Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,681
- 149,880
Niliwahi leta mada hapa ya kumpongeza Mhariri wa hili gazeti na timu yake kwa kazi kubwa ya kizalendo ya kufichua maovu ya baadhi ya wakubwa waliopewa dhamana katika nchi hii.Kila toleo la hili gazeti ni tuhuma nzito nzito za vigogo serikalini na katika mashirika ya umma na cha ajabu na kushangaza ni kuwa mpaka leo hii hakuna hata mtuhumiwa mmoja aliewahi kulipeleka gazeti hili Mahakamani(kama yupo nisahihishwe).
Sasa wadau swali langu ni hili:Kama serikali itakuwa inafanyia kazi taarifa za gazeti hili,hii itakuwa inaleta picha gani ili hali tuna vyombo vyenye jukumu hili kwa serikali?
Kama serikali inapata taatifa hizi,kwanini haichukui hatua mapema mpaka taarifa hizi zinafika kwenye vyombo vya habari?
Je,si kweli kuwa ingependeza zaidi kama mpaka taarifa hizi zinafika kwenye vyombo vya habari watuhumiwa hawa wanakuwa teyari mikononi mwa vyombo vya dola?
Mbona hii "trend" haifiki mwisho?