kifupi kirefu
JF-Expert Member
- Oct 29, 2018
- 539
- 3,507
Watanzania yameletwa kwetu maneno matatu ambayo yanatoa tafsiri ya Tanzania ya kesho chini ya Chadema. Tujiulize maswali haya na tuyataftie majibu kabla ya siku ya kupiga kura.
1. Je, Tanzania hatupo huru? Kwanini tuamini baada ya miaka mingi ya kushangilia na kusherekea siku ya Uhuru bado sisi siyo huru? Uhuru gani tunataka kwa maana ya watumishi, wakulima,wafanyabiashara, wanafunzi na makundi mengine?
2. Haki ni neno gumu na zito kidogo, linapotajwa kwenye ilani ya chama maana yake wamebaini hakuna haki hivyo wanakwenda kuisimamia. Je, Tanzania hakuna haki? Nani anayetakiwa kutoa haki na kwanini ataki kuitoa hiyo haki? Tutaipate na tutajuaje kwamba tumeipata?
3. Maendeleo. Dunia yote inataka maendeleo ila maendeleo endelevu....je tunakosa maendeleo au tunakosa maendeleo endelevu? Nini wanataka kukifanya kuleta maendeleo? Ila pia yapo maendeleo ya watu na maendeleo ya vitu, je tunayo yote au kimoja hakipo? Kipi tunatokosa?
CHADEMA wameleta Jambo hili kwetu, tulijadili