TUJADILI IGA KIFUNGU KWA KIFUNGU

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
9,219
6,650
Mode tafadhali msiunganishe bandiko hili ili makubaliano/mkataba (IGA) tuujadili kifungu kwa kifungu ikizingatiwa wahusika: Serikalini (Mwanasheria Mkuu na Wizara husika) na Bunge, wamekuwa wakitoa majibu ya jumla jumla yanayohusu faida ya uwekezaji bandarini kuliko madhara ya IGA kwa Taifa.

Mimi nitaanza na kifungu kinachohusu IGA kurekebishwa, wakati umekwisha kuridhiwa na Bunge, kama ulivyo tayari umesainiwa na pande zote, JMT na Serikali ya Dubai.

KIFUNGU CHA 22: MAREKEBISHO YA MKATABA
Mkataba huu unaweza kurekebishwa wakati wowote, kwa maandishi, kwa
makubaliano ya pande zote za Nchi Wanachama. Hakuna marekebisho ya Mkataba huu yatakayotumika bila makubaliano hayo kwa kutia saini na kuridhiwa na/au kupitishwa kwa hati zinazofaa na Nchi Wanachama.


Kwa uelewa wangu, swali kuhusu nafasi yetu kufanya marekebisho ya vifungu visivyo na maslahi kwa Taifa, ni pale mkataba unapohitaji makubaliano ya pande zote kurekebishwa: Je, Serikali ya Dubai ikikataa marekebisho au rekebisho lolote lile litalopendekezwa na JMT?
 
Back
Top Bottom