Tujadili kuhusu HESLB

Elai

Senior Member
May 26, 2011
150
7
Habari wana JF? Tutafakari kuhusu mafanikio ya bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu katika utekelezaji wa mapendekezo ya tume iliundwa na raisi JK kutafiti mfumo bora wa utoaji wa mikopo. Uundwaji wa tume ulitokana na migogoro/maandamano/migomo isiyokwisha vyuoni kutokana na mfumo mbovu wa utoaji wa mikopo.Kutokana na utekelezaji wa mwanzo wa mapendekezo ya tume,je dawa ya kumaliza tatizo imepatikana?tunaishauri ni wizara husika?
 

CR wa PROB

Senior Member
Sep 21, 2011
170
29
Wao ni zuri, lakini taifa limechakachukuliwa kwani kwenye kuundwa kwa ille tume ya akina Prof Maboko watanzania walitangaziwa kuwa tume imeundwa, lakini kwa uzembe wa hali ya juu sidhani kama hao Watanzania walitangaziwa kuhusu majibu ya ile tiume so tunaweza kusema kwamba Makenya Maboko amegalagaza heshima yake kama wakati ule alipopewa ile tume ya Baraza la mitihani.

Na sidhani kama kuna mtanzania yeyote asiyejua matatizo ya hii bodi ya mikopo na kwa mda mwingine huwa nakaa na kuwaza kuwa huwa serikali yetu haielewi hata maana ya kumkopesha mtu. Na endapo wakiendelea na ule utaratibu wao ni vyema tufanye mpango wa kuifanyia hii bodi Nomeclature mpya kwani haina maana yeyeote ya kuiita bodi ya mikopo huku walalahoi wa kitanzania hawapati huo mkopo ambao wataurudisha ipasavyo.

MUNGU IBARIKI AFRICA, MUNGU IBARIKI TZ, MUNGU IBARIKI BODI YA MIKOPO.
 

Kebara

Member
Oct 2, 2011
9
1
HESLB nahic hawajal maisha ya wanafunz! Mi wameninyima mkopo ' wakat vigezo vyote ninavyo! Kisa nimechaguliwa second selection! Wakat mkopo niliomba mapema tu! Cjui wanafil nitaish vip chuon? Vyuo vyenyewe husajiliw mpak nusu ada itoke! Huna uhakika wa pesa, hapo kuna kusoma kweli? Tangu mwanzo walijua idad ya wanao taka mkopo, wamefanya wanayojua ili kutuumiza! Et bajet haitosh wakat wanapanga kumlipa dowans mabilion! Inakatisha tamaa na watoto wa wakulima hatutasoma kwa mwendo huu.
 

Apollo

JF-Expert Member
May 26, 2011
4,902
3,077
Mimi sitaki hata kulisikia hivo jina. Marafiki zangu wamekosa mkopo wakati wana vigezo vyote.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom