Hii Mada ni tamu kwani nami ni Addicted wa Smart equips.
Nlinunua Samsung Smart TV Series 6 LED 40" lakini Cha ajabu sikuweza kuifaidi kwani unapotumia Internet zetu za kibongo,inakuwa inastaki sana. Huinjoi vizur.
Nlichokifanya, nlilazimika kununua Streaming Device
#1 Duniani, "ROKU3" hapo ndio nkajua kuwa Watu wanaoishi ulimwengu wa kwanza Mungu amewabiriki kwa Kila Kitu. Huwezi amini ukiwa na hiki kifaa, unaweza ukaangalia Movie Iliyozinduliwa hii leo tena kwa Pesa Kidogo $3 hadi $5, ukilinganisha na bei ya kwenyeKumbi zetu za Cinema.
Unakuwa na access ya kuangalia Movie zaidi ya One Milion,nyingine nyingi zikiwa za bure kabisa.
Pia upande wa Music ndi Usiombe, ziko channels kama VEVO/Pandoro/Spotify/YouTube n.k
Kwa kifupi, haka kadubuasha kazi kinachofanya na umbo lake ni vitu viwili tofauti.
Upande wa Bei, pale Ebay/Amazon wanakiuza kwa bei ya $99 tu. Lakini thaman yake inazidi hiyo hela.
Cha kufurahisha,Remote yake unaweza chomeka Earphones na uka-mute sauti wakati wa usiku ukiwa unaangalia Movie ili usidistabu wengine.
Angalizo: Ukinunua haka kadubuasha(ROKU3) uwe na Uhakika wa Internet yenye Speed anzia 2Mbps. Pia lazima TV yako iwe na Port ya HDMI.