Mhe. Slaa kuwa wagombea wenye kuweza kutwaa kiti cha Urais. Hatutarajii muujiza utakaomwingiza madarakani Mhe Lipumba au Mhe Dovutwa. Hivyo, sioni kama ni busara kuelekeza nguvu zetu kuwajadili hawa wawili wanaosubiri uamuzi wetu tutakaoutoa Oktoba 31.
Kwa maoni yangu, ni wakati sasa wa kujadili mustakhabali wa nchi yetu ambao kwa kiasi kikubwa utaathirika (+ve and -ve) na maamuzi yatakayofanyika kati ya tarehe 3 hadi 30 Novemba, 2010 yaani uteuzi wa Baraza la Mawaziri; Mwanasheria Mkuu wa Serikali; Uchaguzi wa Spika; Wenyeviti wa Kamati za Bunge, Safu ya Wajumbe wa Kamati za Bunge (tumeona mchango mzuri wa kamati hizi katika chaguzi zilizopita, je tutaweza kuwa na safu nzuri 2010-2015?) na nafasi nyingine nyeti kama Ofisi Binafsi ya Rais Mteule (Marekani hapa ndipo watu hutolea macho). Watakaoshika nafasi hizi zenye dhamana kubwa wanaweza kwa kiasi kikubwa kutufanya tuendelee au kuturudisha nyuma.
Tujielekeze Wiki Tatu baada ya Uchaguzi; ni teuzi zipi zitakazosisimua na kuamsha tumaini jipya la Watanzania? Na ni teuzi gani zitakazokwaza na kufuta matumaini ya Watanzania?
Tanzania kwanza!