Tuitafsiri vipi serikali ya ccm katika hili la magamba?!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuitafsiri vipi serikali ya ccm katika hili la magamba?!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by shizukan, Dec 3, 2011.

 1. shizukan

  shizukan JF-Expert Member

  #1
  Dec 3, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Nimesoma front page ya Mwananchi ya leo kwenye mtandao, kuna habari za CCM kuunda kamati ya nidhamu ya chama kushughulikia 'magamba' yaliyogoma kuvuka kwa hiyari. Kiini cha hoja yao ni 'utuhumiwa wa ufisadi' na wengi wa watuhumiwa ni 'viongozi wa serikali na wastaafu wa umma'

  soma habari hapa

  Kinachonishangaza ni kuona CCM wako bize kuwaondoa hawa ndugu zao katika chama lkn kasi ya kuwaondoa ktk serikali haipo. Readding between the lines, nia ni kukinusuru chama kwa wananchi na wala sio uadilifu wa chama kwa wananchi. Hapa ninamaanisha kuwa, naona kwamba CCM inafanya hivi kwa sababu tu wananchi wanapiga kelele lkn bila ya hivyo wao wenyewe kama chama hawako committed kwa nchi na uadilifu wao ni wa kusukumwa na heka heka na hofu za kukosa ushindi ktk uchaguzi ujao tu.

  Kama CCM inaamini kuwa wanachama wake wanaotajwa ktk RADA, EPA, RICHMOND, KAGODA na kwingineko wana hatia, mbona serikali ya chama hicho hicho haioni hatia kwa watumishi wake hao ktk mambo wanayohusishwa nayo?

  Ina maana intelijensia ya Kamati ya Maadili ya CCM ni bora zaidi kiasi itaweza kuwatia hatiani watuhumiwa ambao intelijensia ya serikali imeshindwa kuwapata na makosa?


  Wakati mamlaka za sheria za nchi yetu hazina ushahidi wa kuwatia hatiani waliohusika na maajabu ya RADA, wabunge wa Uingereza na Kamati ya Maadili ya CCM wanao ushahidi na tayari Kamati ya Maadili ya CCM inataraji kuanza kazi ambayo intelijensia ya nchi imeshindwa. Ninachojiuliza mimi: serikali hii ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inaundwa na nani?
   
Loading...