Tujiandae kikamilifu fursa hizo zinakuja from india

sirbuff

JF-Expert Member
Jun 19, 2016
487
263
Nadhani waziri mkuu wa India ana dhamira nzuri kwa Tanzania na rais Magufuli naye ameeleza jinsi gani ya kung'amua hizo fursa kutoka serikali ya India
 
Isije kuwa amekuja kumuombea yule Gabachori wa million 7 kila dakika.
 
Wakati wanajenga Bomba la Gesi Mtwara to Dar, walisema hivyo hivyo

Wakati wanawapa Wazungu migodi ya Dhahabu, walisema hivyo hivyo

Wakati Dangote anakuja, walisema Cementi bei nafuu

Katika Ahadi za Rais Wetu mpendwa JPM, ahadi zipi zimetekelezwa..

Ahadi ambayo ilipewa msukumo mkubwa kuwa ingetekelezwa ni punguzo la Vifaa vya ujenzi

Mikoa ya Morogoro, Dodoma na Shinyanga ni Ngome za CCM, ila ndo mikoa inayoongoza kwa nyumba za Tope (Tembe). Sasa asante kwa hawa wapiga kura ni nini?

Wakati Dangote Anakuja na wakati gesi inatolewa Mtwara....CCM walisema kwa sauti kubwa kuwa Cementi itakuwa 8000 Tshs kwa mfuko...

Sasa mbona hii ahadi imepotea? Au Hapa Kodi tu?

Raw material (Mali ghafi) kubwa inapatikana Hapa Tanzania......Nini sababu cementi inakuwa Ghali? Serikali inatoza kodi kubwa au Umeme ghali

Watanzania wanalipa Kodi PAYE, VAT on everything you buy, Na sasa VAT on Banking and Mobile Money

HAPA KODI TU....

Serikali itengeneze ajira mpya kwa vijana..

Nguvu kazi ya Taifa inapotea chini........

Ajira mpya zitaongeza kodi kwenye serikali na uchumi wa nchi utakuwa

Ni Hayo tu.....
 
Back
Top Bottom