Tujadili mechi ya Simba Vs Yanga leo

Sajenti

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
3,651
412
Zikiwa zimebakia tabribani saa 8 ili ule mpambano wa watani wajadi Simba na Yanga ufanyike, kumekuwa na tambo za kila aina kutoka pande zote mbili. Kinachonifanya nione mpambano wa leo kuwa mtamu si tu kuwa Simba na Yanga wanacheza bali ni aina ya mechi ya leo. Kwa mujibu wa kanuni za mashindano ya Tusker hii ni hatua ya nusu fainali hivyo leo vyote vyote iwavyo lazima mtu apigwe bao ili apatikane mshindi wa kuingia fainali hatimaye kukutana na Sofapaka ya Kenya. Hilo ndio kubwa linalofanya pambano la leo kuwa tamu tofauti na mengine tuliyozoea ambapo timu zikitoka sare ndani ya dakika 90 kila mtu anaenda nyumbani na maumivu nusu. Leo mpaka kieleweke.

Mimi binafsi naipa Simba nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi ndani ya dakika 90. Piga uwa mnyama atatafuna kandambili 2-0.
 
Unaota wewe mchana kweupe

Oktoba 31 ulisema hivyohivyo naona hukomi tu. Mechi ya leo itaisha kwa sare ya moja moja halafu itaenda kwenye matuta ambapo simba atashinda kwa penati nne kwa tatu. Kaseja atafuta mbili.
 
Mechi ya leo haina matuta ni dk 90 tu Mnyama chaliiiiiiii mbona leo unajua kabisa Jangwani wanashinda
 
Zikiwa zimebakia tabribani saa 8 ili ule mpambano wa watani wajadi Simba na Yanga ufanyike, kumekuwa na tambo za kila aina kutoka pande zote mbili. Kinachonifanya nione mpambano wa leo kuwa mtamu si tu kuwa Simba na Yanga wanacheza bali ni aina ya mechi ya leo. Kwa mujibu wa kanuni za mashindano ya Tusker hii ni hatua ya nusu fainali hivyo leo vyote vyote iwavyo lazima mtu apigwe bao ili apatikane mshindi wa kuingia fainali hatimaye kukutana na Sofapaka ya Kenya. Hilo ndio kubwa linalofanya pambano la leo kuwa tamu tofauti na mengine tuliyozoea ambapo timu zikitoka sare ndani ya dakika 90 kila mtu anaenda nyumbani na maumivu nusu. Leo mpaka kieleweke.

Mimi binafsi naipa Simba nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi ndani ya dakika 90. Piga uwa mnyama atatafuna kandambili 2-0.

I have watched these teams kwenye mechi zao za Tusker, Simba have been good kama walivyo kwenye ligi.

Yanga have improved a lot baada ya kocha kukaa na wachezaji muda mrefu, so I would say both teams are good but Yanga wana njaa zaidi ya ushindi in terms of pride coz last time walifungwa.

I will go for Yanga win during 90 minutes, but if it goes to penalties Simba will win it.
 
Mi nahesabu masaa tu nikae kwenye kiti kirefu nasherekea ushindi
...Mi mbona nimeshaanza kusheherekea ushindi mazee?? Hapa nilipo nameza nyara ndogo ya tatu minazini. Ni uhakika kabisa mnyama anafanya kweli..Poleni sana wateja!
 
Hehehe najua tumbo lako hapo unahisi kushusha vitu na vitu vinagonga kwa boxer vinarudi we subili.
 
Mechi ya leo ndio fainali, kuna uwezekano wa watu kula sikuu ya x-mas huku wakiwa na simanzi kubwa, record iliyowekwa na simba mpaka naandika huu ujumbe ya kutopoteza mechi toka mwaka huu uanze ni ishara tosha kabisa kwamba; Leo mnyama lazima atafune ndala na kushushia na uji wa yeboyebo,
 
Zikiwa zimebakia tabribani saa 8 ili ule mpambano wa watani wajadi Simba na Yanga ufanyike, kumekuwa na tambo za kila aina kutoka pande zote mbili. Kinachonifanya nione mpambano wa leo kuwa mtamu si tu kuwa Simba na Yanga wanacheza bali ni aina ya mechi ya leo. Kwa mujibu wa kanuni za mashindano ya Tusker hii ni hatua ya nusu fainali hivyo leo vyote vyote iwavyo lazima mtu apigwe bao ili apatikane mshindi wa kuingia fainali hatimaye kukutana na Sofapaka ya Kenya. Hilo ndio kubwa linalofanya pambano la leo kuwa tamu tofauti na mengine tuliyozoea ambapo timu zikitoka sare ndani ya dakika 90 kila mtu anaenda nyumbani na maumivu nusu. Leo mpaka kieleweke.

Mimi binafsi naipa Simba nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi ndani ya dakika 90. Piga uwa mnyama atatafuna kandambili 2-0.
Tegete na Ngassa wana uchu wa magoli hao....Leo Simba mtakiona...Canavarro mwenyewe anamaliza ....ni full ulizi....I hope YANGA 4 SIMBA 0....
 
Yanga walie tu, Fainali ni Simba na Sofapaka, maana hawa ndo wanaofahamu kuucheza mpira na si haoNgamiawakaa jangwani.Sasa leo watanyeshewa na mvua ya magoli.
 
Back
Top Bottom