Tuisaidie Serikali yetu ya Tanzania, kila mwananchi soma hii

PastorA

JF-Expert Member
Jul 14, 2016
361
275
Kimsingi nimesukumwa kutoka ndani kuanzisha uzi huu, kwa kila mtanzania hii itamhusu, tujifunze kuipenda serikali yetu na nchi yetu kiujumla. Sina maana ya kuwagawa kivyama au kiitikadi isipokuwa NAOMBA KILA MTANZANIA UNAEMFAHAMU MTU AMBAE NI POTENTIAL KWA TAIFA LETU yaani kama unajua mtu aliyegundua kitu chchte mfano, aliyegundua na kutengeneza engine ya pikipiki au chochote, au mtu aliyebuni chchte ambaye anastahili kuendelezwa.

Naomba tuwaorodheshe humu kwa majina yao na namba zao za simu na kazi zao (walicho kitengeneza) ili kuisaidia serikali kulifanyia kazi jambo hili. Maana imeonekana tuna Wataalam wengi Tanzania ambao bado hatuna watumia.

Napenda kuwasilisha watu wa Serikali kama mkiona hii ina tija naomba muifikishe kwa Mh. Rais na tutafutane, nitakuwa huru kuwapa ushirikiano juu ya hili.

TANZANIA TUNAWEZA KUWA NA VIWANDA TUKIJITATHMINI WENYEWE KWANZA."INAWEZEKANA"

Karibuni kwa hoja
 
Sayansi ni moja kwa dunia nzima. Tuna watu wengi sana wanaoweza kutumia ujuzi walionao kulisaidia taifa kufanya mapinduzi katika uzalishaji mali na kutoa huduma.
Tatizo lililopo ni zile fikra potofu (hasa kwa viongozi) kuamini wageni wa nje kuliko watu wao.
Hatuhitaji kuanza kuwaza mambo makubwa sana, tuanze na madogo madogo kama kuwapa wenye nchi kazi zote za ukarabati na matengenezo wanazoziweza.
Adui mkubwa wa mwafrika ni mwafrika mwenzake, na zaidi viongozi wasioanzia chini.
Kuendeleza nchi ni rahisi kwa wanaojua hali halisi. Hata hivyo, viongozi wengi wanajua nadharia tu.
 
Back
Top Bottom